January usilalamike, huo ndio ubatizo wa moto ambao mzee wako aliunadi hadharani kuwa utafanywa na bwana mkubwa

Naogopa kuamini kama kale kautamaduni wetu wa kupokezana vijiti baada ya 10 yrs kataendelea tena
Subiri ujionee akitumbuliwa ..Anachokifanya Joka la mdimu ni kummeza kila mtu ambaye anaonyesha kuwa ana nguvu ya ushawishi ambayo inaweza kumtoa katika kiti chake. ....So ndio ameanza rasmi sasa ...Bwana Hahahahahahahahah dah CCM kume Pamba moto
 
Nimeikumbuka kauli...."anayeondoka aliwabatiza kwa maji"...ajaye atabatiza kwa moto"...
Kuna maandiko ambayo hayatakiwi kunakiliwa na kuradidiwa bila tafakuri ya kina kutokana na uumbaji wake.
Maneno huumba kwa wale wanaoafiki hili huweka hadhari kubwa sana na akiba ya maneno yao.
Kuna maneno yakisemwa husukuma matokeo kwa kasi ya ajabu sana na hivyo kuyatumia kunahitaji utayari wa kupokea matokeo halisi.
 
.
IMG-20190721-WA0015.jpeg
 
Jana ilikuwa niguse ninuke leo ubatizo wa moto
Hii kasi ya misimu ya kisiasa ni ya aina yake.
 
Wakati awamu ya tano inaingia madarakani, mzee Makamba alijtokeza mara kwa mara kwa madai kwamba Rais aliye pita alibatiza kwa maji ila huyu aliyekuja atabatiza kwa moto, Makamba alijaribu sana kunuu vifungu kutoka katika biblia takatifu kuaminisha umma wa watanzania kuwa utawala huu ni chaguzi za mbingu, baadhi ya watanzania walikemea sana lugha aliyo itumia mzee Makamba kuwa haikuwa bora, kwa kufananisha kazi inayoweza kufanywa na mbingu ukaipeleka kuwa ya uwezo wa kibinadamu, leo tunashuhudia akiwa anaupitia ubatizo aliousifia sana yeye mwenyewe.
Watanzania wengi walipiga kelele kuhusu mwenendo wa viongozi wetu kuwa sio mzuri na una muelekeo wa kuwagawa watanzania , lakini matokeo yake yalikuwa ni kubezwa, nambuka kuna muda fulani Mheshimiwa Tundu Lissu alisema, kuwa CCM mnafurahia wapinzani wanavyo shughulikiwa kwa manyanyaso makubwa , ila akimaliza kwa wapinzani atarudi kwenu na ndicho kinacho fanyika.
Napenda kutoa pole kwa mzee Makamba na wenzake wanaopitia huo ubatizo ambao nimemsikia Lusinda akitamani sana wakamatwe na kuhojiwa.
Jambo la uwazi na ukweli ni kwamba CCM inampasuko ambao umesababishwa na kundi la vijana na wahamiaji ambao pia wameingia huko kwa kujipendekeza na kujali matumbo yao huku wakichukua nafasi za wafia chama.
Chonde chonde wazee wastaafu fanyeni harakati za kukiokoa chama lasivyo 2020 tutaitosa.
 
Mchimba kaburi kaingia mwenyewe Mungu endelea kutulipia waliotuletea shida Bila wao tusingebomolewa nyumba zetu,wala kufukuzwa kazi Kwa shida za vyeti
 
Back
Top Bottom