Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,706
- 8,657
Wasalaam.
Jamii tuzungumze tubadilishane mawazo kidogo.
Malalamiko mengi kuhusu watoto kutelekezwa, kwenye upande wa mtelekezaji, mara zote anakuwa baba watotoðŸ˜, kwa nini lakini? Napokea mengi mengi, inasikitisha, tuzungumze kidogo.
Ndugu BAADHI YA WABABA; tunzeni watoto wenu tafadhali. Unakuta wababa wengine mmejaaliwa afya njema kabisa, kazi ya heshima ofisi ya umma au binafsi tena na cheo juu, wengine na biashara za kipato kabisa, bado kweli mnashindwa kuwa kielelezo cha baba mwema, kutwa mashtaka ya huyu hatunzi watoto wake, kawatelekeza, mama nahangaika peke yangu, watoto wanalia na kujuta. Kweli?
Unasikiliza, unamwangaliaa, unamtafakari unasema Eeh Mungu, mfunulie huyu ajue majukumu yake kuhusu baraka ulizompa.
BAADHI YA WABABA; Hivi kweli tuanze kuwatuma maafisa ustawi wa jamii huko ofisini kwenu na mwisho mabossi wenu wajue halafu mje mtulaumu? Wengine mnapelekwa mahakamani na hukumu ikitoka hamtekelezi hadi mivutano.
BAADHI YA WABABA; Mjitafakari, haipendezi hata kidogo, mmebarikiwa, msituongezee kazi za kuwataka mtimize majukumu yenu kwa njia ambazo zinaweza kumfanya Mwenyezi Mungu aondoe baraka zake.
Nasema BAADHI YA WABABA maana, ni nadra sana kusikia kesi za WAMAMA kutelekeza watoto.
Pongezi ziwafikie Wababa wote wanaoshirikiana vema na wamama au wazazi wenzao wa kike kutimiza wajibu wao.
Hivi hawa baadhi ya wababa wana shida gani hadi mioyo yao inakuwa migumu hivi na kuathiri watoto wasio na hatia halafu, wanaharibu utambulisho wa mwanaume kuwa, ni mbeba maono ya taasisi ya familia? Haya maono gani sasa haya? Wanafeli wapi?
Tubadilishane mawazo maana najua humu JF wababa na wamama wote ni wema kabisa 🌹na maoni yao yatakuwa mema kabisa....