Jamhuri kuleta mashahidi watano kesi ya Nondo

Jamhuri kuleta mashahidi watano kesi ya Nondo

Hakimu, umsamehe kwa kuwa hajawahi kutenda kosa kabla, na umpe onyo kali asirudie tena.
 

Inasikitisha sana, ikumbukwe huyu Nondo ana miaka 24 ila watu wazima wenye umri sawa na baba yake ndio wanamfanyia huo upuuzi ambao kila mmoja mwenye akili timamu na kutenda haki anaona kuwa Nondo anaonewa.
 
Kifupi ajiandae kulipa faini maana shtaka lke ataamliwa kwenda jera au faini ndo maana Wakiri naomba isikilizwe mfururizi ili awahi masomo ila ndo kaharibi CV Na chama alichokuwa anakiongoza


Labda ana jambo hajaliweka wazi anasubiri dakika za mwisho aliseme
 
Kujua bwana Nondo alitekwa au alijiteka tuiachie mahakama itaamua lakini ukituliza kichwa na kuangalia mfululizo wa matukio yaliyofuatia dhidi ya dogo unaona kama yanampa meseji fulani hivi. Kuna kipindi bora kujifanya mjinga siku ipite.
 
View attachment 740162View attachment 740164

Leo tarehe 10 April 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) na Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo amefika mahakama ya Wilaya ya Iringa kwaajili ya kusikiliza maelezo ya awali kuhusu kesi inayomkabili.

Akisoma mashtaka Upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Abel Mwandalamo amesema kuwa Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambalo la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijiji Dar Es Salaam na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Nondo amekana mashtaka hayo yanayo mkabili mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Iringa Hakimu John Mpitanjia.

Aidha upande wa Jamhuri unakusudia kuleta mashahidi watano ambao ni Copro Salum, Veronica Fredy(Mpenzi wa Nondo), Alphonce Mwamule, Copro Abdulkadir na mtu kutoka Mtandao wa Tigo.

Kadhalika, upande wa jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni Taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, Maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Upande wa Jamhuri umeomba kuanza usikilizwaji wa shauri hilo na watakuwa tayari kuleta mashahidi baada ya wiki moja.

Naye Hakimu John Mpita Njia amehairisha kesi hiyo na kuanza kusikilizwa tena mfululizo tarehe 18 na 19 kutokana na maombi ya upande wa utetezi wakili Chance Mloga kuiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo kwa mfululizo.

Chanzo: dmgidange
Nimeitupa line yangu ya Tigo.
 
Back
Top Bottom