Japan yatoa bilioni 116/- Bajeti 2016/17. Wizara ya fedha yasisitiza miradi ya REA ipo salama

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SERIKALI imesaini hati mbili za makubaliano na Japan, yatakayoiwezesha Tanzania kupata Yen za Japan bilioni sita ambazo ni sawa na Sh bilioni 116.4 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha bajeti ya mwaka 2016/2017.

Akizungumza wakati wa kutia saini na kubadilishana hati za makubaliano, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hati ya kwanza ya mkataba huo, ina lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini na kuongeza kasi ya uzalishaji wa ajira.

Alisema hati ya pili ni iliyosainiwa mwaka 1966 ya Wajapani waliokuwa wakija nchini kwa ajili ya kufanya shughuli za kujitolea, hivyo imerekebishwa kwa kuweka neno Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili waje kusaidia katika sekta za afya, elimu na sekta nyingine Tanzania Bara na Visiwani.

Aidha, Dk Likwelile alisisitiza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka Marekani za Changamoto ya Milenia (MCC-2), hakutaathiri miradi iliyokuwa ikiendelea, ambayo ni pamoja na Mradi wa Umeme Vijijini (REA) kwa kuwa fedha hizo hazikujumuishwa katika bajeti.

“REA haiwezi kuathirika kwa sababu hizo fedha za MCC-2 hazikuwa kwenye bajeti, lakini tungeshukuru kama tungezipata kwa sababu zingeongeza uwezo na kufanya uboreshaji,” alisema Dk Likwelile.

Hata hivyo, aliwataka Watanzania kuhakikisha kila mmoja anashiriki katika kuwezesha miradi ya maendeleo kwa kulipa kodi na kutoa taarifa juu ya wanaokwepa kodi ili nchi ijitegemee.

Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida alisema Serikali ya Japan itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kutengeza ajira hasa katika sekta binafsi kwa kupunguza gharama za kufanya biashara na kutengeza mazingira mazuri kwa viwanda.

“Serikali ya Japan ina nia ya dhati ya kuendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli na serikali yake katika maono yake ya kujenga viwanda na kutengeneza ajira pamoja na kuwavutia wawekezaji wa kigeni kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara,” alisema Balozi Yoshida.

Balozi Yoshida aliongeza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Japan unaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo na kwamba utasaidia kuongeza ukuaji wa uchumi na kijamii.
 
nimependa sanaaa kwan ushrikiano uo ni mzuri sanaaa lakin wasije kwa lengo lingne tofauti na hilo kwani Tanzania ni nchi changa sanaaa kulinganisha na nchi yenyeweee.Ivyoo wakija kwa lengo lakusaidia na kuhuudumia kwa maendeleo Mungu awabariki sanaaa.
 
“REA haiwezi kuathirika kwa sababu hizo fedha za MCC-2 hazikuwa kwenye bajeti, lakini tungeshukuru kama tungezipata kwa sababu zingeongeza uwezo na kufanya uboreshaji,” alisema Dk Likwelile.
 
Bora sasa tujitegemee kwa misaada ya Japan wakikataa nao tunajitegemea tena na misaada hata ya india.
 
Si mlisema mnataka kujitegemea? Hii tena misaada ya japan rea na china inatoka wapi? Au japani na china siyo nchi za nje? Pumbavu kweli kweli! Ccm ni mauti kwa taifa.
 
“REA haiwezi kuathirika kwa sababu hizo fedha za MCC-2 hazikuwa kwenye bajeti, lakini tungeshukuru kama tungezipata kwa sababu zingeongeza uwezo na kufanya uboreshaji,” alisema Dk Likwelile.
Tanzania kwa sanaa sasa hivi tunatisha! REA lazima iathirike na virus kwa sababu bajeti kubwa ya vijijini ilikuwa inatoka MCC, sasa mtasemaje iko salama? kuna umeme wa jua walikuwa wanatoa Fedha kwa asasi (LRTC 2016) mpaka sasa hivi wako kimya maana fedha hakuna! Wauadanganye majitu majinga kama jingalao!
 
Si mlisema mnataka kujitegemea? Hii tena misaada ya japan rea na china inatoka wapi? Au japani na china siyo nchi za nje? Pumbavu kweli kweli! Ccm ni mauti kwa taifa.
Huu si msaada... Ni mkopo wenye masharti nafuu... Unlike MCC...
 
Huu si msaada... Ni mkopo wenye masharti nafuu... Unlike MCC...

Kipi bora? Huu si zaidi ya ushenzi huu? Nchi imelemewa na madeni, halafu mijitu isiyokuwa na uchungu inaona ni heri kutesa watu na kuwazidishia madeni badala ya kufuata misingi ya utawala wa haki kwa maslahi ya taifa na kupata msaada wa kusukuma maendeleo mbele huku ikijipanga kujitegemea.

Ninaona hapa ccm ni zaidi ya shetani kweli!.
 
Umenena...tusubiri haya 'mashetani' yatatuambia nini baada ya EU nayo kusitisha budgetary support ..... Each a tuwe wazalendo na kufa njaa au kula nyasi ...
 
Sasa kumbe mnataka misaada? Yaani kuwaelewa wapiga debe wa Ccm inahitaji uwe kichaa ndio mtaelewana.
Huku mnasema hamna haja na pesa za MCC huku mnapokea hela za mkopo toka Japan. Watanzania tunatakiwa kupuuza maneno w
Ya hawa wana mtandao wa Lumumba maana hawajui wafanyalo.
 
Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida alisema Serikali ya Japan itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kutengeza ajira hasa katika sekta binafsi kwa kupunguza gharama za kufanya biashara na kutengeza mazingira mazuri kwa viwanda.

“Serikali ya Japan ina nia ya dhati ya kuendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli na serikali yake katika maono yake ya kujenga viwanda na kutengeneza ajira pamoja na kuwavutia wawekezaji wa kigeni kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara,” alisema Balozi Yoshida.

Je kufungwa kwa ofisi za MCC Tanzania ni wafanyakazi wangapi watakuwa wamekosa ajira??

Serikali wanapaswa kutueleza hili ni jinsi gani watazilinda ajira zao ndugu zetu hawa waathirika.

"KWANI MCHEZO WA KURUSHA MAWE KATIKA DIMBWI NA WEWE UNASHANGILIA MAJI YANAVYOLIA "TUBWI" UJUE WANAATHIRIKA VIUMBE WAISHIO MAJINI KWANI UNAWAPIGA NA MAWE YAKO"
 
Back
Top Bottom