James Millya apewa siku 4 alete ushahidi juu ya uhusiano wa Jenister Mhagama na Yusuph Mhagama

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,694
239,259
Mbunge wa Simanjiro (CHADEMA), James Millya amepewa siku 4 kuwasilisha ushahidi bungeni juu ya uhusiano wa Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu , sera ,bunge , kazi ,vijana , ajira na walemavu Mh Jenister Mhagama na Yusuph Mhagama , mume wa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Sky Associates , inayomiliki mgodi wa Tanzanite One.

Ikumbukwe kwamba mei 20 mwaka huu wakati akichangia makadirio ya wizara ya nishati na madini Millya alisema Mh Mhagama ana uhusiano wa kindugu na mmoja wa viongozi wa kampuni ya SKY ASSOCIATES Asia Gonga , aliyeolewa na Yusuph Mhagama ambaye ni ndugu wa waziri .

Naibu spika Dk Tulia Ackson alitangaza uamuzi huo wakati wa kikao cha bunge jana .

Chanzo: Nipashe

My Take

Haya mambo yanahitaji sana busara ya Spika , uthibitisho wa Lema kuhusiana na Mh Pinda ni Makinda pekee anayefahamu uliko .
 
Hizi duplicate standards?? Hata mototo mdogo anaweza kuona mabazi machoni mwa wenye kutaka u-sha-hd-i
 
Sijawahi kusikia mbunge wa c.c.m akiombwa usahidi
huenda huwa hausikilizi tu , kumbukumbu zako hazipo sawa kumbuka utasikia ukibisha nitakupa mfano ... lakini pia nikukumbushe hii kanuni ya kuleta ushahidi inamtaka mbuge kufuta kauri ya uongo aliyoisema bungeni au aamuliwe na spika au mwenyekiti kuleta ushahidi wa jambo hilo, sasa kwa maneno hayo wabunge wa CCM hufuta kauri walizozisema na ndo maana hawamuliwi kuleta ushahidi.
 
Back
Top Bottom