Jan 7 unabii katika nchi ya Tanzania 2015

Jan 7 unabii katika nchi ya Tanzania 2015

2013

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
11,361
Reaction score
6,080
Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na kwa jina lingine anaitwa Nabii Issa, yeye ambaye atakuja kulinyakua kanisa lake na pia atakuja katika wakati wa kiama. Yeye ndiye aliyenituma nikafanye kazi yake na akaniambia katika nchi uliyotokea MUNGU alikuisha iandaa ndiyo Edeni yake ya sasa ila nitaiinua mimi mwenyewe YESU (Nabii Issa) kwa utukufu wa MUNGU mbinguni. Tokea mwaka 2012 April kama nilivyoelezea katika vipindi vya redio, television, na hata katika makala ya Nabii Hebron mengi mmeyaona na yametokea, nilisema uchawi haufanyi kazi tena katika nchi ya Tanzania, na katika meneo yote na mmeona. Walioiibia nchi wakatumia na uchawi ili wasijulikane wamejulikana, nilisema mawaziri wazembe, waizi na wasio waaminifu watafukuzwa na wengine wataacha wenyewe na mmeyaona, zaidi usome makala ya Nabii Hebron 2012, 2013 kuhusu nchi ya Tanzania utayaona yametimia, nilieleza mengi ila yasome tena na na uangalie tarehe yaliyotokea, unabii wa Nabii Hebron kuhusu nchi umetimia kuanzia kiuchumi, amani na mengineyo imetimia kuhusu viongozi wa nchi kunyanyuliwa yaani Rais Jakaya Kikwete katika Umoja wa Mataifa, viwanja vya ndege, mbuga za wanyama na mengineyo mengi kama nilivyoelezea huko nyuma.

Haya yote ni MUNGU kayafanya ili kuiinua nchi yake kama Edeni ya pili ambaye hata sasa yeye yupo Tanzania na ndio sababu Tanzania haitakaa ivamiwe na nchi yeyote ile na tokea niwaeleze haijatokea nchi ya Tanzania kuvamiwa kivita na haita tokea, huo ndio ukweli japo wapo maadui wa nchi hii waliopo nje ya nchi na hata ndani ya nchi hawatafanikiwa lolote wakafanye kazi nyingine watafanikiwa ila siyo kuigusa nchi hii, hata kama ni nchi matajiri kiasi gani hawataweza na wameshashindwa tokea 2012. Hayo mengine ni yangu mimi mwenyewe kama nilivyoelezwa na MUNGU. Katika mwaka 2015 yapo mambo mengi ambayo MUNGU atayafanya yeye peke yake na lazima yatatimia kabla ya 2015 kuisha na hata sasa tayari ameanza mengine:-

A. UCHUMI
Uchumi utapanda na kuvunja historia tokea nchi ipate uhuru. Uchumi utakuwa zaidi katika viwanda, mbuga za wanyama, madini, viwanja vya ndege na Watanzania wataongezeka kununua ndege zao binafsi za usafirishaji.

Katika kilimo 2015 mvua zitanyeesha nyingi na kwa wakati na ardhi itazaa zaidi sababu ardhi imerejeshwa uthamani wake ulioibiwa na joka kuu pamoja na baadhi ya wakoloni na wawekezaji ambao waliwekezaga katika nchi hii wakiwa wana nia ya kuifilisi tu na siyo mema. Mashamba ya serikali yatafufuka na viwanda vilivyokufaga na yale niliyotabiri 2012, 2013 yataendelea kuwa juu na kukua zaidi. Haya yote ni MUNGU ndiye aliyeamua wala hakuna wa kuzuia tayari imeshakuwa na MUNGU ameniambia Hebron nitayafanya haya yote na mengineyo.

