Jamani TANAPA hebu nendeni na wakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani TANAPA hebu nendeni na wakati

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIBURUDISHO, Feb 24, 2012.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Wana wa familia ya JF habari za wakati huu natumai mu wazima.
  Natumai kuna mtu alikwisha wahi andika humu suala hili kama miaka miwili iliyopita ila naona hawa jamaa hawaendi na wakati na teknolojia ya mawasiliano ya sasa.
  Suala lenyewe ni kuhusu WEBSITE yao na kwa kila Hifadhi.Hifadhi hazina tovuti na kama zina tovuti hazina habari zilizo up to date najiuliza hivi watu wanao waajiri wa IT wanashughurika na nini?.Ninachowashauri hebu jaribuni kwenda na wakati kwa kuzifanya tovuti za hifadhi zenu ziendane na wakati na kuripoti matukio na habari kwa muda uaotakiwa.Unaweza ukawa unahitaji kuelewa nitafikaje katika hifadhi fulani kutalii kama mtalii wa ndani taratibu ni zipi zinifuate ili niweze fika mahali hapo ila inakuwa vigumu sana hadi usubirie maonyesho ya nanenane ndio wakupe maelekezo kwa mdomo,sasa mimi ninayeishi Mtwara nahitaji kutembelea hifadhi ya Serengeti nitajuaje jinsi ya kufika huko ni mengi sana yanayowasibu ila leo naishia hapo.
  Nawasilisha.
   
 2. Chimps

  Chimps JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 571
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 80
  Haya ni majungu. sema wewe hujui unachokitafuta.
  Kuwa muwazi umekosa nini kwenye website ili usaidiwe, sio kuongelea mambo juujuu tu.
  Taarifa zote kuhusu utalii wa TANAPA zipo kwenye website yao ya The official site of the Tanzania National Parks - Home.
  Hifadhi zote zipo, ila kama umeshindwa kufika unapopatafuta omba msaada usaidiwe, ila sio kwa kuponda.

  Watanzania tuna kawaida ya kuponda vitu vya watu wengine bila wao kuonyesha jitihada zao.

  Kwenye website kuna kurasa ya wageni ambapo unaruhusiwa kuweka maoni yako jinsi ya kuboresha mtandao huu, cha kushangaza watu wanaanza kuponda kazi za watu wengine bila kutoa maoni yao.

  Nafikiri tubadilike kisaikologia, tujenge utamaduni wa kushauri kuluko kuponda.
   
Loading...