January Makamba ni mzigo usiobebeka

January Makamba ni mzigo usiobebeka

busaraza2015

Member
Joined
Jul 30, 2014
Posts
22
Reaction score
9
Pamoja na kujitangaza sana katika media (magazeti, tv na radio) na kwenye mitandao ya kijamii, January Makamba bado ameshindwa kuonyesha mvuto wake katika utendaji, kijana huyu anayejiona MSOMI wa juu sana amekuwa ni katika wabunge wa CCM ambao raisi Kikwete amewaweka serikalini kwa shinikizo la wapambe (baba yake Mzee Makamba).

Itakumbuka kwenye baraza la mawaziri la kwnza kabisa pamoja na matarajio makubwa kabisa, mh Raisi ailimuacha January kwenye uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri, hili lilikuwa pigo kwa familia yake na yeye mwenyewe.

Lakini hata baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri wa mawasialiano, technolojia na sayansi baada ya mabadiliko yaliyofanya na mh raisi, January ameendelea kubaki kwenye wizara akiwa akama naibu waziri kwa kipndi chote cha uongozi wa Mh Kikwete.

Tumeona wabunge wenzake vijana na wazee ambavyo wamekuwa wakipata nafasi ya kupanda ama kubadilishiwa wizara mara kwa mara....yeye palepale tu na inasemekana hata hapo alipo ni mzigo.

Wapo wasiojua kwamba hata January kuondolewa ikulu kama msaidizi wa raisi ilikuwa ni baada ya kuonekana hana uwezo na amekuwa ni mzigo kwa raisi, ndipo kumpooza wakamsaidia kuingia bungeni kwa gharama kubwa.

Eti sasa anataka kuwa raisi wa nchi hii, jamani!
 
kwani kina nape walipozunguka na kusema mawaziri mizigo ccm mliwafanya nini
 
Ni nani kati ya watendaji ndani ya CCM si mzigo kwa taifa kama si chama ?
Ziara za Kinana zinajenga CCM au yeye Urais ?!
 
Raisi mtarajiwa asietaka kusikia maoni ya wapiga kura wake watarajiwa, amechemka...
 
Suala la miundombinu ya usafirishaji ni lazima tulipe umuhimu wa kipekee. Uchumi wa nchi unaendeshwa na miundombinu ya usafirishaji. Kihistoria hakuna nchi iliyoendelea duniani bila ya mapinduzi katika usafirishaji na uchukuzi. Reli na bandari zina uwezo mkubwa kuchangia Pato la Taifa na kuchochea shughuli za uchumi na biashara huko mikoani na hata nchi jirani.

Watu wengi hupenda kuongelea kuhusu reli ya kati na bandari ya Dar es Salaam. Na swali lako ni wazi limejikita hapo hapo. Hata hivyo, tukitaka maendeleo ya kasi na sawia na tukitaka biashara ishamiri katika maeneo yote nchini lazima tuitazame na tuishughulikie miundombinu ya usafirishaji nchini kama mfumo mmoja.

Kwa hiyo, kwa upande wa bandari, lazima tuziongelee bandari zote muhimu kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, bandari kubwa za Mtwara, Tanga na Dar es Salaam, Unguja na Pemba na bandari ndogo za Lindi, Kilwa, Mafia, na Pangani. Lakini pia lazima tuziangalie na tuzizungumzie bandari katika maziwa yetu matatu makubwa: katika Ziwa Victoria, bandari kuu ya Mwanza, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma; katika Ziwa Nyasa, bandari za Itungi, Manda, Liuli na Mbamba Bay; na katika Ziwa Tanganyika, bandari za Kigoma na Kasanga. Mimi nimepata bahati ya kufika katika bandari zote hizi za maziwa yetu haya matatu.

Nafahamu kwamba kuna biashara kubwa sana inafanyika na watu wengi wanazitegemea bandari hizi lakini miundombinu na udhibiti katika bandari hizi si wa kuridhisha. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kama viongozi, tusijisahau tunapoongelea bandari basi ni bandari ya Dar es Salaam tu. Kazi ipo kubwa ya kuufanya mfumo mzima wa bandari zetu na muunganiko wa bandari hizi na reli zetu, barabara zetu na viwanja vyetu vya ndege kuwa mfumo thabiti na wa kutegemewa wa miundombinu ya usafirishaji nchini na katika ukanda wa maziwa makuu.

