Janga la Kufikiri Bila Kuanza!: Denis Mpagaze

Janga la Kufikiri Bila Kuanza!: Denis Mpagaze

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,232
Wanaofikiri ni wengi ila wanaoanza ni wachache! Unajua kwa nini? Kuanza ni kazi ngu sana!

Watu wana mawazo mazuri ila wameshindwa kuyabadilisha kuwa pesa, kuwa mali, kuwa mtaji, kuwa maisha!

Kwahiyo hata uwe na mawazo mazuri kiasi gani, **** huanzi watu watakuona mwehu tu! Watakusikiliza na kukuweka kwenye jopo la watu waliochanganyikiwa😄😄. Utasikia amesoma sana mpaka amekuwa kichaa!

Thamani ya wazo iko katika kulitekeleza na siyo katika kulisema. Tunasemaga amefanya vizuri na siyo amesema vizuri!

Kuanza ni kazi ngumu, ndiyo maana hata aliyesomea vizuri biashara utamkuta kwenye biashara za watu anatumwa. Kwa nini asifungue biashara yake?

Mafanikio yetu yamejifika katika kuanza. Kuna neema katika kuanza. Kuna noma katika kutoanza! Hata Mungu anasubiri tuanze ndipo atuunge mkono. Mimi naanza leo, wewe je?

Wengi maisha yanatuchapa kwa sababu hatuanzi. Tunasema vizuri, tunafikiri vizuri, tunasoma vizuri, tunashindwa kuanza. Hili ni janga kubwa!

Kila mtu ana pesa nyingi kichwani, issue ni kuziprint hizo pesa azitumie. Ndiyo! Kuna mtu akianza kuongea, pesa unaiona! Mwambieni sasa aanze, loh!

Hata mtu mwenye mawazo makubwa ukimwambia kwa nini huanzi atakwambia anasubiri mambo yake yakae sawa! Yanakaaje sawa bila wewe kuyaweka sawa?

Tunaweka mambo sawa kwa kuanza na siyo kwa kusema. Usiwe kama anayesema ati ana akili ya biashara tatizo amekosa mtaji. Akili gani sasa hizo zisizoweza kukupatia mtaji?

Sikiliza! Akili ni uwezo wa kupata unachokita na siyo uwezo wa kufikiri unachokita. Kufikiri tu kutakufanya uogope maisha ya kesho.

Kesho yako inategemea na unachofanya leo na siyo unachofikiri leo. Umahiri kufikiri bila kuanza unawalaza watu njaa kila siku!

Kesho ni ya wale wanaoanza leo, maana hata wakiondoka walichokianzisha kitaendelea kuishi! Wataacha alama. Hatuachi alama kwa kufikiri, tunaacha alama kwa kuanza kufanyia kazi yale tunayofikiri.

Kuanza maana yake ni kupumzika kufikiri na kuanza kufanya. Ukitumia muda mwingi kufikiria kitu hutofanya kitu alisema Bruce Lee! Kila unavyozidi kufikiri ndivyo unavyozidi kuwa na hofu ya maisha!

Tony Robbins aliwahi kusema watu wengi wanajua nini cha kufanya lakini ni watu wachache tu ndiyo wanafanya wanachojua.

Kumbe kujua tu haitoshi, fanya hicho unachojua tuone! Ubunifu wa kweli unaanzia pale maneno yanapoishia na matendo yanapoanzia. Ukiacha maneno, ukaanza matendo utaonekana mtu wa maana.

Kwahiyo tupunguzeni kupepeta midomo, tuanzeni kufanya. Tusiwe kama baiskeli ya kunolea visu, inapiga kelele nyingi lakini haitembei. Iko palepale! Tuache tararila!

Kuna miujiza mikubwa katika kuanza alisema Josiyah Martin. Tuanzeni sasa ili tushuhudie miujiza. Kufikiri bila kuanza kunakufanya uonekane muoga wa maisha. Maisha ni kuanza!

Tunajikuta kwenye matatizo makubwa kwa sababu ya kufikiri kupitiliza, wazungu wanaita overthinking. Overthinking ni sanaa ya kutengeneza matatizo ambayo hayakuwepo.

Kuwa makini na mtu ambaye maneno yake yanapishana na matendo yake. Anaongea hutendi.Wa nini sasa?

Mtu ana mawazo makubwa ya kujiajiri lakini hajiajiri. Kazi yake ni kulalamika ati mwajiri wake hampi likizo, haongezi mshahara, hampi safari. Kwa nini asianzishe vyake.

Ni rahisi kujenga hoja za kukosoa kuliko kuanza cha kwako. Utasikia hajui kuimba! Anayesema hajui kuimba hajawahi kuimba. Hili ni janga!

Kufikiri sana bila kuanza ni ugonjwa alisema Dostoyevsky. The transition from thought to action often requires a higher level of motivation and discipline wanasema wazungu.Sitafasiri!

Kuanza ni kazi ngumu inayohitaji ujasiri mkubwa ndiyo maana watu wanakufa na mawazo mazuri kichwani kwa sababu hawakuwa jasiri wa kuanza!

Jipatie Kitabu Kimoja kwa Sh 5,000 tu, softcopy. Mpesa 0753665484! Hardcopy piga, +255 753 690 907!

Vitabu hivi hapa!

1. Malezi: Muandae Mwanao Kuwa na Hadhi
2. Biashara Huanzia Kichwani Siyo Mfukoni
3. Fikra Tunduizi: Tungo za Kufikirisha
4. Wasomi Huru Gerezani
5. Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana
6. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika
7. Fungua Ubongo
8. Miamba ya Afrika
9. Viongozi Walioandika Majina yao Vibaya
10. Mbinu 16 Alizotumia Yesu Kutoboa
11. Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa
12. Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa!
13. Ukombozi wa Fikra

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
 
Back
Top Bottom