B. BUNGE
Kama nilivyokuisha sema bunge la Tanzania linabadilishwa na MUNGU kalishika yeye peke yake. Mliona bunge lilivyobadilika wakijali maswala ya nchi hii, na kufichua uovu na mengineyo. 2015 watafanya zaidi na yapo mambo mengi ambayo MUNGU atawafungulia wabunge wayajue tena kwa wepesi na yatafichuka peupe peupe, ikiwemo rushwa, mikataba mibovu, uwizi wa pesa za nchi katika manispaa na wizara mbali mbali. Wabunge watakuwa wakali sana katika kusimamia maswala ya sheria za nchi hii tofauti na 2014, MUNGU ameshayaandaa hayo na mengineyo ambayo sijaruhusiwa niyaseme.

C. UNABII KUHUSU RAIS WA TANZANIA 2015.
Kama nilivyoelezea 2012, 2013, 2014 kuhusu Rais wa Tanzania 2015, tayari MUNGU amekuisha muandaa mwaka huu na uchaguzi nawaeleza rais hatatoka kwa waganga wa kienyeji au kwa kuiba kura au kwa kuwanunua watu kwa pesa. Wengi wanaotamani cheo hicho watatoa pesa na kuwahonga watu ili wawachague wakianzia katika vyama vya siasa na katika makundi makundi, haya yote MUNGU kasha yaona. Nawaeleza, muache, mtajuta kwa jinsi mambo yatakavyogeuka. Watu walizoea wanajipangia wenyewe, mwaka 2015 MUNGU atamweka rais peke yake kupitia Watanzania ambao ni watoto wa MUNGU aliyewaumba yeye, hawatalogeka, siku ya uchaguzi atawabadilisha wapige kura kwa yule ambaye MUNGU anamtaka na nataka muelewe Watanzania siku zote kusudi la MUNGU halizuiliki kabisa na ndivyo itakavyokuwa maajabu 2015. Itakuwa hivyo hivyo pamoja na Zanzibar pia.

D. UCHAGUZI WA UBUNGE.
Wabunge wapya wataingia katika bunge na wapo ambao ikikaribia kipindi cha uchaguzi watakosa kupewa nafasi na vyama vyao. Wengi watahamia katika vyama tofauti tofauti na baadhi yao 70% watashinda ubunge, wapo mawaziri watakaopoteza ubunge kabisa na hii itafanyika pia kwa madiwani, madiwani wengi watakuwa ni wapya. Na pia mpaka sasa wapo wabunge ambao tayari nawaona wameshapita katika uchaguzi wa ubunge na ushindi ila wakati wake wa kuyasema haya sijaambiwa, haya alinijulisha MUNGU wakati nikiombea nchi kwa jinsi nilivyomuomba yeye anionyeshe ila akanionya usiyaseme hayo na mimi ninayatii maneno ya BABA yangu wa mbinguni.

NOTE:

Watakaotumia uchawi hawatashinda kiti chochote, MUNGU hapendi uchawi kabisa. Yeye atasimamia uchaguzi mwenyewe na mtaona waliotumia uchawi watakavyoaibika baadhi yao. Na pia wengine watashindwa kutokana na hali ya wananchi kutokumpigia kura pasipo yeye kushiriki uchawi katika hali ya kawaida tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, UZIZI KUIINUA KATIKA JINA LA YESU WA NAZARETI. AMEN.

source; Welcome to Prophet Hebron blog
 
Kadi Ya Kupigia Kura Bila LOWASA=0.0000000000000000..........................................................
LOWASA ndie Shujaa Pekee Mwenye Uchungu Na nchi Hii, Hivyo Anafaa Kuwa Rais Wetu Watanzania!
 
CCM ndio pekee wanaotumia mstunguri kuwafanya washinde, mwaka huu washindwe na walegee!
 
