Jamii ya wasomi ni Rais gani anahitajika Tanzania??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Najiuliza maswali juu ya mstakabali wa nchi hii na siasa zake nakoswa jibu, maana nikikumbuka tangu 1977 CCM ilizaliwa lakini kila miaka ikienda nilitegemea kitakuwa chama chakuwatoa wananchi katika lindi la umaasikini!

La kushangaza ni kwamba kimekuwa akikumbatia mafisadi nchi nzima hata rais anayekuwa madarakani hanakuwa hana sauti yakuwaweka kizuizini walewote wanaobainika na rushwa na mbaya zaidi rais wanchi anatamka wazi kwamba

"Wala rushwa tunawajua na tutawafunga"

Hivikweli rais wanchi unajua yote unakubali kuyumbishwa? Kwanini usiwatie ndani kwanza then sheria ije ichukue mkondo wake na idhihirishe kwamba rais anachukia rushwa!

Nashindwa kuelewa anahitajika rais wa aina gani anaye weza kukemea walarushwa kwa kuanzia kwa viongozi serikalini hadi nje ya serikali!

Wewe kama mtanzania, unadhani hapa Tanzania panahitajika rais wa aina gani wakuwezakuleta maendeleo ya nchi yako?
 
Je ni zipi sifa za wasomi ili nijue kama nami ni mlengwa kwenye swali hili ili niweze kujibu.
 
Unataka upewe nini zaidi ya kuletewa mkombozi wa watanzania na Rais bora kama Dr. Slaa
 
Tafadhali nauliza hivi jamii ya wasomi ni ipi hiyo, na inahitajika kuwa na kiwango gani cha elimu ili uingie ktk hii jamii??????
Ila kwa upande wangu wangu sisikii wala siambiwi lolote kwa Dr. SLAA.
2010 HATUDANGANYIKI
 
Je ni zipi sifa za wasomi ili nijue kama nami ni mlengwa kwenye swali hili ili niweze kujibu.

Msomi simply ni mtu aliyesoma (bila kujali ameelimika au la) kwahiyo kama una uthibitisho kuwa wewe umekalia madawati au viti vya shule mpaka level ya college wewe ni msomi (haimaanishi kama umeelimika).

Sasa basi, kwa mtazamo wangu, wasomi walioelimika wengi wangependa Dr. Slaa ashike usikani ila kuna makanjanja wachache wasomi ambao hawakuelimika wanamuunga mkono mkwere na ufisadi kwa ujumla.
 
Tena wanaishi kwa kunyonya mapato yetu, wako tayari kuua, kukuweka jela, kuiba au kutuachia mashimo makubwa ya migodi bila dhahabu, kujenga madarasa kwa nguvu za wananchi na kudai wao ndo wamejenga bila walimu, kuhakikisha watz wengi hawapati elimu nzuri, wanafunzi wengi vyuoni hawatulii madarasani ili wasije elimika na kuwapindua, wako tayari kurisishana madaraka ndani ya familia zao hadi hapo mtakaposema enough is enough. Wako tayari kukutumia wewe kama chambo ili wapate kuibia nchi.

I hate this kind of leadership jamani.
 
Back
Top Bottom