Jamhuri kuleta mashahidi watano kesi ya Nondo

Jamhuri kuleta mashahidi watano kesi ya Nondo

dajari

New Member
Joined
Oct 12, 2013
Posts
3
Reaction score
1
InShot_20180410_101922345.jpg
InShot_20180410_101533026.jpg

Leo tarehe 10 April 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) na Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo amefika mahakama ya Wilaya ya Iringa kwaajili ya kusikiliza maelezo ya awali kuhusu kesi inayomkabili.

Akisoma mashtaka Upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Abel Mwandalamo amesema kuwa Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambalo la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijiji Dar Es Salaam na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Nondo amekana mashtaka hayo yanayo mkabili mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Iringa Hakimu John Mpitanjia.

Aidha upande wa Jamhuri unakusudia kuleta mashahidi watano ambao ni Copro Salum, Veronica Fredy(Mpenzi wa Nondo), Alphonce Mwamule, Copro Abdulkadir na mtu kutoka Mtandao wa Tigo.

Kadhalika, upande wa jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni Taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, Maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Upande wa Jamhuri umeomba kuanza usikilizwaji wa shauri hilo na watakuwa tayari kuleta mashahidi baada ya wiki moja.

Naye Hakimu John Mpita Njia amehairisha kesi hiyo na kuanza kusikilizwa tena mfululizo tarehe 18 na 19 kutokana na maombi ya upande wa utetezi wakili Chance Mloga kuiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo kwa mfululizo.

Chanzo: dmgidange
 
Duuu dogo anakanyaga Mafuta iringa to dar kwa mwezi Mara mbili
 
Mungu amsimamie huyu kijana
Atavuna alichopanda na Mungu atamsimamia kwa hicho. Sasa basi akiwa alidanganya itakula kwake na ikiwa hakudanganya atashinda udhalimu dhidi yake.

Lakin nionacho kwa ushahidi wa Tigo sms na simu pamoja na mpenzi wake ikiwa na kweli kwamba siku hapatikani watu wanamtafuta yeye anakula bata na mpenzi wake itakula kwake. Na kuna uwezekano mkubwa ndicho kilichotokea
 
Vipi ikiwa alilazimishwa kutuma izo message ?.. Au sim yake ilichukuliwa ikawa sio yeye alikuwa anatuma??
 
Ngoja tuone picha litaisha vipi
 
Kifupi ajiandae kulipa faini maana shtaka lke ataamliwa kwenda jera au faini ndo maana Wakiri naomba isikilizwe mfururizi ili awahi masomo ila ndo kaharibi CV Na chama alichokuwa anakiongoza
 
Vipi ikiwa alilazimishwa kutuma izo message ?.. Au sim yake ilichukuliwa ikawa sio yeye alikuwa anatuma??

Mkuu ushahidi mahakamani hautolewi kama kupiga soga kijiweni. Shahidi alishatoa vielelezo na maelezo yake wakili anavi-cross examine yaani anahoji uhalali wa taarifa. Sio rahisi sana kupindisha ikiwa mahakama ipo huru.

Pia ushahidi sio meseji tu na simu. Kuna mpenzi wake na askari waliomhoji.

Atapata haki yake. Ikiwa alijiteka au alitekwa. Cha msingi mahakama iwe huru.
 
Hii kesi inapoteza fedha za Taifa bure tu!
Sio kihivo mkuu. Suala la mtu kutekwa sio kitu kidogo ujue. Lina athari kubwa sana kwa uchumi, usalama na siasa
 
Namuonea huruma, huyo mpenzi wake awe upande wa Nondo jamani, ingekua mimi ningejifanya nimepoteza kumbukumbu au hata naanguka mapepo ila sio kumkandamiza mtu wangu wa karibu.
 
Ndo basi tena, unategemea nini kama mpenzi wake ni Shahidi. Mapenzi ni hatari sana papachu ipo Iringa hakuna namna zaidi ya kuifuta ilipo.
 
Atavuna alichopanda na Mungu atamsimamia kwa hicho. Sasa basi akiwa alidanganya itakula kwake na ikiwa hakudanganya atashinda udhalimu dhidi yake.

Lakin nionacho kwa ushahidi wa Tigo sms na simu pamoja na mpenzi wake ikiwa na kweli kwamba siku hapatikani watu wanamtafuta yeye anakula bata na mpenzi wake itakula kwake. Na kuna uwezekano mkubwa ndicho kilichotokea
think in and out of the box
 
Back
Top Bottom