James Mbatia: Rais Magufuli ndiye alipitisha mikataba Bungeni kwa "Ndio" za "Mia kwa Mia"

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Heshima kwenu wakuu,

Nlikuwa namsikiliza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akutoa maoni juu ya Report zilizotoka za Mchanga wa Madini.

Amesema Watanzania tuwe Watulivu na tujue Tanzania sio Kisiwa. Amepongeza nia nzuri ya Rais Magufuli.

Amesema kinachotakiwa sasa kabla ya Mambo yote, wabunge Wapewe Elimu ya Madini na Elimu ya Soko la madini ili tusirudie Makosa tuliyoyafanya.

Amesema kipindi Mikataba ya madini na Sheria zake zinapitishwa, rais Magufuli alikuwa bungeni na alipitisha sheria hizo asilimia mia kwa mia huku akishangilia. Hali hiyo imefanya wabunge kupitisha mambo mengi yasiyo faa hasa madini tangu 1998 hadi elfu 2010 na madiliko yote yalikuwa yanafanywa kwa jaziba.

Rais Magufuli alikuwa bungeni miaka 20 ambayo ndo sheria hizo zimepitishwa. Walikuwa wanajibu ndio tena kwa kushangilia. Hivyo haipendezi kama taifa turudi huko tena.

Wanasheria wetu wafanye kazi usiku na mchana kuangalia Sheria za Kimataifa zipoje na Sheria zetu zipoje

Rais ana nia njema, tujipe muda, tuwe watulivu.. Tusifanye tena kwa mihemko kama huko nyuma. Japo wanasema walifanya kwa nia njema.

Nasikia wabunge wanasema repoti hizi ni za upande mmoja, tujipe muda wa kusikiliza upande wa pili.

Tutumie nguzo tatu katika Wimbo wetu wa Taifa; Nguzo ya Hekima, Nguzo ya Umoja wa kitaifa na nguzo ya Amani ya Taifa letu kijiweka katika ramani ya dunia.
 
wanamuonea bure chenge. Yeye alikuwa anatekeleza ilani ya ccm ya kuliibia taifa...
Ccm akiwemo magufuli ni wapumbavu sana kwa sababu haya yote ni sababu yao wote kwa umoja wao dhidi ya rasilimali za watz. Alafu wanaunda mitume kwa kuwapa ulaji wa bure watu wkt walipitisha haya yote kwa mbwembwe huku wakiwatukana watz matusi ya nguoni.
Shame on them ccm + their corrupt leaders
 
Ni upuuzi kudhani na kupuuza kinachofanyika sasa eti tu alikuwa bungeni kwa anayethubutu kuchukua hatua kuondoa unyonyaji.

Kwa usemi huu manake nikuwa Nyerere hakutakiwa kungwa mkono kuleta uhuru Tanganyika kwa sababu alikuwa amzaliwa tulipokuwa tukitawaliwa na wakoloni.

Mawazo dhaifu.sana haya. Tuwapuuze.
 
Uki iwazia sana tanzania uta konda bule. Nchi haija pata doctor hii ni lamli juu ya lamli.
 
Heshima kwenu wakuu,

Nlikuwa namsikiliza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akutoa maoni juu ya Report zilizotoka za Mchanga wa Madini.

Amesema Watanzania tuwe Watulivu na tujue Tanzania sio Kisiwa. Amepongeza nia nzuri ya Rais Magufuli.

Amesema kinachotakiwa sasa kabla ya Mambo yote, wabunge Wapewe Elimu ya Madini na Elimu ya Soko la madini ili tusirudie Makosa tuliyoyafanya.

Amesema kipindi Mikataba ya madini na Sheria zake zinapitishwa, rais Magufuli alikuwa bungeni na alipitisha sheria hizo asilimia mia kwa mia huku akishangilia. Hali hiyo imefanya wabunge kupitisha mambo mengi yasiyo faa hasa madini tangu 1998 hadi elfu 2010 na madiliko yote yalikuwa yanafanywa kwa jaziba.

Rais Magufuli alikuwa bungeni miaka 20 ambayo ndo sheria hizo zimepitishwa. Walikuwa wanajibu ndio tena kwa kushangilia. Hivyo haipendezi kama taifa turudi huko tena.

Wanasheria wetu wafanye kazi usiku na mchana kuangalia Sheria za Kimataifa zipoje na Sheria zetu zipoje

Rais ana nia njema, tujipe muda, tuwe watulivu.. Tusifanye tena kwa mihemko kama huko nyuma. Japo wanasema walifanya kwa nia njema.

Nasikia wabunge wanasema repoti hizi ni za upande mmoja, tujipe muda wa kusikiliza upande wa pili.

Tutumie nguzo tatu katika Wimbo wetu wa Taifa; Nguzo ya Hekima, Nguzo ya Umoja wa kitaifa na nguzo ya Amani ya Taifa letu kijiweka katika ramani ya dunia.

Muda huwa haujawai kusema uongo
 
Namuunga mkono Mbatia kweli elimu ya kutosha itolewe kabla ya sheria kupelekwa bungeni ili makosa haya yasirudiwe,wabunge wajadili kitu wanachokifahamu siyo tena kama walivyofanya zamani kwamba wapitishe ilani ya Chama.

