EMMYGUY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 11,094
- 25,336
Habari zenu Wakuu!
Tupo katika siku chache zilizobaki ili tuweze kuukamilisha mwaka 2015, sina budi kumshukuru Mungu kwa uzima anaozidi kutujaalia japo tunapita katika changamoto nyingi.
Nimeamua kuyasema ya Moyoni kuhusu JamiiForums jinsi inavyotoa elimu katika nyanja mbalimbali pamoja na utoaji wake wa habari, nimejifunza vitu vingi sana kupitia mtandao huu hadi sasa.
Sina budi kusema JamiiForums ni darasa kubwa ambalo nimekuwa nikijifunza pasipo kulipia ada yoyote, naomba kwa watoa Elimu msisite kuzidi kutuelimisha na kutupa elimu juu ya mambo yanayotukabili.
Moja ya Majukwaa yanayozidi kutoa mafunzo ni pamoja na jukwaa la Tech, Gadgets and Science, JF Doctor na mengine mengi.
Shukrani kwa uongozi mzima wa JamiiForums Media pamoja na Wanachama kwa kuzidi kuleta Mada mbalimbali ambazo Zinatuelimisha, Kutuhabarisha na Kutuburudisha.
Niwatakie Sikukuu Njema za kufunga mwaka 2015 na kufungua mwaka 2016.

Last edited by a moderator: