January Makamba kawalipua wala rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January Makamba kawalipua wala rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ground Zero, Apr 20, 2012.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeikuta hii kwenye facebook page yake kuhusu rusha katika mchakato wa ubunge wa Afrika Mashariki.

  "Asanteni sana kwa maoni yenu mengi iliyotoa katika Facebook Status yangu niliyoweka juzi kuhusu uchaguzi wa wabunge EALA: Kwa faida ya wengi, narudia maelezo yangu ya ziada niliyoweka chini ya Status ile maana nahisi wengine hawakunipata vizuri:

  Napata ujasiri wa kusema yaliyojiri kwasababu sijachukua rushwa hata siku moja. Nimeumbwa na kiburi cha kukataa kununuliwa. Hata wagombea walijua hivyo Ndio maana hakuna aliyejaribu kunishawishi kwa fedha.

  Taarifa zilifika TAKUKURU lakini Hakuna hatua iliyochukuliwa. Kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ni tabia iliyojengeka kwenye jamii yetu ya kutaka vitu au mafanikio kwa njia ya mkato. Pamoja na kuimarisha taasisi za kutafuta na kupata haki, lazima utamaduni wa haki, ukweli, maadili, na uchapakazi uanzie kwenye mioyo yetu na kwenye familia. La sivyo, hata TAKUKURU ikiwa na Ofisi kwenye kila mtaa na kila kijiji, rushwa itaendelea kushamiri.

  Naambiwa wapo wahadhiri vyuo vikuu wanaomba rushwa ya ngono kuwapa gredi nzuri watoto wa kike. Rushwa ipo mahakamani, vyuoni, polisi, sekta binafsi. Tujitazame sote.

  Binafsi nataraji kuanzisha mpango mahsusi ifikapo mwezi Juni kutoa mchango wangu binafsi kupambana na Kansa hii.

  Asanteni sana, JM".
   
 2. a

  akelu kungisi Senior Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeipenda. Huyu jamaa ana tofauti kubwa sana kimtizamo na babake, labda abadilike hapo baadaye
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  January Makamba kuna taarifa kwamba hata wewe uliupata ubunge kwa njia ya kumwaga fedha za rushwa kutoka kwa mafisadi ili kumuondoa Wiliam Shelukindo kulikoni leo umegeuka mpambanaji wa rushwa? Inatoka moyoni au una mission mbele unasafisha barabara mapema kuondoa tope na mashimo uweze kupita vizuri?

  Kumbuka mzee shelukindo wakati huo alikuwa adui mkubwa wa mafisadi kutokana na tume ya Mwakyembe.

  Tuhuma nyingi za kukemea ufisadi zimekupita ukiwa kimya leo kulikoni? Ni baada ya pepo baya la watuhumiwa wakuu kupita? Ni kambi yako?

  Hizi rushwa ndogo unazisema hadharani tulipopiga kelele za rushwa kubwa hukuwa mmoja wao!!!

  Sitasita kusema umekichoka chama chako uko tayari kukiangamiza.
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Maelezo yake yanaonyesha kutolewa na mtu aliyekaa chini akafikiri na siyo THINK tank feki mzee Wassira a.k.a mzee wa kulala
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  January zipo habari kwamba ulikuwa mtumishi wa Ikulu nini kimetokea umekazana kuandika facebook je malalamiko hayo usingeweza kupeleka Ikulu ambako wewe ni nyumbani?

  Nani atapiga vita rushwa kwa dhati kabisa kama hata nyinyi watu wa jikoni mnashindwa kumweleza Rais?

  January nina hakika unayo simu ya JK kwani wewe ulikuwa mwandishi wa hotuba zake....mpigie simu mweleze huko facebook tuachie sisi wanyonge walalahoi.

  Nina matumaini sana na wewe kuwa daraja la bunge na Ikulu kutokana na kazi yako ya mwanzo.

  nchi hii kila mtu malalamikaji tunakwenda wapi?
   
 6. a

  akelu kungisi Senior Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama inaonyesha unamfahamu sana huyu kijana, endelea kutapika tumjue huyu kijana maana kwa maelezo yako anaonyesha kuwa ni Peter Serukamba wa pili!
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  January ninakuagiza kwa mamlaka ya mimi kuwa mwajili wako (mwananchi) Rais atakaporudi nenda mwambie na mpatie ushahidi wa rushwa unaosema na kisha rudi facebook tuambie umefikisha tuhuma hizo kwa ajili yetu wanannchi.

  Balaa blaaa za watu mlioko jikoni hatutaki tunataka matendo yenu yawe mwanga wetu wanyonge.....vitendo mbele maneno nyuma.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hakuna siri tovuti ya bunge iko wazi inaweka CV yake wazi huhitaji kuumiza kichwa
   
 9. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are getting it wrong. Kuwahi kufanya kazi ikulu kuna uhusiano gani na alichokisema January. Yeye mwenyewe amesema; vita dhidi ya rushwa ni zaidi ya uwezo wa kitaasisi, inahitaji dhamira ya mtu mmoja mmoja kuchukia.
   
 10. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 11. a

  akelu kungisi Senior Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi tunavyoendelea na mjadala huu, January Makamba anaendelea kuwachana mawaziri wa nishati na madini! Angalieni
   
 12. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hivi January si yuko bungeni?
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mbona nimeisoma hii habari sijaona sehemu ambayo kawalipua hao wala rushwa?:A S angry:
   
 14. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Still huu bado ni unafiki wa hali ya juu.., Sasa kama wewe kiongozi umeona wala rushwa unawajua na umewapeleka Takukuru ambapo hawajafanya kitu.., umefanya nini kuhusu hili tatizo kama sio kubwabwaja hapa.. (hata majina huwataji, siku hizi kuna camera's na recordings, kwanini usingeongea na takukuru ukaweka mtego..., Hizi ni kelele tu ambazo hazimsaidii mtu (hakuna mtu ambae hajui kwamba kuna rushwa.., This is not News..) kwahio hizi kelele unazopiga bila kufanya chochote ni kelele tu... (tafanya hiki, tafanya hiki..!!! My foot why don't you do it now by starting naming and shaming the culprits... :( )

  [​IMG]
   
 15. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  huyu kijana hana lolote. tunataka ajibu hija ya kununua wapiga kura na hata wagombea wa vyama vingine jimboni kwake ili kupata ubunge.

  huyu mtu amepata ubunge kwa rushwa. anapata wapi moral authority ya kukemea rushwa na ufisadi. eti"ameumbwa na kiburi cha kukataa kununuliwa'. huwezi kuwa na kiburi hicho alafu wakati huo huo ukawa na tabia inayokinzana na kiburi hicho.yani kutoa rushwa ili kupata madaraka.

  tunataka uthibishe dhamira yako pasipo shaka kabisa.

  alafu ndg zangu tutofautishe uwezo wa kujenga hoja na usafi wa mtu. usafi wa mtu hauthibitishwi na uwezo wake kwa kiushawishi au kujenga na kutetea hoja vizuri.hivi ni vitu viwili tofauti.

  isitoshe self-praise ni kielelezo cha kiburi kingine kinachokinzana na tabia ya unyenyekevu.

  kwa wale wanaopenda kujisomea pindi wanapopata nafasi someni nadhari inayoitwa Soft "power".Huyu kijana anajaribu kuitumia kutuhadaa ili tumuaminina kwa kufanya hivyo ajpAtie madaraka ambayo kwa kweli he dorsnt deserve.

  ni hayo tu kwa leo wadau
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kaza mwendo na imani tutafika lakini kwa chama ulimo ni ukoma usiweza kutibika
   
Loading...