Jaribio la kombora la korea kaskazini lafeli

kwalele

Member
Mar 18, 2013
36
15
Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wamesema jaribio la kombola la korea Kaskazini limefeli kwani kombola hilo lilianguka punde tu mara baada ya kupaa angani.Maafisa wa Marekani wamesema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka,hii ni ishara kwamba korea Kaskazini haina ujuzi wa kutosha kiteknolojia ama pia huenda ikawa Marekani imepata mbinu ya kuingilia mifumo yake ya teknolojia.Gazeti la the Newyork Times limesema kwamba Marekani imeweka virusi kwenye kompyuta za kijeshi za korea kaskazini.
Maafisa wa korea kusini na Japani wamekashifu vikali majaribio hayo
 
Huyu kiduku ni chizi. Hivi hajui kama anazidi kuharibu mazingira? Anadhani ni mawe ya manati yale? Sasa akapojaribia tena limlipukie yeye mwenyewe na wenye akili kama zake ili watkaosalia wapte akili. Jamaa utadhani linaish kwenye sayari nyingine.
 
Kama hayo yanakuwa guided na mifumo ya satellite kuwa interfered na marekani inakuwa nje nje.Technologia kwa sasa na hao NK hawana uwezo wa kuwekeza kwenye research wanategemea wataalamu wa ndani tu
 
Mkuu acha kupost habari za uongo ,

Media za south Korea zinasema kombora lililorushwa limefanikiwa ns haijafeli Bali walilipua tu makusudi "Detonation"

Mods futeni Uzi au rekebisheni
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Huyu kiduku ni chizi. Hivi hajui kama anazidi kuharibu mazingira? Anadhani ni mawe ya manati yale? Sasa akapojaribia tena limlipukie yeye mwenyewe na wenye akili kama zake ili watkaosalia wapte akili. Jamaa utadhani linaish kwenye sayari nyingine.
Jaribio halijafeli

Kwa mujibu wa south Korea jaribio limefanikiwa ila walilipua makusudi "Detonation"

Mtoa thread sijui taarifa kaipata wapi ,wakati media za south zinasema jaribio halikufeli
 
Mkuu acha kupost habari za uongo ,

Media za south Korea zinasema kombora lililorushwa limefanikiwa ns haijafeli Bali walilipua tu makusudi "Detonation"

Mods futeni Uzi au rekebisheni
Hizi ni habari zako
Maana kila mtandao wanasema hivyo
Af kwa akili yako mtu atalipuaje ballisticmissile atatumia combora gan kulifukuzia
 
Marekani na washirika wake wanajiaminisha kwa mataifa kuwa wao ni zaidi lakini ki ukweli wao wenyewe wanajua kwa NK wamechemka na wanaonyesha uoga
 
Back
Top Bottom