Nakuunga mkono Nabii...na iwe hivyo ktk Jina la Yesu...Hakuna uchawi ktk nyumba ya Yakobo,Haijalishi tupo vipi mwaka huu Tanzania mpya inakwenda kuzaliwa,Hakuna utawala wowote utakaopita kwa hila,wala kwa uchawi Si Raisi,Ubunge,Udiwani,M/kiti serikali za mitaa..
 
hicho kipengele cha uraisi kama unabii ni wa kweli Lowassa hausiki kabisaaaa kuwa ndiye chaguo la MUNGU
 
huo unabii inafanana na unabii flani wa miaka mingi ukitabir rais wa tanzania 2015 tena ukayokea.mara mbili kwa watumish wawili tofauti mmoja akitoka ulaya akisema Mungu atatawala mwaka huu na niseme kwelu magufuli anahusika sana kwa utabiri huo ni mtu mwaminifu sana na anasali pentekoste church hofu ya Mungu iko ndani yake.hii vita kali unayoiona ni kwa sababu shetani hapendi Utawala wa Mungu angalia Musa alivyowatoa wana israel misri vita ilikuwa kali sana ila siku zote Upande wa Mungu ni upande wa ishindi.watu hawajui tu maandalizi ya huyu wa ukawa mapesa aliyogawa kabla ya na angalia kila anakokwenda amani inakosekana huyu si mgeni mwema,mwenyeji gapaswi
 
Member 2015 amekunywa viroba, maana anatabiri against an old date - Jan 2015
 
1.Dar kuna kipindupindu cha kufa mtu. Chama kinachohusika hakioni uchafu uliokithiri. Wewe mganga wa kienyeji aka mtabiri unasemaje kuhusu hili.
2. Do not beat about the bush. Tuambie..rais ni Lowasa au Magufuli. Mtabiri gani wewe unajificha nyuma ya pazia. Toa msimamo kama sheikh fulani.
 
Member 2015 amekunywa viroba, maana anatabiri against an old date - Jan 2015

Mkuu hope una maanisha mimi 2013, ni kwamba huuu utabiri ulitolewa tangu january 2015. mkuu. nilichofanya ni kuu-paste hapa ili ujadiliwe na kucheki validity yake mpaka sasa katika kipindi hiki cha kampeni.
 
JINSI TANZANIA MPYA ITAKAVYOKUWA MUDA WOWOTE KUANZIA APRIL 2012 UNABII WA NABII HEBRON!

Nawasalimu kwa jina la mwenyezi MUNGU, MUNGU aliyeumba mbingu na ulimwengu na ndiye MUNGU aliumba watu kwa mfano wake, MUNGU asiye na dini, MUNGU wa watu wote. Napenda kuwajulisha kuwa nchi hii ya Tanzania imechaguliwa na MUNGU na ndio Edeni ya sasa, na nchi hii ameipenda yeye kwa makusudi yake kwa ajili ya kuandaa kanisa lake la mwisho ambalo linaloongozwa na mwana wa pekee YESU WA NAZARETI. Aliponiita nimtumikie, aliniambia hayo japo yapo mengi bado hajaniruhusu niyaseme, ila nitaelezea kwa ufupi katika baadhi ya maeneo tofauti.

Jambo la kwanza uchawi au viongozi watakaotumia uchawi hawatakaa katika madaraka ya kuongoza nchi hii, hii ni sababu sasa hivi ipo katika mkono wake nay eye hashirikiani na uchawi, na pia nchi hii ndiyo iliyochaguliwa ili mataifa yote waje wamjue YESU WA NAZARETI wa kweli na watu wafunguliwe fahamu zao wamjue YESU wa kweli na ni yeye MUNGU peke yake atawaleta na kuwaongoza ili waje wafunguliwe, sababu YESU WA NAZARETI amesalitiwa na watumishi 98% wote katika ulimwengu wote wauache njia ya MUNGU. Wengine ni wachawi, wengine wamejiita, wengine ni watumishi wa mishahara, wanabakia kuwadanganya watu, hao wanampenda YESU kwa kinywa bali ndani ya mioyo yao ni unafikii umejaa. Maneno hayo siyo yangu mimi Hebron, ni maneno ambaye aliniambia YESU WA NAZARETI au jina lingine anaitwa Nabii Issa, mimi mwenyewe nilikuwa siyajui hayo aliponiambia peke yake.

