Jambo jema: Hayati Magufuli alikabidhiwa CCM ikiwa na mpasuko mkubwa lakini ameiacha ikiwa moja na Imara zaidi


Bwashee CCM ni jukwaa la maslahi; si chama cha siasa. Kuna vikundi na mitandao inayochipuka kila fursa inapojitokeza ya kukamatia dola na kuvuna rasilimali za umma kwa kadiri wanavyojisikia. Bashiru alifafanua hilo alipothibitisha kuwa CCM inatumia dola kubaki madarakani.

Sisi watazamaji tunashuhudia tu timu za ushindi zikipishana. 2015 timu ya ushindi ilikuwa ya mwendazake. Ikapoteza hatamu ghafla bin vuu mwaka huu mwanzoni. Sasa imeingia timu mpya. Kina bashite, sabaya, msiba na machinga wanapita kati ya bonde la kivuli cha mauti. Zaburi ya 23 inawahusu.

Hapa JF tuna wapiga debe wapya. Wa zamani wamenywea. Wengine wamekuwa vinyonga; wengine wamemng’ang’ania mwendazake at their peril. Wanasemwa eti wameanza chokochoko zao; wanaleta vijimanenomaneno vyao! Aisee. Sisi nafuu tuliyopata si haba. Angalau sasa hatofokewi tena kama tunaijua V8. CCM bado moja?
 
Vipi akina mama wenzako wapo Pwani wewe uko wapi mkuu?
 

Mbona Hujawatag jamaa zako John banaa
Hembu watag kama 3 hivi
usiishie kuwaita tuu bwashee watag bana kwwnye huu uzi
 
Kwa ufupi Mama ana kazi kubwa mno kuwaunganisha wana CCM, Magufuli alifanya sehemu yake ndio maana CCM iko imara kama mnavyoiona apumzike kwa amani kwa kweli…
 
Bado mko segerea?

Nimecheka hadi Machozi kaka!
Kweli watu na shughuli zenu...
Hivi ni Kweli Mkuu wanakulipa au Ni Porojo za hapa Jukwaani?

Mi machozi ya Kicheko hapa baada ya Kusoma uzi flani kuwa kuna watu wamezuiwa kuwaona ndugu/Jamaa segerea...
Ila Kaka Unafurahisha mnoo John
labda na kuudhi pia
 
Hahahaaaa...... Bwashee haya maisha ni mafupi bora tufurahi tu hapa Jf!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…