Janga: Bodaboda zinaua watatu kila siku nchini

Janga: Bodaboda zinaua watatu kila siku nchini

1.jpg



Ajali hii mbaya iliokea asubuhi ya Septemba 26, 2013 kwenye barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.

Kamera ilimshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.

Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.

1+(2).jpg


2.jpg


3.jpg


4.jpg


5.jpg


7.jpg


Chanzo: http://zanzibarelite.blogspot.co.uk/2013/09/ajali-mbaya-kati-ya-gari-na-bodaboda.html
 
Dar+es+Salaam-20130611-00229.jpg


Ajali ilitokea Mtaa wa chuma road karibu na bodi ya nafaka.

Wenye pikipiki walikua wanatoka Veta kunyoosha mbozi road na mwenye gari anatokea kwa sokota.

Mwenye gari akapinda kona ya Simba Plastiki na kuwazoa wenye pikipiki.

Dar+es+Salaam-20130611-00232.jpg


Dar+es+Salaam-20130611-00231.jpg


Dar+es+Salaam-20130611-00233.jpg


Dar+es+Salaam-20130611-00240.jpg




Chanzo: KARIBU TEMEKE: AJALI MBAYA KATI YA MWENDESHA BODABODA NA LORI.....DEREVA WA BODABODA AMEFARIKI DUNIA
Haya ndiyo madhara ya nchi iliyojaa harufu ya rushwa . Sasa kama leseni zinatolewa hata kwa watu wasiojua sheria za usalama barabarani unategemea nini?
 
Ingekua amri yangu ningezipiga marufuku kabisa. Zisitumike kibiashara, mtu akiwa na pikipiki iwe yake mwenyewe, unatumia at your own risk. So far kuna watu wangu wa karibu wasiopungua watano ambao wametangulia mbele ya haka kwa sababu tu ya bodaboda.
 
Ingekua amri yangu ningezipiga marufuku kabisa. Zisitumike kibiashara, mtu akiwa na pikipiki iwe yake mwenyewe, unatumia at your own risk. So far kuna watu wangu wa karibu wasiopungua watano ambao wametangulia mbele ya haka kwa sababu tu ya bodaboda.

Tatizo, ajali za bodaboda zimefumbiwa macho pamoja na kwamba zinapoteza maisha ya watu wengi na wengine kubakia na vilema vya maisha.

Mbaya zaidi bodaboda zimeanza kutumiwa kisiasa ili kupata support kutoka kwa vijana wa kima cha chini.
 
Hii ajali inadaiwa kutokea Iringa dakika 20 tuu baada ya kuanza kwa mwaka 2014.

IMG_9325.JPG


IMG_9328.JPG


IMG_9329.JPG


Hii ni ajali mbaya ya piki piki iliyotokea eneo la Ilala katika Manispaa ya Iringa ikiwa ni dakika 20 baada ya kuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014

​
IMG_9330.JPG


Hawa ni majeruhi wa ajari hiyo kushoto ni dereva wa boda boda JOseph Nyegele na kulia ni abiria wake ambae hajitambui kabisa

​
IMG_9332.JPG


IMG_9341.JPG


IMG_9344.JPG


IMG_9345.JPG


IMG_9348.JPG


Wasamaria wema wakisaidia kushusha majeruhi ambao wamepata ajali ya pikipiki usiku huu wakati wakiuanga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 mjini Iringa

Chanzo: Burudan Mwanzo - Mwisho: MWAKA MPYA 2014 WAANZA KWA AJALI MBAYA IRINGA NI DAKIKA 20 BAADA YA MWAKA MPYA
 
Seriously hili ni janga kwa taifa, juzi nimepoteza class mate kwa ajali ya pikipiki. Lazima tujadiri tuje tupate suruhisho la tatizo.
 
Tatizo, ajali za bodaboda zimefumbiwa macho pamoja na kwamba zinapoteza maisha ya watu wengi na wengine kubakia na vilema vya maisha.

Mbaya zaidi bodaboda zimeanza kutumiwa kisiasa ili kupata support kutoka kwa vijana wa kima cha chini.


Tatizo kubwa liko hapo, hakuna kiongozi wa kisiasa anayeweza kusimama jukwaani akasema zipigwe marufuku, hata kwenye mijadala mingi wanasiasa hawataki kabisa kuliongelea hili utadhani hakuna madhara yeyote wakati kila siku watu wanateketea.
 
Kwanza kabisa ziliwekwa kwa sababu ya siasa .Ndio maana hawawezi kuongea kitu chochote kuhusu badaboda .Ni bora ziuwe watu na kuwatia vilema vya maisha na wao waendelee kupeta kwenye mambo yao .Sasa hapo wanajenga au wanaendelea kujenga taifa la vilema ?
 
Back
Top Bottom