Na zaidi 2012 alinipeleka mbinguni akanionyesha ulimwengu wote ulivyoharibika, ila nitaelezea kwa upande wa Tanzania, aliponionyesha niliogopa sana, sikuona sura yeyote ya mtumishi wa MUNGU zaidi ya marehemu Moses Kulola peke yake. Akaniambia katika Tanzania kwa upande wa watumishi wenye majina makubwa au kujulikana, akaniambia amebakia yeye peke yake hao wengine mimi sipo nao, na baadhi yao sijawaita hata siwajui bali wanawadanganya watu nimewaita na walifikaga mbinguni. Akanionyesha sura zao ila nitataja kazi zao tu kwa leo. Waliokuwa na benki, akaniambia huyo anajiita Nabii wangu, mimi hata simjui huyo ni mchawi, anawadanganya watanzania na wanaangamia. Akaniambia nenda ukaseme kweli yangu kama nilivyo na nitakavyo kuwa nakutuma, na usiogope mtu yeyote wala chochote, mimi nitakuwa na wewe siku zote, atakaye shindana na wewe anashindana na mimi MUNGU, je? Mwanadamu ataniweza? Akasema kwa sauti ya uchungu nenda uniandalie kanisa langu, watoto wangu wanateseka, wanapotezwa, na kupitia wewe mataifa yote nitawaongoza na kuwaleta kwako uwaongoze njia ya kweli.

Akaniambia kanisa linaloitwa kwa jina langu imebakia only 2% katika ulimwengu wote, hiyo ni 98% ni shetani ndie katawala na kuyamiliki pamoja na watu. Niliwatuma watumishi wachache na hao wamenisaliti wamegeukia upande wa adui. Ila sasa nitalikomboa kanisa langu na watoto wangu. Akaniambia nchi hii ni yangu na ni mali yangu mimi MUNGU, nitaibadilisha na itakuwa ndio taifa langu teule kwa ajili ya ukombozi wa mataifa yote, akaniambia mimi MUNGU ndiye nitakayefanya hayo kwa wakati wangu na tayari imeshaanza mengine kuyafanya, nitawatumia watu hao hao na nitawaongoza na viongozi watafanya vizuri, ila wale watu wenye nia mbaya na nchi hii atawatoa katika uongozi na hawatakaa katika serikali hii, yeye YESU atafanya ajuavyo yeye kuhusu uchawi.

Nimeelezea mara nyingi katika makala, Television na redio mbali mbali hata kabla hayajatokea na sasa yameshatokea mfano nilieleza kuhusu kuinuliwa mbuga ya Serengeti, mlima Kilimanjaro, kuinuliwa viwanja vya ndege Tanzania, gesi, mawaziri kutolewa kazini, ndege kutua kwa wingi katika nhi ya Tanzania na madini kurejeshwa kwa watanzania, mikataba mibovu kufutiwa na misamaha ya kodi itafutwa yote. Hayo ni baadhi ila yapo mengi zaidi soma makala ya Nabii Hebron kuhusu Tanzania.

·Kuhusu mikataba ya madini bado tena hata hizo share za 50% katika serikali na wawekezaji wa nje, itafika wakati itafutwa na nchi kumiliki 100%.
·Mikataba mibovu itafutwa yote, hata walogeje, this is the last time, YESU anaitengeneza nchi na ni yeye ndie atakaye yafichua yote ya uozo yaliyofanywa na watu kwa ajili ya ufisadi na kuwanyonya watanzania
·Rais bora atatokea katika nchi ya Tanzania (atakuwa bora kuliko wote katika ulimwengu wote) ni MUNGU aliyeishikilia nchi atafanya hayo.
·Tanzania itakuwa ndiyo headquarter ya airport katika bara la Afrika.
·Nchi ya Tanzania jeshi lake limenyanyuliwa sana litatengeneza silaha ambao haijawahi tegenezwa ulimwengu wote. Na nchi hii haitakaa ivamiwe kivita na nchi yeyote (ni peke yake ipo mkononi wa MUNGU).
·Tanzania ndiyo taifa tajiri kuliko nchi zote ulimwenguni, hayo yatatokea muda mchache ujao.

