serengo
JF-Expert Member
- Jul 30, 2013
- 488
- 362
Wana JF nimekuwa nikijiuliza kila kukicha Tanzania wanaongelewa wasomi kila kukicha , nafasi zote za uongozi zimekuwa za wasomi , hebu tujiulize huu utitili wa wasomi tulio nao umeisaidia nini Tanzania? mbona nchi inaelekea kubaya tofauti na kipindi ambacho hatukuwa na wasomi wengi, tunawasomi hata kutengeneza SINDANO hawawezi kila kitu tunaagiza kutoka nje ya nchi, kazi yao kujidai wasomi na degree za kununua au elimu za kwenye MAKARATASI ndo maana wanakuwa na uelewa mdogo?leo hii kila msomi anataka awe kiongozi serikalini wanalenga kuiba tu hakuna cha maana, tungewatambua usomi wao kama wangeleta mabadiliko mfano kwenye elimu, afya , uchumi , wasomi wetu wamebaki kupiga kelele za kuongezewa posho ndo maana tunazalisha division 5, ni mda umefika tuwahoji wasomi wetu hizo PHD zao wameifanyia nini tanzania, kuna watu wanaelimu ya kawaida sana form iv hadi vi lakini wanauelewa kuliko mtu mwenye PHD, hivyo tukiendekeza maswala ua usomi nchi yetu itapoea, tua Ndo tumpe uongoziangalie uelewa wa mtu na ameifanyia nini nchi yetu.