Jambo gani baya umewahi kumfanyia mpenzi wako na utajutia milele?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
Katika maisha ya ujana tunakutana na mambo mengi sana, mengine ya kutisha na mengine ya kawaida. Binafsi katika ujana wangu nimepitia mambo mengi mazito, nimeumizwa sana katika mapenzi na nimeumiza sana wanawake.

Kati ya kitu siwezi kusahau katika maisha yangu na namuomba Mungu anisamehe na najutia sana ni mambo mawili;

Jambo la kwanza: Nilikuwa na mwanamke ambaye alinipenda na nilidumu naye miaka minne katika mahusiano huku akinisubiri kwamba ntamuoa, lakini kiukweli moyoni mwangu sikuwa na hata wazo la kumuoa zaidi ya kumnyandua tu. Hadi pale ambapo alinishtukia kwamba mimi siyo muoaji na hadi sasa huyo binti ameolewa na kwa ndoa kabisa.

Alikuwa ni mwanamke mwema sana kiukweli, namkumbuka sana katika maisha yangu. Kinachoniuma zaidi na namuomba Mungu wa mbinguni anisamehe sana ile dhambi ni kwamba huyo dada ameshatoa mimba zangu tatu. Hakuna kitu najutia kama kumlazimisha atoe mimba zangu mara tatu.

Najua wengi mtasema kwanini alikubali kutoa, sababu ni kwamba alikuwa ananiogopa sana akihisi akikataa nitamuacha na kwa kuwa alinipenda na kuniamini basi hakutaka kuniudhi, kifupi alikuwa ananisikiliza sana. Nakukumbuka sana ewe dada na Mungu akupe maisha marefu na naomba unisamehe sana.

Jambo la pili: Ni kwamba nimewahi kutoka kimapenzi na shemeji yangu (rafiki wa mpenzi wangu). Kwa kweli inaniumiza sana juu ya unafiki wangu niliokuwa naufanya. Ewe kijana jitahidi sana kuwa kijana mwema kwa jamii na kwa Mungu ili usije ukajutia sana hapo baadae kwa makosa unayoyafanya leo. Mungu atusaidie sana.

Je, wewe ni lipi linakufanya huwa unaniumia sana ulilowai kumfanyia mpenzi wako?
 
Katika maisha ya ujana tunakutana na mambo mengi sana.mengine ya kutisha na mengine ya kawaida.Binafsi katika ujana wangu nimepitia mambo mengi mazito,nimeumizwa sana katika mapenzi na nimeumiza sana wanawake.kati ya kitu siwezi kusahau katika maisha yangu na namuomba Mungu anisamehe na najutia sana ni mambo mawili.Jambo la kwanza
Hao wapenzi wako ulikuwa mzigo kwao kwakuwa hata kuandika hujui. Ni heri uliachana nao wapate watu sahihi.
 
nlikuwaga na demu alikuwa ananipenda sana,
alitamani nimuoe,alikuwa ananiamini sana pia alikuwa ananisikiliza sana
kipindi hichohicho nlikuwa na demu flani alikuwa amenizidi umri,yule demu aliniambia nikamgegede alafu kipindi hicho nlikuwa doro mfukoni ikabidi nikamdanganye yule demu wangu anayenipenda,,alinipa 20000 then nikaenda kulipia Lodge nikamgonga yule demu mwingine aliyenizidi umri,,
hiyo kitu ilinitesa sana moyoni mpaka nlipokuja kugundua yule demu wangu anayenipenda sana kumbe alikuwa na jamaa mwingine kisirisiri,,
ilibidi nimwambie ile hela uliyonipaga nilienda kugegedea demu mwingine,,
alafu sikuwahi kujibu sms yake toka hiyo siku
 
Katika maisha ya ujana tunakutana na mambo mengi sana.mengine ya kutisha na mengine ya kawaida.Binafsi katika ujana wangu nimepitia mambo mengi mazito,nimeumizwa sana katika mapenzi na nimeumiza sana wanawake.kati ya kitu siwezi kusahau katika maisha yangu na namuomba Mungu anisamehe na najutia sana ni mambo mawili.Jambo la kwanza
Matumizi ya R na L ni janga Kwa taifa.
 
Katika maisha ya ujana tunakutana na mambo mengi sana, mengine ya kutisha na mengine ya kawaida. Binafsi katika ujana wangu nimepitia mambo mengi mazito, nimeumizwa sana katika mapenzi na nimeumiza sana wanawake.

Kati ya kitu siwezi kusahau katika maisha yangu na namuomba Mungu anisamehe na najutia sana ni mambo mawili;
Hao wote umewaomba msamaha kama unavyoonesha hapa au ni mwendelezo wa unafiki kwa Muumba, kwako binafsi, kwa wahusika na kwetu?
 