NOTE:
Na haya yote atafanya peke yake MUNGU ajuavyo yeye aliyeumba nchi hii, hakuna uchawi utakaofanya kazi tena, iwe katika viongozi wa siasa, na viongozi wowote wa serikali. Na pesa zilizoibiwa na nyingine kuwekwa nje ya Tanzania zitarejeshwa zote, myaonapo hayo msishangae. Ni YESU WA NAZARETI anayafanya hayo wala hasaidiwi na mtu yeyote (Nabii Issa). Na itafika muda siyo mrefu iwe ni Rais, mawaziri, wabunge, madiwani watakaotumia uchawi ili wapate hivyo vyeo wataanguka (hawatapata) kama mnafikiri natania haya ng'ang'anieni hayo wale wanaopenda ushirikina majibu mtayaona (negative-).
 
Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na kwa jina lingine anaitwa Nabii Issa, yeye ambaye atakuja kulinyakua kanisa lake na pia atakuja katika wakati wa kiama. Yeye ndiye aliyenituma nikafanye kazi yake na akaniambia katika nchi uliyotokea MUNGU alikuisha iandaa ndiyo Edeni yake ya sasa ila nitaiinua mimi mwenyewe YESU (Nabii Issa) kwa utukufu wa MUNGU mbinguni. Tokea mwaka 2012 April kama nilivyoelezea katika vipindi vya redio, television, na hata katika makala ya Nabii Hebron mengi mmeyaona na yametokea, nilisema uchawi haufanyi kazi tena katika nchi ya Tanzania, na katika meneo yote na mmeona. Walioiibia nchi wakatumia na uchawi ili wasijulikane wamejulikana, nilisema mawaziri wazembe, waizi na wasio waaminifu watafukuzwa na wengine wataacha wenyewe na mmeyaona, zaidi usome makala ya Nabii Hebron 2012, 2013 kuhusu nchi ya Tanzania utayaona yametimia, nilieleza mengi ila yasome tena na na uangalie tarehe yaliyotokea, unabii wa Nabii Hebron kuhusu nchi umetimia kuanzia kiuchumi, amani na mengineyo imetimia kuhusu viongozi wa nchi kunyanyuliwa yaani Rais Jakaya Kikwete katika Umoja wa Mataifa, viwanja vya ndege, mbuga za wanyama na mengineyo mengi kama nilivyoelezea huko nyuma.

Haya yote ni MUNGU kayafanya ili kuiinua nchi yake kama Edeni ya pili ambaye hata sasa yeye yupo Tanzania na ndio sababu Tanzania haitakaa ivamiwe na nchi yeyote ile na tokea niwaeleze haijatokea nchi ya Tanzania kuvamiwa kivita na haita tokea, huo ndio ukweli japo wapo maadui wa nchi hii waliopo nje ya nchi na hata ndani ya nchi hawatafanikiwa lolote wakafanye kazi nyingine watafanikiwa ila siyo kuigusa nchi hii, hata kama ni nchi matajiri kiasi gani hawataweza na wameshashindwa tokea 2012. Hayo mengine ni yangu mimi mwenyewe kama nilivyoelezwa na MUNGU. Katika mwaka 2015 yapo mambo mengi ambayo MUNGU atayafanya yeye peke yake na lazima yatatimia kabla ya 2015 kuisha na hata sasa tayari ameanza mengine:-

A. UCHUMI
Uchumi utapanda na kuvunja historia tokea nchi ipate uhuru. Uchumi utakuwa zaidi katika viwanda, mbuga za wanyama, madini, viwanja vya ndege na Watanzania wataongezeka kununua ndege zao binafsi za usafirishaji.

