Jambazi akamatwa Kimboka, Buguruni

Jambazi akamatwa Kimboka, Buguruni

MWASA78

Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
54
Reaction score
17
HALI imekua ya Nderemo kwa wakazi wa Majumbasita , Karakata na Stakishari kufuatia kutiwa Mbaroni kwa Jambazi wa kizazi kipya ajulikanaye kama RAMBO.

KIJANA huyo ambaye amekua tishio kwa maisha ya binadamu na ustawi wa watu maeneo hayo alikamatwa katika purukushani zilizotokea Kimboka BaR Maeneo ya Buguruni usiku wa kuamkia leo.

10403327_991556374193508_8583760584072188434_n.jpg



10730807_991556327526846_479493439838630046_n.jpg

1966890_991556297526849_765884326830269793_n.jpg
 
duh hatimae rambo kadakwa
 
Mbona anaweza kupanda mwenyewe kipila??? Hajachapwa vizuri huyo
 
Chalii asante kwa Picha na taarifa lakini na wewe kimboka usiku unatafuta nini?
 
Br ako ni kajambazi kweli au kakibaka uchwara.Au kalikuwa kanamendea videmu videmu vinvyo jiuza pale
 
Si ndio hapo!!!kanaonekana katoto kabisa haka inawezekana bado kanakaa nyumbani Kwao kwa mshua na maza!!

Ni kweli Mkuu kumwita huyu Jambazi ni kuidhalilisha Taaluma na Hadhi ya Ujambazi, kajitu hata bunduki za kuchezea watoto hakajui kuitumia. Huyu alikuwa Kibaka Mkuu na alikuwa anakaa kwao maeneo ya Njia panda Aiport, jirani na Transit Motel, Dar na alikuwa na tabia ya kutembea na mapanga usiku wakati mwingine akiwa na vibaka wenzake wakaiwa wameyaficha sambamba na mapaja yao kwenye suruali, wakikutana na wewe wanakwambia "tupe chetu" kwa maana ya simu na pesa au kitu chochote chenye thamani, ukiwapatia bila kubisha, wanakucharanga mapanga kidogo ambayo sio sawa na kama ungebisha, ukibisha mapanga yanakuwa makali zaidi. Hata hivyo, alikuwa na tabia ya kutoshambulia watu anaowafahamu, nimekutana naye kama mara 4 bila kuombwa chao na kuishia kuambia Bro vipi mambo, lakini nikishawapita kidogo naanza natimua mbio zaidi ya Husein Bolt. Aidha, watu walikuwa wanamfahamu kwa sababu ni mtoto aliyezaliwa maeneo haya ila kutokana na malezi mabaya, akaingia kawenye tabia hiyo ukichanganaya na bangi za kijiwe cha pale Transit Motel. Kuna siku wananchi wenye hasira waliingia nyumbani kwao, Bibi yake akamkatalia kuwa hawezi kuawawa labda wamue yeye kwanza.
 
Back
Top Bottom