Rais wangu mimi nakuunga mkono kabisa ila kabla ya kumlaumu mwizi tujitathimini wenyewe je nyumba yetu imekuwaje mpka inaingiza mwizi? Pili hawa walinzi tuliowapa dhamana watulinde walikuwa wapi mpka tunaibiwa? Ingekuwa leo tu tumeanza kuibiwa ningesamehe hawa walinzi,lakini miaka 19 kweli hawajui kama kuna mwizi anatuibia?? Okey kama walijua walifanya juhudi gani kumjulisha mwenye nyumba kwamba kuna mwizi? BRELA?? TRA? Wapi Waziri wa mambo ya ndani? Wapi Wizara ya nishati na madini? Wapi wakuu wa mikoa na wilaya zenye hizo hazina? Wapi Wizara ya ulinzi na usalama?Wapi basi hata waziri wa mambo ya nje atushtue jamani mbona mnapigwa?? Na mamlaka zote zinazohusika?? Zote hizi zisigundue uozo uliopo kwenye madini?? Kama ni kweli basi sawa na msemo wako tumerogwa inabidi pepo litolewe!!

Mhhh mimi silaumu mwizi hata kidogo wenye makosa ni sisi wenyewe,mwizi huwa anaangalia wapi fursa ipo,mwizi adhabu yake huwa inajulikana wala haitajiki majadiliano ni Mahakama tu,na mahakama ikishindwa ni wananchi kujichukulia sheria mkononi,haya mambo si madogo ati!! Ndo yanafanya wenzetu huko DRC kugombana kila siku.

Rais umeyajua haya kabla ya kumpiga mwizi safisha nyumba yako kila kona kisha tuungane kumpiga mwizi wetu na wezi wengine wasije thubutu kuingia tena.
 
Heshima kwenu wakuu,

Nlikuwa namsikiliza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akutoa maoni juu ya Report zilizotoka za Mchanga wa Madini.

Amesema Watanzania tuwe Watulivu na tujue Tanzania sio Kisiwa. Amepongeza nia nzuri ya Rais Magufuli.

Amesema kinachotakiwa sasa kabla ya Mambo yote, wabunge Wapewe Elimu ya Madini na Elimu ya Soko la madini ili tusirudie Makosa tuliyoyafanya.

Amesema kipindi Mikataba ya madini na Sheria zake zinapitishwa, rais Magufuli alikuwa bungeni na alipitisha sheria hizo asilimia mia kwa mia huku akishangilia. Hali hiyo imefanya wabunge kupitisha mambo mengi yasiyo faa hasa madini tangu 1998 hadi elfu 2010 na madiliko yote yalikuwa yanafanywa kwa jaziba.

Rais Magufuli alikuwa bungeni miaka 20 ambayo ndo sheria hizo zimepitishwa. Walikuwa wanajibu ndio tena kwa kushangilia. Hivyo haipendezi kama taifa turudi huko tena.

Wanasheria wetu wafanye kazi usiku na mchana kuangalia Sheria za Kimataifa zipoje na Sheria zetu zipoje

Rais ana nia njema, tujipe muda, tuwe watulivu.. Tusifanye tena kwa mihemko kama huko nyuma. Japo wanasema walifanya kwa nia njema.

Nasikia wabunge wanasema repoti hizi ni za upande mmoja, tujipe muda wa kusikiliza upande wa pili.

Tutumie nguzo tatu katika Wimbo wetu wa Taifa; Nguzo ya Hekima, Nguzo ya Umoja wa kitaifa na nguzo ya Amani ya Taifa letu kijiweka katika ramani ya dunia.

Hii ni hatari sana kwa huyu mchawi anayeitwa ccm, tangia uhuru hadi leo nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine isipokuwa ccm.

Mikataba yote ya kuibia wananchi imesainiwa na ccm. Ufisaidi wote ambao umefanyika nchini umefanyika china ya serikali ya chama cha mapinduzi.

Watu ambao wameibia nchi hii hadi kugeuka shamba la bibi wote ni makada wa ccm. Leo tunaambiwa Acacia haikuwa imesajiliwa, inashangaza nchi yenye usalama wa taifa, vyombo mbalimbali vya dola, yenye intelejensia ya kugundua mikutano ya vyama vya upinzani kuna watu waliopanga kufanya fujo au walikusudia kufanya uovu mbaya, leo tunaambiwa kampuni iliyokuwa inasafirisha makontena hadi 270 kwa wakati mmoja haijasajiliwa ni kituko.

CCM ndio waliofanya yote haya, badala ya kutuomba radhi watanzania leo wanaibuka na mbwembwe za uongo kwamba wao wanatetea wananchi ila wapinzani ndio wanatetea wezi. this is not serious. siku zote mchawi ujibaraguza harakaharaka ili aonekane ana huruma kumbe ni yeye aliyeuwa

CCM ndio waliologa nchi wasijifanye waganga wa kutibu nchi. Ni wao waliopiga meza ndioooooooooo akiwemo naniiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hawa ndo walipitisha mikataba kwa dharura leo ndo wanasema mibovu kweli wakina yuda wako wengi sanaaa
 
Magufuli na genge lake ndio walikuwa washangiliaji wakuu wa hizi sheria za madini.

Tena walikuwa radhi kumtolea lugha kali yeyote aliyezipinga.

Leo hii MAGUFULI anajifanya ametoka sayari nyingine, hajui hata kama yeye ni mmoja wa wahusika wa uchafu huu.

Ujinga sana, upuuzi sana!
 
Back
Top Bottom