Katika kilimo 2015 mvua zitanyeesha nyingi na kwa wakati na ardhi itazaa zaidi sababu ardhi imerejeshwa uthamani wake ulioibiwa na joka kuu pamoja na baadhi ya wakoloni na wawekezaji ambao waliwekezaga katika nchi hii wakiwa wana nia ya kuifilisi tu na siyo mema. Mashamba ya serikali yatafufuka na viwanda vilivyokufaga na yale niliyotabiri 2012, 2013 yataendelea kuwa juu na kukua zaidi. Haya yote ni MUNGU ndiye aliyeamua wala hakuna wa kuzuia tayari imeshakuwa na MUNGU ameniambia Hebron nitayafanya haya yote na mengineyo.

B. BUNGE
Kama nilivyokuisha sema bunge la Tanzania linabadilishwa na MUNGU kalishika yeye peke yake. Mliona bunge lilivyobadilika wakijali maswala ya nchi hii, na kufichua uovu na mengineyo. 2015 watafanya zaidi na yapo mambo mengi ambayo MUNGU atawafungulia wabunge wayajue tena kwa wepesi na yatafichuka peupe peupe, ikiwemo rushwa, mikataba mibovu, uwizi wa pesa za nchi katika manispaa na wizara mbali mbali. Wabunge watakuwa wakali sana katika kusimamia maswala ya sheria za nchi hii tofauti na 2014, MUNGU ameshayaandaa hayo na mengineyo ambayo sijaruhusiwa niyaseme.

C. UNABII KUHUSU RAIS WA TANZANIA 2015.
Kama nilivyoelezea 2012, 2013, 2014 kuhusu Rais wa Tanzania 2015, tayari MUNGU amekuisha muandaa mwaka huu na uchaguzi nawaeleza rais hatatoka kwa waganga wa kienyeji au kwa kuiba kura au kwa kuwanunua watu kwa pesa. Wengi wanaotamani cheo hicho watatoa pesa na kuwahonga watu ili wawachague wakianzia katika vyama vya siasa na katika makundi makundi, haya yote MUNGU kasha yaona. Nawaeleza, muache, mtajuta kwa jinsi mambo yatakavyogeuka. Watu walizoea wanajipangia wenyewe, mwaka 2015 MUNGU atamweka rais peke yake kupitia Watanzania ambao ni watoto wa MUNGU aliyewaumba yeye, hawatalogeka, siku ya uchaguzi atawabadilisha wapige kura kwa yule ambaye MUNGU anamtaka na nataka muelewe Watanzania siku zote kusudi la MUNGU halizuiliki kabisa na ndivyo itakavyokuwa maajabu 2015. Itakuwa hivyo hivyo pamoja na Zanzibar pia.

D. UCHAGUZI WA UBUNGE.
Wabunge wapya wataingia katika bunge na wapo ambao ikikaribia kipindi cha uchaguzi watakosa kupewa nafasi na vyama vyao. Wengi watahamia katika vyama tofauti tofauti na baadhi yao 70% watashinda ubunge, wapo mawaziri watakaopoteza ubunge kabisa na hii itafanyika pia kwa madiwani, madiwani wengi watakuwa ni wapya. Na pia mpaka sasa wapo wabunge ambao tayari nawaona wameshapita katika uchaguzi wa ubunge na ushindi ila wakati wake wa kuyasema haya sijaambiwa, haya alinijulisha MUNGU wakati nikiombea nchi kwa jinsi nilivyomuomba yeye anionyeshe ila akanionya usiyaseme hayo na mimi ninayatii maneno ya BABA yangu wa mbinguni.

NOTE:

Watakaotumia uchawi hawatashinda kiti chochote, MUNGU hapendi uchawi kabisa. Yeye atasimamia uchaguzi mwenyewe na mtaona waliotumia uchawi watakavyoaibika baadhi yao. Na pia wengine watashindwa kutokana na hali ya wananchi kutokumpigia kura pasipo yeye kushiriki uchawi katika hali ya kawaida tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, UZIZI KUIINUA KATIKA JINA LA YESU WA NAZARETI. AMEN.

source; Welcome to Prophet Hebron blog

We we ni nabii wa uongo. Lakini Mwaka huu Lowassa rais.
 
Sir God anakataaa kuamini katika unabii na uchawii na mambo mengineee..!!!.
 
Back
Top Bottom