Vilevile, kutokana na jiografia ya nchi yetu, miundombinu ya usafirishaji, hasa bandari, reli na barabara, ni muhimu kuitazama kwa mtazamo wa kikanda. Tunao wajibu wa kuwaunganisha na kuwawezesha majirani zetu ambao hawana bahari kufanya biashara ya kimataifa kwa ufanisi kupitia bandari zetu. Kwa bahati nzuri, wajibu huu tunapoutimiza ipasavyo, sio tu majirani zetu wananufaika bali na sisi pia tunapata ongezeko la ajira, mapato na masoko ya bidhaa zetu.

Nchi yetu imebahatika kuzungukwa na nchi 8 zikiwa majirani zetu na kati ya nchi hizo, ni nchi mbili pekee, yaani Kenya na Msumbiji, ndizo zenye ufukwe wa bahari. Hakuna nchi nyingine yoyote katika eneo la Maziwa Makuu au katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo imepata bahati kama hii. Hapa tuna fursa mbili. Fursa ya kwanza ni ya kufanya biashara na hawa majirani zetu wengi. Fursa ya pili ni hawa majirani kutumia bandari zetu, reli zetu na barabara zetu kufanya biashara na mataifa mengine duniani.

Hii ni biashara kubwa sana. Miaka mitatu tu iliyopita, biashara ya usafirishaji wa mizigo kupitia Tanzania (transit trade) ilikuwa inaingiza mapato kwa Serikali yanayokaribiana na mauzo ya nje ya mazao ya kilimo ambacho tunahangaika nacho kila siku.

Vilevile, kwa kuwa shughuli ya kupitisha bidhaa, yaani transit trade, yenyewe ni biashara kubwa, ni muhimu kuitazama miundombinu ya usafirishaji kwa mtazamo wa kiushindani. Kwa maana kwamba bandari zetu za Tanga na Dar es Salaam zinashindana na bandari nyingine katika ukanda huu. Kwa mfano, kwa sasa, majirani zetu wa upande wa kaskazini, wametengeneza Korido ya Usafirishaji ya Kaskazini (Northern Infrastructure Corridor) inayounganisha bandari za Mombasa na Lamu na nchi za Rwanda, Uganda na Burundi, Kongo, Ethiopia na Sudani ya Kusini kwa barabara, reli na bomba la mafuta. Ni dhahiri kwamba miradi hii, ambayo utekelezaji wake unaenda kwa kasi, itatoa ushindani kwa Korido ya Kati, inayotegemea kwa kiasi kikubwa Bandari ya Dar es Salaam na Reli ya Kati. Tusipokuwa makini, na tukaharakisha upanuzi na uboreshaji wa reli na bandari zetu, bandari yetu na reli yetu itakuwa ni kwa ajili ya mizigo ya Tanzania tu na tunaweza kukosa kiasi kikubwa cha fedha ambacho sasa tunapata kwa biashara ya kupitisha mizigo kwa ajili ya nchi za jirani.

Bandari ya Dar es Salaam, licha ya malalamiko yaliyopo, licha ya changamoto zilizopo, bado 2012 ilitengeneza faida ya takribani shilingi bilioni 40. Sidhani kama kuna kampuni yoyote hapa nchini, ya umma au ya binafsi, iliyotengeneza faida ya kiasi hiki. Na licha ya changamoto zilizopo, bado inapitisha mizigo ya thamani ya dola za Kimarekani bilioni 15 kwa mwaka, ambazo ni karibu ya nusu ya Pato la Taifa. Kwa mujibu wa utafiti wa Benki ya Dunia, tukiiboresha kidogo tu bandari ya Dar es Salaam, angalau ikafikia ufanisi wa bandari ya Mombasa, uchumi wetu utanufaika kwa kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 1.8 au sawa na asilimia 7 ya Pato la Taifa. Jambo hili linawezekana bila gharama kubwa. Ufanisi unaweza kuongezwa kwa kuondoa ushuru usio na lazima, rushwa katika upitishaji wa mizigo, kupunguza milolongo ya usafirishaji mizigo na kutumia teknolojia za kisasa katika usafirishaji na upakuzi wa bidhaa. Baadhi ya haya mambo yameanza kufanyika na mabadiliko yameanza kuonekana ingawa kasi inahitajika.

