Japan yamwaga Bil.2.9 sekta ya afya, utalii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Japan yamwaga Bil.2.9 sekta ya afya, utalii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280


  [​IMG]

  SERIKALI Japan imetoa kiasi cha shilingi billion 2.9 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na utalii nchini.

  Jana serikali ya Tanzania na Japan walitia saini kwa pamoja mikataba hiyo ambapo waliotia saini mikataba hiyo ni Balozi wa Japan nchini, Hiroshi Nakagawa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Tanzania, Ramadhan Khijjah, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Khijjah alisema misaada hiyo ya kutoka Japan ni katika muendelezo wakutoa misaada nchini kupitia shirika lale la misaada ya maendeleo la JICA.

  Khijjah alifafanua kuwa, kati ya fedha hizo shilingi. bilioni 2.07 ni kwa ajili ya kupambana na ukimwi na zilizosalia shilingi. milioni 862 zitatumika kuboresha kituo cha maelezo cha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

  Alsiema fedha hizo wka upande wa afya zimelenga kuboresha huduma za upimaji afya ya ukimwi kwa hiari na kuongeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV).

  Kwa upande wa Balozi Nakagawa alisema kuwa, msaada huo utaweza kusaidia kuboresha hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya ushirikiano kati ya nchi Japan na Tanzania.

  Alisema kituhicho kikiweza kukamilika kitaweza kuongeza idadi ya watalii kutoka Japanna kwingineko

  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  tunaishi kwa kutegemea Misaada toka nje mpaka lini jamani? Nchi imeoza jamani ehhhhhhhhhhhh
   
Loading...