Mi Kuna demu nilitokea kupendana naye ila yeye alikuwa ananipenda Sana kuliko jinsi nilivyokuwa nampenda Mimi, ila ilifikia wakati fulani nikamchoka nikawa simpendi kbsa nikaanza kumpotezea akipiga Simu sipokei Wala kujibu texts zake.Siku Moja akaunga Safari kunifata kwetu kujua Ni kwanini namfanyia ivo,aliponikuta akaniuliza kwanini namtesa kiasi hicho wakati yeye ananipenda kwa dhati Yake yote. Jamaa nikauchuna nikajifanya bubu siongei.Akachoka akarudi kwao huku analia Sana.Ikawa ndo imeisha hivyo.

Kiukweli huwa namind Sana hii kitu sijui kwanini nilimkataa yule binti bila sababu ya maana.Huwa najutia Sana hiki kitendo.Nilipewaga za chini ya kapeti kwamba kaolewa na jamaa fulani mwalimu wa shule ya upili.

Aisee Tangia hyo siku sijawahi pata mwanamke akanipenda Kama alivyokuwa ananipenda huyo demu😥
 
Aisee Tangia hyo siku sijawahi pata mwanamke akanipenda Kama alivyokuwa ananipenda huyo demu

Duh pole sana mkuu! Bahati haiji mala mbili kaa ukilijua hilo
 
Mi Kuna demu nilitokea kupendana naye ila yeye alikuwa ananipenda Sana kuliko jinsi nilivyokuwa nampenda Mimi, ila ilifikia wakati fulani nikamchoka nikawa simpendi kbsa nikaanza kumpotezea akipiga Simu sipokei Wala kujibu texts zake.Siku Moja akaunga Safari kunifata kwetu kujua Ni kwanini namfanyia ivo,aliponikuta akaniuliza kwanini namtesa kiasi hicho wakati yeye ananipenda kwa dhati Yake yote. Jamaa nikauchuna nikajifanya bubu siongei.Akachoka akarudi kwao huku analia Sana.Ikawa ndo imeisha hivyo.

Kiukweli huwa namind Sana hii kitu sijui kwanini nilimkataa yule binti bila sababu ya maana.Huwa najutia Sana hiki kitendo.Nilipewaga za chini ya kapeti kwamba kaolewa na jamaa fulani mwalimu wa shule ya upili.

Aisee Tangia hyo siku sijawahi pata mwanamke akanipenda Kama alivyokuwa ananipenda huyo demu😥
Ndo ukome kuchezea hisia za watu
 
Nilimsaliti mwanamke wangu ambae nimedumu nae kwa Miaka sita na Kuja kujua mchepuko anaruka na ungo iliniuma sana. Ukiachana na mambo ya kuniloga Mimi na mwanamke wangu. Yule dada aliniweza. Ila nimejifunza sana Hawa viumbe nawafaidi kwa macho. Sitaki stress za mapenzi 😊😊

Najutia kwanza yule mchawi alitupanga wanaume watatu. Mie niligonga mchana mwamba akagonga usiku alizima siku nzima akapelekwa hospital kijaziwa maji hapo tukakutana Kila mjinga kaleta kiepe, wakati mie nimeleta na mishikaki wana wameleta vipaja. Tena mjinga mmoja kaleta vipaja viwili wale wote😂😂😂
 
Hawa viumbe wa kuogopa sana
 
Mi Kuna demu nilitokea kupendana naye ila yeye alikuwa ananipenda Sana kuliko jinsi nilivyokuwa nampenda Mimi, ila ilifikia wakati fulani nikamchoka nikawa simpendi kbsa nikaanza kumpotezea akipiga Simu sipokei Wala kujibu texts zake.Siku Moja akaunga Safari kunifata kwetu kujua Ni kwanini namfanyia ivo,aliponikuta akaniuliza kwanini namtesa kiasi hicho wakati yeye ananipenda kwa dhati Yake yote. Jamaa nikauchuna nikajifanya bubu siongei.Akachoka akarudi kwao huku analia Sana.Ikawa ndo imeisha hivyo.

Kiukweli huwa namind Sana hii kitu sijui kwanini nilimkataa yule binti bila sababu ya maana.Huwa najutia Sana hiki kitendo.Nilipewaga za chini ya kapeti kwamba kaolewa na jamaa fulani mwalimu wa shule ya upili.

Aisee Tangia hyo siku sijawahi pata mwanamke akanipenda Kama alivyokuwa ananipenda huyo demu😥
Kunatokeaga kapepo kama hako
 
Back
Top Bottom