Japo ni muathirika lakini ananipenda vilivo

Sumah

Member
Feb 29, 2016
23
13
Habari zenu wakuu. Ninarafiki yangu nampenda sana ni msichana mmoja mtulivu sana kwanzia nyumbani kwao, shuleni mpaka ugenini. Ila ni muathirika Wa virusi vya ukimwi ugonjwa huo alizaliwa nao. Ni binti mdogo tu miaka 24 sasa na ni binti ambaye ni mrembo hapana mfano. Kuna kijana mmoja ambaye anamfualia kwa muda Wa miaka5 sasa mpaka sasa rafiki yangu ajamkubalia hataki kuwaribia watu maisha yao na alimueleza ukweli kuwa yeye ni muathirika Wa virusi vya ukimwi lakini jamaa amekazana tu anampenda hivo hivo na yuko tayari kumuoa ata sasa ila best kagoma. Na si kijana mmoja tu wapo wengi wanaomuhitaji ila anawakataa .

Mnamshaurije kuhusu yule kijana anaehitaji kumuoa ...?
 
Hivi inakuwaje mtu anamng'ang'ania muathirika na mbaya zaidi anajua kabisa kuwa mwenzie kaungua tayari?

Binafsi nimeshuhudia kijana mdogo akimuoa mdada aliyeathirika.
Na dogo alikuwa anaambiwa ila ndio hasikii wala haoni!
Hatari sana.
 
Huu ni unyanyapaa
HIV ni condition ssio ugonjwa
na wataalam wanazo njia za kushauri watu wanaotaka mahusiano na watu ambao ni HIV positive

Hakuna mtaaaalam aliesema ni kosa kuoa au kuolewa na mtu HIV positive..

Dunia nzima watu wanaoa na kuolewa na watu HIV positive..sio jambo jipya
mradi mfuate wataalam wanacho shauri
 
Hivi inakuwaje mtu anamng'ang'ania muathirika na mbaya zaidi anajua kabisa kuwa mwenzie kaungua tayari?

Binafsi nimeshuhudia kijana mdogo akimuoa mdada aliyeathirika.
Na dogo alikuwa anaambiwa ila ndio hasikii wala haoni!
Hatari sana.
INAONEKANA UNA ASILI YA UNYANYAPAA HATARI
 
Wanaweza kuoana, wanachotakiwa kufanya ni kwenda kwa dr na kuelezwa jinsi ya kuish safe life ili familia iweze kusonga mbele
 
Tauche unyanyapaa, nani anayejua sehemu anayopita kuna nini?Ninao ushahidi wa waliooana HIV+ na HIV- na mpaka leo wapo salama kabisa, waliamua tuu kutozaa
 
Amkubali waende kwa wataalamu wa afya wataelekezwa namna ya kuishi wala wasijal muhimu ni upendo wa dhati
 
Sina unyanyapaa lakina siwezi kumuoa muathirika wa HIV sina uhakika 100% kuwa sintakuja kuathirika na hili gonjwa lakini nisubiri kwanza I'm to young to die early ingawa kifo kipo kwa namna mbalimbali lkn naamini Mungu bado ananilinda.
 
Mapenzi ni kitu cha ajabu sana binafsi inanishangaza...

Ila vijana wa siku hizi atataka amfumue na ndomu then atoke nduki ataanza kusema hamna future
 
I think the best course of action is for them to go get tested together, as it will help clear out some uncertainty, and save the guy some major grief. The big question being..............."Does he really want to be with her despite the poz status or is he simply in denial, assuming HIV is just being used as an excuse ya kunyimwa tunda?"
 
Sina unyanyapaa lakina siwezi kumuoa muathirika wa HIV sina uhakika 100% kuwa sintakuja kuathirika na hili gonjwa lakini nisubiri kwanza I'm to young to die early ingawa kifo kipo kwa namna mbalimbali lkn naamini Mungu bado ananilinda.
Inshallah atazidi kukulinda,namtangulize mbele kwenye kila jambo lako inshallah..
 
Hivi inakuwaje mtu anamng'ang'ania muathirika na mbaya zaidi anajua kabisa kuwa mwenzie kaungua tayari?

Binafsi nimeshuhudia kijana mdogo akimuoa mdada aliyeathirika.
Na dogo alikuwa anaambiwa ila ndio hasikii wala haoni!
Hatari sana.

Duh..hata wewe
 
Back
Top Bottom