Jamii ya Monduli inaungua, wanahitaji utetezi sasa...!

Konakali

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
1,533
263
Ningeomba waandishi wa habari wakaifuatilie jinsi uongozi wa CCM unavyoitafuna aridhi ya Wanamonduli....! Maeneo yanayotafunwa na uongozi huo ni pamoja na Lorkisale; katika kata ya Lorkisale, Sepeko; katika kata ya Sepeko, Losimangori; katika kata ya Lepurko, na eneo linalofahamika kama Manyara Rach; katika kata ya Esilalei....! Mara nyingine hisia za kwamba "wamejitakia wenyewe kwa kumng'ang'ania mtuhumiwa mkubwa kwa Ufisadi; Lowasa", hunitokea...! Lakini mara nyingine najikuta nikiwahurumia kwa kuwa bado ni ndugu zetu, na aridhi hiyo ni yetu wote kama Watanzania.....! Kwa kifupi mchawi mkubwa ni viongozi wa kimila; maarufu kwa jina la "Malaigwanani" ambao wamekuwa wakiendeshwa na njaa na tamaa bila kutazama mbali dhidi ya jamii wanayoiongoza...! Ama kweli nawasikitikia Wanamonduli kwa hili....! Wanahitaji watetezi, nami nimeona hatua ya kwanza ni kuanika kwanza haya matukio hadharani ili kila mmoja aelewe nini kinaendelea na nini kinatakiwa kifanyike, na kivipi....!
 
Tutakapokuja kushituka tutakuta tunapanga kwenye nchi yetu kila ardhi imeuzwa..
 
kwani kuna nini kimebaki chetu Tanzania? hasa Tanganyika, hebu fanya utafiti halafu niambie...
 
Watakuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko 2015 wmchague mkombozi anayefaa,EL atakuwa akigombea ubwana mkubwa!
 
Back
Top Bottom