Jamani ushauri.

diwan

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
308
Reaction score
114
Mimi ni kijana ambae kwa sasa nina miaka 31, nimekuwa na mpenzi wangu ambae tumekuwa na uhusiano kwa takriban miaka 5. Kwa kuwa nilimtangulia chuo mwaka mmoja tulipanga mpaka apate kazi ndio tufanye taratibu za kuoana. Baada ya kumaliza masomo yake nilijitahid kuhakikisha kwamba anapata kazi katika mkoa ambao mimi nafanya kazi. Bahati nzuri alipata katika shirika moja katika wilaya nyingine ila ndani ya mkoa ule. Kutoka ninapofanyia kazi mimi mpaka kwake ni mwendo wa masaa matatu. Baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja tukiwa tunatembeleana kila wkend na kila mtu anapopata mda mimi nilipata nafasi ya kwenda kusoma Shahada ya pili. Nilipofika chuoni Dar es salama nilianza kuiona tofauti za mawasiliano,mawasiliano hafifu na msg au Majibu ya mkato. Nilijitahid sana kujikaza kama mwanaume lakini hali iliendelea kuwa tete. Alichokuja kuniambia ni kwamba mimi na yeye basi, iliniuma kwa sababu tayari nilishaanza taratibu za kwenda kujitambulisha Kwao mwezi wa 4 '2013. Suala hilo limenifanya niwaogope wasichana kiasi kwamba kila ninaemuona naona ni wale wale. Najitahid kumuomba mungu lakini mpaka sasa kama binadamu hali hii ya hodí hainiishi na kwa sasa ni dhahiri nahitaji mke.
 
Hebu kuwa mwanaume basi na uache kulilia lia...

Hivi kuna kiungo chochote mwilini kwako kilichopungua baada ya kuachwa na huyo mwanamke?
 
Kuachwa kubaya sana, halafu hayo mapenzi ya Chuo Chuo huwa ni kupunguza stress tu wala hakuna future. Naona dem ulivyomfanyia mishemishe kumpeleka mkoa wa Zitto, ukaona umeshaoa ee? Jipange kijana mbona wakuoa wapo wengi tu au ameondoka na Mgegedo wako?
 
Heri kufiwa kuliko kuachwa !!
Aliyekufa unajua huwezi muona tena lakini
kuachwa maana unaweza kumuona tena.

Piga moyo konde ndiyo maisha utapata
mzuri zaidi ya huyo halafu nae atakukumbuka akirudi usikubali.
 
Hebu kuwa mwanaume basi na uache kulilia lia...

Hivi kuna kiungo chochote mwilini kwako kilichopungua baada ya kuachwa na huyo mwanamke?

Unachosema ni kweli, wakugegeda wapo tu. Mimi nilikuwa nayasema haya yanapowakuta wezangu. Na nilicheka saana nilipoona mtu analalamika. Asikudanganye mtu kuachwa kubaya.
 
Tatizo ni kwamba Fimbo ya mbali haiuwi nyoka ndio maana
 
Unachukua shahada ya pili hata kujieleza hujui utaachaje kuchapiwa? Eti chuoni Dar es salama! Kwanza taratibu za uandishi taabu tupu... Mimi nakushauri uache masomo urudi wilayani huko huenda mtandao ndio taabu!
 
Pole, ila piga moyo konde and move ahead.
 
Unachukua shahada ya pili hata kujieleza hujui utaachaje kuchapiwa? Eti chuoni Dar es salama! Kwanza taratibu za uandishi taabu tupu... Mimi nakushauri uache masomo urudi wilayani huko huenda mtandao ndio taabu!

Hahahahaha, naamini kuwa dhumuni limeeleweka. Hayo mambo ya taratibu za uandishi ni yako.
 

Mkoa wa zitto nimekuja juzi, Wala sifanyii kazi huku Mkuu.
 
kuachwa kuachwa ni shughuli,
mwenzako ananenepa wewe unakonda kwa mawazo kwa mawazoooo.
He he nimeukumbuka huu wimbo wa charlz baba,josee mara khalid chokoraa na kalala junior afu video king ni twalib.
Aaaaa wana mmu embu mnisaidie kuniwekea video ya huu wimbo umshindikize ndugu diwan
 
Last edited by a moderator:

sasa braza utakuaje na uchumba na mtoto wa mtu kwa miaka 5?
Wakati ulikua na ajira?
Wanawake wako wengi Muombe Mwenyezi Mungu na atakupatia,Mke mwema mtu hupewa na Mungu!
 
Mkoa wa zitto nimekuja juzi, Wala sifanyii kazi huku Mkuu.

Teh teh teh yaani umeona KGM tu ukasahau na ushauri wangu mwingine. Sikiliza kijana jifunze kukataliwa kua ni sehemu ya Maisha. Kwani wakati mlipokua Chuo ktk mkoa ule wenye Mjengo wa Bunge ulimkuta Bikra?
 
Pole sana mkuu,ni wanawake wachache sana wenye kujua kuapriciate
 
kuachwa kuachwa ni shughuli,
mwenzako ananenepa wewe unakonda kwa mawazo kwa mawazoooo.
He he nimeukumbuka huu wimbo wa charlz baba,josee mara khalid chokoraa na kalala junior afu video king ni twalib.
Aaaaa wana mmu embu msisaidie kuniwekea video ya huu wimbo umshindikize ndugu diwan
 
Last edited by a moderator:
.. ..kinachokutesa si MAPENZI bali ni roho ya UTUMWA iliyotokana na kiwango duni cha kufikiri, kupanga na kuhakikisha kuna utekelezaji fanisi wa kile kilichopangwa. Umeachwa kwasababu moja tu hukuwa mtekelezaji wa yale yaliyokuwa yakitoka kinywani mwako huyo dada alitegemea akuone kama MME, MWANAUME na BABA WA WATOTO WAKE na kama kwa miaka mitano hiyo hakuona mambo hayo matatu, then ni HAKI kwake kukutupia mbali, funguka kijana na acha kulia lia hapa..ka vipi mtafute Baba V, watu 8 au Bujibuji watakupa somo zuri namna ya kuanza upya toka hapo ulipokwama penye roho ya utumwa wa mapenzi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…