Jaribio la kuomba hela

Lady of Destiny1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2019
Posts
588
Reaction score
869
Hhahahaa uwi dunia in mambo jamani acheni tu

Basi buana juzi Kati natoka dar-dom kwenye siti nimekaa na mtu mzima Sana, no stori Hadi tunafika,mbele Kuna kijana wa makamo ambaye kwenye kiti hatulii Ni Kama anatamani Mzee akaye mbele yeye arudi nyuma tukae wote (wabadilishane),Kila baada ya dakika mbili ananiangalia.
Muda mwingine ikabidi anisemeshe kabisa ,Mambo vipi Safi ,tumefika msamvu tunashuka akasema vipi Safari yani kwa vyovyote anatamani kuongea na Mimi ila nafasi ikakosekana.

Tumefika Dom tunashuka akahakikisha anakaa nyuma yangu wakati wa kushuka akanisalimia vipi waelekea wapi nikamwambia ahha nashukuru nimepata mwenyeji ,unaondoka kwa usafiri gani nikasema boda boda ,tuchukue tax au bajaji usijali nitalipia naenda maeneo hayo hayo unayoenda,ok,sawa nikajibu

Akaita usafiri hao ,njiani naitwa Henry waitwa Nani ,naitwa lady of destiny unafanya kazi wapi nikamtajia ,aah buana nimeamishiwa dodoma uwe mwenyeji wangu daah maisha sijui yatakuwaje basi ghafla nikamwambia Mimi nimefika ok ,basi naomba mawasiliano Mana ofisi uliyopo ndo na Mimi nimehamia,japo nilikuja kujua yupo sehemu nyingine kubwa.

Ok ok bye bye
Kesho badae simu za kutosha ananiuliza unaish wapi,kazi,na maisha yangu kwa ujumla ,nimekupenda na Nini na Nini hivyo
Sasa nikamuuliza familia iko wapi kasema dar ok nikajua huyu tayari Ni mume wa mtu ,ok njoo tuende lunch,njoo sijui tuende wapi,nikagoma Kila nilichoombwa naomba one night nipo tayari kukupa chochote,hutajutia maamuzi yako , tule maisha bwana
Yani ningekuwa mhuni ningemmaliza ,anapiga simu mara zaidi ya 20 per day,usipopokea unaenza kuta mced Cal hata 15 akianza kukutumia sms ukiandika moja kashaandika tano,njoo hapa hotelin nimekumis Yani maneno mengi , ikabidi nimwambie nina familia na Mr kafuma sms zake akapowa kidogo,

Tukaenda hivyo Nikaona hakati tamaa ,ghafla nikamtext sorry naomba uniazime elfu 50 nimepata dharura (sikuwa na shida )ila nilitaka tu kumkimbiza Mana nilishachoka na Sina tabia ya kutembea na watu wenye familia zao

Hadi Leo hiyo sms haijajibiwa ,sijajua kama alikufa au yupo hai
 
Hahahaaaa mtu anayefanya kaz nyeti hawezi kukosa elfu 50 hata ya kukopa.

Pia aliahid atakupa chochote sasa amekwama wap mzee baba
 
Mshahara jana wameweka kwa akaunti,mkumbushe tena leo labda atatuma.niko
 
Mshahara jana wameweka kwa akaunti,mkumbushe tena leo labda atatuma.niko
Hhh bahati mbaya sikusave namba yake na sms nili clear,I wish hata anitafute nimkumbushe ombi langu
Ila ndo hivo sijui kapatwa na nini
 
Hata siku moja, ila pia usiwe na pesa za mawazo maana utajutia kwa siku nyingi, nafikir jamaa kawaza familia yake inavyooiitaji hizo elfu 50, dah genye zikaisha ghafla [emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wanaume:Kazi kweli kweli unaamishwa mkoa unaohamia unataka danga wakati home umeacha mama watoto ,hivi mkojeee
 
Sasa bora ni yupi kati ya hao 2 uliokutana nao kwenye bus?? Kile kizee kilichokula kobis au huyo domo kaya aliyekubwagiza maneno ya ulaghai ili tu akutoe pichu?
Basi mshukuru yule mmbabu kwani alikaa kwa hishima japo moyoni akiugumia ka mmeza quinine au muarobaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…