Jamhuri Kihwelu Julio a.k.a The Special One

Jamhuri Kihwelu Julio a.k.a The Special One

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Ureno wana Jose Mourinho, Germany wana Jurgen Klopp but Tanzania tuna Jamhuri Kihwelu a.k.a Alberto Julio.
Julio ni kocha ambaye ambaye amajijengea jina kutokana na kauli zake za ndani au nje ya uwanja, baadhi ya hizo kauli ni;

1. "Yanga ni sawa ni mti wa maembe wa uani, nikijisikia hamu ya embe natoka nje na kwenda kuchuma!"
Hapa akijisifu kuwa tangu ameanza kufundisha mpira hajawahi fungwa na Yanga.

2. "Simon Msuva wa nini wakati nina Julius Mrope, ambaye ana kasi kama Msuva, tena kuzidi Haruna Chanongo"
Hapa alikua akiwaponda Simba kwanini wanataka kumsajili Msuva, kwanini wasimchukue Mrope.

3. "Kama ingekua kila ukisafiri nje kwa ajili ya mpira, unapewa kiti kimoja basi mimi ningekua na uwezo wa kupanga viti vyangu toka Tanga hadi Dar"
Hapa alikua katika mazoezi mjini Tanga na timu yake ya Coastal akiwahamasisha wachezaji.

4. "Kugombea Uongozi Simba ni sawa na kumtongoza mwanamke kwani akikukubali utapata sifa hata akikukataa unapata sifa vilevile"
Haya aliyatamka baada ya kuchukua fomu kugombea u makamu mwenyekiti Simba Sc.

5. "Wewe ulilia kuliko ndugu wa Kanumba na alipokuja Rais ukajitupa kabisa chini kuonesha una uchungu sana nadhani ilikua janja ya nyani maana hauna uchungu na wadau wa mpira"
Hapa akimponda Steve Nyerere kwa kushindwa kuhudhuria msiba wa Mafisango.


Hizo ni baadhi tu ya kauli za Alberto Julio, unaweza kuongeza nyingine zilizokuvutia au kukukera toka kwake.
 
"Yanga ni sawa na gari la maiti linawai kufika makaburin halafu la mwisho kuondoka" hapa alikua akimaanisha ktk mechi iliofanyika morogoro yanga walitangulia kufunga goli kupitia patrick katalay lakini simba ikasawazisha na kuongeza la 2. Magoli ya simba yalifungwa na nurdin msigwa na athuman machuppa..
 
"Yanga ni sawa na gari la maiti linawai kufika makaburin halafu la mwisho kuondoka" hapa alikua akimaanisha ktk mechi iliofanyika morogoro yanga walitangulia kufunga goli kupitia patrick katalay lakini simba ikasawazisha na kuongeza la 2. Magoli ya simba yalifungwa na nurdin msigwa na athuman machuppa..

Hahaha.. Hii Kali.
 
Yanga ni sawa na jeneza nje limepambwa kwelikweli lakini ndani kuna maiti.
Hapa anaponda kikosi chote cha Yanga.
 
huyu si alishawahi kupata kashfa ya kuliwa kiboga na wachezaji wake huyu? mnakumbuka ile scandle?
 
watu wa pwan ni shida kwa mipasho kdogo rage alikuwa anaweza kuwakabil
 
Nafuatilia football kwa ukaribu sana, kwa kawaida viongozi wa wa soka duniani wakiongea na vyombo vya habari huwa hawana majigambo au vijembe. Mara nyingi wakihojiwa kabla ya mechi huwa wanaelezea ugumu wa mechi na jinsi gani ya kukabiliana na timu pinzani, na baada ya mechi huwa wanatoa tathmini ya mchezo. Lakini kwa Tanzania ni tofauti sana, viongozi wamekuwa na maneno kama waimba taarabu wakati mpira wenyewe wa makaratasi.
Hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom