mkude kibwana
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 348
- 27
Hivi ndivyo Janury Makamba anavyouzungumzia mfumo wa utoaji haki nchini.
Mambo yote katika nchi yanaweza kwenda kombo, lakini mfumo wa utoaji haki ukiharibika, nchi inaingia hatarini. Watu hustahili na hupenda kupata haki zao. Tumeweka Mahakama na taasisi nyingine za umma kwa ajili hiyo. Ikiwa hazifanyi kazi vizuri, ikiwa hazitoi haki kwa wakati na kwa usahihi, siyo kwamba watu wataacha kutafuta haki zao, bali watazitafuta kwa namna wanayojua wao, na tukifika huko nchi inaweza kuvurugika.
Kwa hiyo taasisi kama Polisi na Mahakama lazima ziwe zinafanya kazi vizuri na tena kwa uadilifu wa hali ya juu sana. Sasa hivi hali siyo nzuri. Kila mtu anaona.Masuala ya kubambikiwa kesi yamekithiri. Masuala ya kuoneana yapo mengi.
Haki ni suala la msingi wala halipaswi kuonekana kama ni la upendeleo. Msingi mkuu kwenye mfumo wa utoaji haki ni kwamba sote tuko sawa mbele ya sheria, au kwa Kiingereza wanasema equality before the law. Kwa sasa siyo hivyo. Ukiwa ni mkubwa au una pesa unapata haki zaidi, unapata dhamana kwa urahisi, kesi yako inaenda haraka, na wakati mwingine inaamuliwa kwa namna unavyotaka. Hii siyo sawa na ni lazima ibadilike.
Kesi za watu zinazopelekwa mahakamani lazima zimalizwe haraka. Na lazima watu wawe na uhakika wa kesi zao kuamuliwa kwa haki. Mahakama zimepewa nguvu kubwa na nguvu hiyo ni vema itumike vizuri. Mfumo wa jinai na dhamana unahitaji marekebisho makubwa. Takriban nusu ya watu waliopo katika magereza yetu hapa nchini leo hii sio wafungwa bali ni mahabusu.
Wakati mwingine, mahabusu inaonekana ndio njia ya mkato ya kukomesha mtu. Lakini mara nyingi mfumo wa dhamana unapelekea kuwa na mahabusu wengi zaidi. Lakini kubwa zaidi ni ucheleweshaji wa kusikilizwa kesi za jinai. Kesi nyingi za jinai kwenye Mahakamu Kuu zinachelewa kusikilizwa kutokana na ukosefu wa fedha. Na wakati mwingine mahabusu anakaa ndani miaka 7 au 8 halafu anaonekana hana hatia au Mkurugenzi wa Mashtaka anaondoa mashtaka na mtuhumiwa anakuwa amepoteza kila kitu bila fidia yoyote.
Ni vema sasa kukawa na a criminal bench, yaani Mahakama ya Jinai, kama ilivyo Mahakama ya Ardhi, Mahakama ya Kazi, na Mahakama ya Biashara, ambayo inafanya kazi kila siku, ili haki za watu zipatikane haraka. Kupatikana kwa haki za watu kusitegemee uwezo wa kifedha wa Serikali.
Labda la mwisho dogo, lakini naamini ni muhimu, ni kwamba ukiangalia kwenye kesi za madai utaona zimewekewa viwango, kwamba kesi ikiwa ni ya zaidi ya milioni 100 kwa fidia au milioni 50 kwa mali zisizohamishika, yaani fixed assets, inasikilizwa na Jaji, kwenye Mahakama Kuu. Msingi hapa ni kwamba kuna kesi kubwa na kesi ndogo.
Lakini ukienda kwenye jinai unakuta kwamba Hakimu ana uwezo wa kumfunga mtu hadi miaka 30. Mimi nadhani kwamba kesi ambazo zinaweza kupelekea vifungo virefu kama miaka 30 nazo pia zisikilizwe na Jaji wa Mahakama Kuu kwa sababu tunashuhudia mara nyingi huko Wilayani watu wanafungwa miaka mingi, tena kirahisi sana. Kifungo chochote inabidi kiwe na uhakika kabisa kwamba kesi ilikuwa ya uhakika na haki halisi imetolewa.
Mimi naamini kwamba mfumo wa utoaji haki nchini lazima uwe imara zaidi.Majaji, mahakimu, mawakili wa Serikali, waendesha mashkata na watumishi wote wa mfumo wa utoaji wa haki ni muhimu wathaminiwe na wapate nyenzo zote muhimu za kuwawezesha kutimiza majukumu yao vizuri na kwa ufanisi.