Janeth Rithe: Serikali iwasikilize Wamiliki wa mabasi

Janeth Rithe: Serikali iwasikilize Wamiliki wa mabasi

Mie nadhani Mawakala iwe biashara au entity inayojitegemea.. na Wenye mabasi wanaweza kuanzisha mawakala wao wa kuajiriwa ofisini.. ili kuondoa double standards..

Wakala ukiwa na ubia naye alikata tiketi ipewe uzito uleule sio amekatia ofisini ndio anaonekana wa maana.

Na lazima tuamue kama tunataka kutumia mfumo ..basi tutumie mfumo.. sio huku mfumo huku makaratasi.. hatuwezi kwenda.

Kwa mfumo huu sio kama wenye mabasi wanalalamika.. nina shaka.huenda wanaolalamika bioy wale wale madalali wanaonyonya abiria na wenye mabasi.

Mfumo uko safi... Ila inahitaji elimu kutolewa ya kutosha..
Shida ipo kwenye kujaza pesa kila siku, gari inatoka Arusha - Kigoma 50 x 60,000 =3,000,000 unatakiwa uiweke in advance kweli? bado kuna mafuta na service na mengineyo na hujui kama abiria watajaa ama la
 
Hawa madalali ndio wanaoharibu hii kazi, nadhani latra wanapaswa kuwadhibiti
Abiria wanasumbuliwa sana na madalali, sikujua Kama na wenye mabasi nao husumbuliwa pia
Huyu mtu anaitwa dalali 'apigwe chini'. Abiria wote wanaohitaji msaada (walemavu) huenda na ndugu zao vituoni, huyu wakala ni wa kazi gani??
 
Hiyo milioni tatu ni deposit.. serikali haichukui.. mwenye basi anaweka kwenye account yake..kama wakala. Sioni shida maana haiendi kokote..iko humo humo.. yeye akipata abiria anakula aliyopokea kwenye account inabakia pale pale..

Hii naiona kama security ya wasafiri.. ukiharibikiwa chalinze linaitwa gari hata kama sio lako abiria wanapanda wanakwenda.. sio unaanza kukimbia na makondakta.. hii ni sawa kabisa..

Na madalali uchwara wanapotea.. maana hawana hata mia lakini wanaleta makandokando kwa wasafiri.. tunataka ukipiga kelele uwe na uwekezaji umeufanya.
 
Hawa madalali ndio wanaoharibu hii kazi, nadhani latra wanapaswa kuwadhibiti
Abiria wanasumbuliwa sana na madalali, sikujua Kama na wenye mabasi nao husumbuliwa pia
Huyu mtu anaitwa dalali 'apigwe chini'. Abiria wote wanaohitaji msaada (walemavu) huenda na ndugu zao vituoni, huyu wakala ni wa kazi gani??
Mimi natoka mwenyewe nyumbani.. nakuja hadi stand ..wewe unanionesha gari unataka ulipwe!? Kwani mimi sijui kusoma!?
 
TAARIFA KWA UMMA

Serikali Iwasikilize Wamiliki wa Mabasi.

Kwa wiki sasa, sekta ya usafirishaji imeingia mushkeli baada ya Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA) kutishia na hata kusitisha huduma zao kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.

Chanzo cha mgomo huo, kinatajwa kuwa ni kutokana na mabadiliko ya mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielektroniki ambao Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) inataka wamiliki wa mabasi kutumia mfumo mpya ujulikanao kama POS.

Baadhi ya wadau wa biashara ya usafirishaji abiria nchini wanadai mfumo huo mpya unawalazimisha kuwa na kiasi cha fedha katika laini ya simu au wakala wa huduma za fedha kwa makadirio yanayolingana na nauli tarajiwa kwa idadi ya viti vya basi ili kuweza kufanyakazi.

Mfumo huo unatajwa kusababisha matatizo kadhaa yakiwamo baadhi ya wamiliki wa mabasi kupigwa faini za mara kwa mara na hata wengine kufungiwa magari yao kutokana na kutokujua vema matumizi ya mfumo huo.

Kutokana na mkanganyiko huo, sisi ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kupitia Latra kuitisha kukao na wamiliki wa mabasi ili kujadiliana kwa pamoja mfumo gani rafiki utumike kukata tiketi za abiria ili kuondoa malalamiko na misigano isiyokuwa ya lazima.

Pili ACT Wazalendo tunaitaka Latra kufanyakazi kwa kuzingatia weledi wa kitaaluma na kukumbuka kwamba mifumo inayotumia teknolojia ya kisasa inayoingia nchini ni mipya kwetu, hivyo inahitaji muda wa kutosha kwa wadau kuielewa na kuitumia kwa ufasaha.

ACT Wazalendo tunaona badala ya Serikali kulumbana na wamiliki wa mabasi na hata kutishia kuwafungia au kuwapiga faini zisizo na tija, ni wakati sasa wa kufanyia kazi malalamiko yao kwa kina sambamba na kutoa elimu kwa wadau faida ya mfumo huo mpya.

Aidha sisi ACT Wazalendo tunaona kwamba wakati Latra inaendelea kutatua changamoto za mfumo huo mpya, iwaruhusu wamiliki wa mabasi kuendelea kutumia mashine zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) maarufu EFD's licha ya kuwa nazo zinakabiliwa na changamoto za mtandao kulingana na jiografia ya nchi yetu.

Sisi ACT Wazalendo, tunaamini njia pekee ya kutatua changamoto ni kukubali kusikilizana kwa njia ya mashauriano na kusikilizana.

Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
N/Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma.

Leo Machi 12, 2021

Kweli kabisa, lengo ni kila mdau apate stahiki yake (serikali, mtoa huduma na abiria). Ila huyu mtu anaitwa dalali sijui wakala huyu adhibitiwe
Yani mtu anunue basi lake kwa jasho lake, abiria atafute nauli yake kwa jasho lake, alafu mpumbavu mmoja aje atege apo katikati kweli jamani? Serikali mko wapi??
Mimi natoka mwenyewe nyumbani.. nakuja hadi stand ..wewe unanionesha gari unataka ulipwe!? Kwani mimi sijui kusoma!
Si ndo apo sasa, kwanza hawalipi kodi yoyote kwa kifupi hawa madalali ni wahujumu uchumi
 
Ni kweli kabisa...

Unaleta mfumo, huutolei elimu yoyote unalazimsisha watu wautumie...

Wakikuambia ukweli unawaona wakaidi unawapiga faini... siyo sawa kabisa...
 
Back
Top Bottom