Kimsingi tunayo fursa ya kunufaika zaidi kuliko ilivyo sasa. Lakini ni lazima kuimarisha miundombinu ya bandari na reli, sio tu katika Korido ya Kati, bali ni lazima pia kuitazama bandari ya Tanga na reli ya Tanga Kilimanjaro. Miundombinu hii ambayo ni muhimu sana katika ustawi wa Kanda ya Kaskazini ina nafasi kubwa ya kushindana na bandari ya Mombasa na Lamu nchini Kenya. Lazima tuangalie namna ya kuifufua reli ya Tanga-Kilimanjaro na kuharakisha mpango wa kuifikisha kwenye bandari ya Musoma katika Ziwa Victoria inatekelezwa.

Bandari ya Mtwara inafaidika na upanuzi mkubwa na matumizi mapya ambayo yanatokana na uchumi wa gesi na viwanda vikubwa vinavyojengwa na vinavyotarajiwa kujengwa huko. Kuhusu Bandari ya Bagamoyo, hii ikikamilika itakuwa ni bandari kubwa kuliko zote mashariki mwa Afrika ikishindana na ile ya Durban ya Afrika Kusini. Itasaidia sana kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam ambayo baada ya miaka michache ijayo itafikia ukomo kwa kukosa nafasi zaidi ya kupanuka. Kwa hiyo ni muhimu kujenga bandari hii kama tunafikiria kukidhi mahitaji ya Taifa miaka zaidi ya 50 ijayo.

Wananchi wa mikoa ya Pwani, Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Rukwa na Katavi wanategemea usafiri wa reli kwa uchumi wao. Tukiiacha reli yetu iwe goigoi maana yake tumewasahau hawa wenzetu katika mikoa 10. Treni ya reli ya kati ni muhimu irudishe safari zake za kila siku. Hata hivyo, reli hii inabidi ifumuliwe na kujengwa upya kulingana na kiwango cha kimataifa, yaani standard gauge.

Mkakati huu umeshaanza lakini kuna haja ya kuongeza kasi ya utekelezaji. Shirika la Reli linabidi lipate mtaji mkubwa wa kujiendesha kifanisi kabla ya kutazama ni jinsi gani ya kushirikisha sekta binafsi. Reli ya TAZARA nayo inahitaji maboresho makubwa na menejimenti imara ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Tanzania ni nchi ya nne Afrika katika soko la usafiri wa anga. Ufanisi wa sekta muhimu ya utalii unategemea sana kutengemaa kwa usafiri wa anga. Kuna mjadala wa haja ya Serikali kuendelea kumiliki Shirika la ndege la Taifa. Cha msingi sio umiliki, cha msingi ni uhakika wa usafiri wa anga. Biashara ya usafiri wa anga ni biashara ngumu yenye gharama kubwa za uendeshaji lakini faida ndogo. Uendeshaji wa shirika la ndege unahitaji nidhamu kubwa sana ya kibiashara na hasa matumizi ya fedha nidhamu ambayo bado kama Serikali hatujaifikia. Tunahitaji wabia wa uhakika na wenye nguvu kubwa na uzoefu wa biashara hii ili tuweze kushirikiana nao kufufua na kuendesha Shirika letu la ndege huku nasi tukiwa na umiliki. Pia, ni vyema kuyaunga mkono mashirika ya ndani na ya wazalendo, na hata ikiwezekana Serikali nayo iwe sehemu ya umiliki. Tumeona mafanikio ya kufungua anga kwa mfumo wa ushindani kwamba usafiri umeimarika zaidi na bei zimeendelea kushuka. Kwa hiyo tuendelee kukaribisha ushindani katika sekta hii, na kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa katika kanda zote katika nchi yetu, na kuimarisha viwanja vya ndege vya mikoa.

Serikali ya Awamu hii ya Nne, imepata mafanikio makubwa sana katika kujenga barabara kuliko awamu zilizopita. Barabara hizi zimefungua fursa zaidi, hasa katika mikoa ya pembezoni mwa nchi yetu na kuweza kuunganisha mikoa yote ndani ya mfumo wa barabara za kitaifa. Awamu inayofuata ni kuunganisha wilaya zote nchini kwa barabara za kiwango cha lami na kupanua barabara za taifa kuwa barabara mbili (dual carriageway).

