Japo kazi ya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga kila kitu. Kwenye maslahi ya taifa, tutangulize utaifa, tuwe wamoja, wakweli na tusipotoshe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi,

Huu ni muswada wa makala ya gazeti.

Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazungumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.

Hitimisho
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee lugha moja kwa sauti moja.

Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja. Wito kwa Serikali: Ikubali Kusikiliza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi. Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
 
Hahaha, kaka umekosea kusema wasipinge bila kujali wanapinga nini, Umoja wa kitaifa siyo lazima wakubali mambo ya rais aliyepo madarakani, inawezekana yote yakawa ya hovyo, hivyo sioni kwanini wasiyapinge yote kwa maslahi ya taifa.

Na ukweli unapimwaje kaka, maaana wewe umesoma sheria, How do you measure the Truth?

Utaifa ndio unafanya wanapinga mambo ya hovyo hovyo yanayofanywa na mtawala aliyepo madarakani.

Lini umesikia wakenya wakipingana na hoja za JPM, au lini umesikia waganda wakilalamikia maamuzi ya mahakam za tanzania, au tume ya uchaguzi, au ukandamizaji wa polisi Tanzania?

Yote yanayolalamikiwa hulalamikiwa na watanzania, na hiyo ni kwa sababu ya utaifa wao, na uzalendo kwa nchi yao.

Ni ajabu kumuacha mtu afanye mambo ya hovyo hovyo TANZANIA hii usiyakemee au kuyakataa kabisa halafu ukawa mzalendo.

Uzalendo ni kuweka maslahi ya wengi na taifa mbele, Siyo ubinafsi na dhuluma.

Sasa tunapotoshwa, na tunapinga kwa nguvu upotoshaji huo, tunaambiwa sisi sio wazalendo, eti mpotoshaji ndiye mzalendo.

Tunaambiwa tumuamini tu, bila hata yeye kutuambia anafanya nini kwa nini?

Ni vyema akawa transparent KWA MASLAHI YA TAIFA, Jiulize kwanini mikataba haiendi bungeni, kwanini manunuzi yasiyo na maelezo yanaamishiwa ofisi ya rais?

Kwanini watanzania wasi hoji mali na rasilimali zao?

Uzalendo ni nini au lina maana gani kwako?

Utaifa ni nini kwako, na umoja na ukweli ni nini au vina maana gani kwako mleta mada?
 
Pascal Mayalla kabla ya kuendelea na uzi baada ya lepe, nikukumbushe jambo

Upinzani ''opposition'' ni wanaopinga, lakini kazi yao si kupinga bali kuwa mbadala

Hivyo kazi ya upinzani ni mbadala ambao hugeuka kupinga pale kunapokuwepo na hoja za chama tawala na Upinzani.

Ni hoja ndizo zinazaa kupinga lakini si kazi yao kupinga bali kutumia mbadala unaozaa kupinga
 
Usitutoe kwenye reli please, bado tupo kwenye mjadala wa kutumbuliwa kwake Steiner February The Rope
 
Nilipoona heading tu nikajua nikifungua nitakutana na habari za ACACIA.
Na kweli imekuwa hivyo
 
Uliwahi kumuuliza Rais kuhusu utawala wa Sheria, akakujibu kuwa maana ya Mayala ni njaa. Leo bado unajikomba na kujibaraguza na sasa unawatetea mabeberu Barrick, be independent of who you are.
 
Uzalendo sio kumkubali rais aliepo wala matendo yake, hatulazimishani, uzalendo utakuja wenyewe automatically, tangu gogoro LA masisiemu lianze mada kama hizi ni miyeyusho sana!
 
Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Mkuu Pascal Mayalla kwenye hilo la class A na B nakuomba upitie ufafanuzi huu.

Kwenye swala la kuwa listed DSE nafikiri serikali ina nafasi ya kukataa pendekezo hilo lakini Barick wao wamesema kwenye hiyo draft kwamba wasilazimishwe kuwa listed DSE.
Kama walivyosema hawatowajibika kujenga mtambo wa kuchakata makinikia hapa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…