Jamhuri yakata rufaa kwa mara ya pili dhidi ya kesi inayowakabili Kitilya, Shose na Sioi

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
UPANDE wa Jamhuri umekata rufaa kwa mara ya pili katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni katika Mahakama ya Rufaa baada ya rufaa hiyo kukataliwa katika Mahakama Kuu.

Kitilya, alikuwa Kameshina Mkuu wa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Sinare, Mkuu wa Idara ya ushirikiano na Uwekazaji Katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic

Rufaa hiyo imekatwa na Buswalo Mganga, Mwendesha mashitaka wa Serikali (DPP) katika kesi hiyo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ulifanywa wiki iliyopita na Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mganga alitangaza kukata rufaa mara baada kushindwa pingamizi lao la kupinga kufutwa kwa shitaka la nane la utakatishaji fedha lililofutwa na Emilis Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa saba baada ya kufutwa kosa la nane na kwamba bado watuhumiwa hao wapo lumande.

JaLada la kesi hiyo lipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwamba kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena tarehe 18 Mei mwaka huu.
 
Matumizi mabaya ya rasilimali na pesa za uma. Wezi walioshiriki walioachwa serikalini waunganishwe, haki itendeke iwe fundisho ili ufisadi kama huu usitokee tena.
Kuendelea kucheza mahakamani bila kuwafikisha wahusika wakuu waliokuwa serikalini ni ufisadi juu ya ufisadi.
 
Ukiona hivyo ujue DPP kesha ona hayo mashtaka saba hana uwezo wa kishinda ukizingatia ni malipo ya commission ambayo serikali yenyewe ndio iliridhia kwa hiari yake ili ipate mkopo. Wana komaa na hilo la utakatishaji kwani ndipo wanaweza kuibukia ushindi, hivyo likiondolewa kesi yao ni kazi Bure na watamjibu nini bwana mkubwa?
 
Madalali wa rushwa wameshitakiwa ila watoaji na wapokeaji wako mtaani wanapeta
Mkuu hapo mimi ndio sipati picha na hii serikali ya JPM full unafiki tu hao jamaa walioshiriki hili sakata ambao wako serikalini hataki kuwagusa!!
 
Wanafanya Kazi kwa hofu kwamba Mkuu akijua hawajakata rufaa anawafuta Kazi,hapo watampelekea ripoti kwamba mzee tumepigwa chini mahakama zote hatuna jinsi tena,kama una kesi ya msingi kwa nini uumizwe na mtuhumiwa kupata dhamana?muache apate dhamana,jipange na mashahidi wako,ielezeeni mahakama,ikiwaelewa afungwe,yaani lengo lao kumkomoa mtuhumiwa na si kuthibitisha kwamba mtuhumiwa ndio mkosaji na afungwe
 
UPANDE wa Jamhuri umekata rufaa kwa mara ya pili katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni katika Mahakama ya Rufaa baada ya rufaa hiyo kukataliwa katika Mahakama Kuu.

Kitilya, alikuwa Kameshina Mkuu wa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Sinare, Mkuu wa Idara ya ushirikiano na Uwekazaji Katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic

Rufaa hiyo imekatwa na Buswalo Mganga, Mwendesha mashitaka wa Serikali (DPP) katika kesi hiyo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ulifanywa wiki iliyopita na Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mganga alitangaza kukata rufaa mara baada kushindwa pingamizi lao la kupinga kufutwa kwa shitaka la nane la utakatishaji fedha lililofutwa na Emilis Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa saba baada ya kufutwa kosa la nane na kwamba bado watuhumiwa hao wapo lumande.

JaLada la kesi hiyo lipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwamba kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena tarehe 18 Mei mwaka huu.

Inaonekana Ofisi ya DPP inapoteza muda wa kusikiliza shauri la washitakiwa, kwa wakati huu hakuna ulazima wa kuendelea kukata Rufaa wakati kuna uwezekano wa Kurekebisha Hati ya Mashitaka.

Kinacho takiwa ni kushinda Kesi ya msingi na sio kuendelea kulumbana kwenye hatua ambazo kimsingi hazitoi hatima ya kesi.

Sielewi haswa dhamira ya DPP ni nini????
 
Back
Top Bottom