Kwa ujumla, nchi yetu inahitaji uwekezaji wa takriban dola za Kimarekani bilioni 2.5 kwa mwaka katika miaka 10 ijayo ili kufikia malengo yetu kwenye miundombinu na kuendana na kasi ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi. Fedha hizi zote sio lazima zitoke kwenye bajeti ya Serikali. Ujenzi wa miundombinu ni shughuli inayovutia sekta binafsi na kote duniani miundombinu mikubwa inayohitaji fedha nyingi haikujengwa na bajeti za Serikali, ilhali hapa hapa kwetu kwa sehemu kubwa inapata fedha kutokana na kodi tunazotoza watu kutoka kwenye mishahara yao na biashara zao ndogondogo. Tukiendelea hivi hivi tutachelewa sana. Tunahitaji falsafa mpya ya namna ya kugharamia ujenzi wa miundombinu hapa nchini ili kukidhi kasi ya ukuaji wa uchumi wetu.

Hatuwezi kuendelea kutegemea misaada ya wahisani kujenga miundombinu kwani misaada haina uhakika na imekuwa inapungua mwaka hadi mwaka. Mwaka 1973, katika misaada iliyokuwa inatolewa na wahisani, asilimia 50 ilikuwa inaenda kwenye ujenzi wa miundombinu, sasa hivi imeshuka na kufikia asilimia 10. Miaka ya nyuma, Rais Mkapa alifanya uamuzi mzuri wa kutumia fedha zetu za ndani kujenga miundombinu. Tumepata mafanikio makubwa, hasa kwa upande wa barabara. Lakini kwa kuwa tuna mahitaji makubwa ya huduma za kijamii, kama vile afya, maji, elimu, ulinzi na usalama huduma ambazo sekta binafsi bado haina interest nazo Serikali inabidi iongeze chachu ya kukaribisha uwekezaji wa sekta binafsi kwenye ujenzi wa miundombinu mikubwa, kama ilivyo kwenye nchi nyingine ili fedha zetu chache za bajeti tuzielekeze kwenye mahitaji mengine muhimu ya watu wetu kama vile madawa, malipo ya walimu, madaktari, askari wetu na huduma nyinginezo. Dhana kwamba ni Serikali pekee ndio ina wajibu, uwezo na haki ya kujenga miundombinu ya usafirishaji imepitwa na wakati. Sekta binafsi ya ndani au nje ya nchi ikijenga bandari, bandari hiyo haitangolewa bali itabaki nchini na kulinufaisha taifa. Mfano mzuri ni utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambao umefanikishwa kwa haraka baada ya Serikali kuingia ubia na mbia (NSSF) ambaye ameleta mtaji mkubwa na weledi katika utekelezaji. Kwa hiyo, sekta binafsi inapotaka kushirikiana na Serikali kujenga au kugharamia ujenzi wa miundombinu isikatishwe tamaa au kuwekewa vikwazo bali iwezeshwe tukizingatia tija na maslahi ya Taifa ya sasa na baadae.

Fursa nyingine muhimu sana ni kutumia maendeleo katika masoko ya kifedha duniani katika kugharamia miundombinu mikubwa. Serikali inabidi kuharakisha utekelezaji wa mipango ya kuuza hati fungani ya taifa, yaani Sovereign Bond, katika masoko ya kimataifa na hati fungani za Halmashauri, yaani Municipal Bonds, ili kutoa fursa ya kupata mikopo ya muda mrefu kugharamia ujenzi wa reli zetu, barabara zetu, madaraja yetu, viwanja vyetu vya ndege, na bandari zetu kwa uharaka zaidi kuliko kutegemea makusanyo ya kodi huku tukiipunguzia Serikali mzigo wa riba unaotokana na mikopo midogomidogo ya muda mfupi kutoka soko la ndani.

Kwa ujumla uongozi wa sasa wa Wizara ya Uchukuzi ukishirikiana na Hazina unafanya kazi nzuri katika kuleta marekebisho kwenye sekta ya uchukuzi. Lazima watiwe moyo ili waongeze kasi na ufanisi.


January Makamba.com
www.tanzaniampya.com
 
aaah! uyu msambaa bhanaa!!

tangia lini msambaa akawa rais
 
Back
Top Bottom