Jamani nini chanzo cha michepuko?

djesco

Senior Member
Jun 26, 2013
166
52
Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada KAMA IFUATAVYO:

Nimeoa na nina mke na mtoto mmoja, niko na mke wangu kwa miaka 6 sasa.Ni mtu ambaye tumetoka kijiji kimoja na shule tulisoma shule moja, maisha yetu ni ya kawaida tu ila tunapendana sana na kukwaruzana kupo kibinaadam,katika suala zima la chakula cha usiku nikimshika lazima maji ayaite mma,binafsi nililkuwa namuamini sana huyu mwananamke na kama ingetokea mtu akauliza ni nani anaamini kwamba mke wake hana mchepuko!?

Mie ningekuwa wa kwanza kunyoosha mkono, ila kumbe nilkuwa najidanganya.Mwaka 2013 alijiunga na mtandao wa kijamii wa facebook na kabla ya kujiunga aliniruhusu nami nikamkubalia mwaka huu mwezi wa pili nikamnunulia simu aina ya TECNO H6 ili mradi mama mtoto nae aende na wakati, aisee kumbe kumruhusu ajiunge na facebook na kumnunulia smartphone ili ajiunge whatsapp na mengineyo.

Lilikuwa ni kosa kubwa sana mara mambo yakaanza kubadilika mdogomdogo,kupewa unyumba ikawa mpaka mieleka na kuchana chupi vinginevyo sipati kitu,mara nikimuita kumuuliza kitu hata kama yuko sentimita moja kutoka mahali nilipo basi mpaka nirudie mara 3 ndo ataitika,simu kaweka pattern hata mpelelezi wa FBI hawezi kuzitoa ila alichokuwa hajui ni kwamba ile e-mail ya playstore nilimfungulia mimi na password nilimuwekea mie so e-mail naijua na password naijua ,majibu ya ovyo na mengine mengi ya kukera.

Ila yote nikawa namwambia mama mtoto umebadilika ila anayekuzuzua nitamjua akanibishia kuwa hana mchepuko mie nikamjibu sawa ila ipo siku nitajua na hatakuwa na la kuniambia akawa anabisha.Ilikuwa ni tarehe 06/076/2015 nikiwa likizo ambapo mke wangu aliamka asubuhi akawa analalamika anajihisi homa nikamshauri aende kazini akaombe ruhusa halafu arudi nyumbani na kwenda hospitalini ili ajue shida ni nini.

Akafuata ushauri wangu na kweli saa 5 asubuhi akawa amerudi nyumbani akiwa na dawa kibao alizopewa huko hospitalini.Siku ya 07/07/2015 jioni nikachukua simu yake nikawa nimeenda nayo kiwanjani ili nikague baadhi ya sms zake za whatsapp,fcebook,na zile za kawaida.

Kwa vile aliweka pattern mie nikaingiza mara 5 simu ikaomba e-mail na password nikaingiza ikakubali nikatoa option ya pattern ikawa free nikawa nafuatilia message za whatsapp mara ikaingia message imeandikwa,"hujambo kipenzi changu?" kuangalia jina limeandikwa "wanyumbani" nikai-trace ile namba kwenye M-Pesa maana ilikuwa ni namba ya Voda ikawa imeleta jina la huyo wa nyumbani,ni mtu ambaye namfahamu kabisa,niliumia sana,nikaendelea ku-chat kwa kujifanya mie ndo mhusika jamaa akafunguka weee then nikaamua kuachana nae.

Nikapiga screen shots yale mazungumzo na zile message nikazifuta ikabaki ile ya hujambo kipenzi,nikarudi nyumbani nikamkuta mama mtoto amelala homa imemkaba kweli jioni hiyo nikamwamsha nikampa simu afu nikamuuliza kwani wanyumbani ni nani!? Maana kakutumia meseji kwenye whatsapp hebu isome akaisoma afu akaniambia ni mtu fulani hakunificha nikazidi kumchimba akasema hajui ni kwanini jamaa aliamua kumtumia hiyo meseji.

Nikajifanya mjinga nikalala ila simu sikumpa asubuhi ya siku iliyofuata nikamchukua mtoto alikuwa anaumwa mapunye nikampeleka hospitalini,nikiwa huko nikaamua kuingia kwenye account yake ya facebook aisee nilitamani kulia sema nikajikaza kiume,nikarudi nikamwambia sasa mama mtoto jana ulikataa na leo unalo la kuniambia!? Akawa hana la kusema! Homa ikapanda mara mbili.

Nikamsubiri akapona nikaanza sasa kumuuliza vizuri aniambie ni kwanini aliamua kunisaliti!? Akasema ni shetani na hata yeye hajui,nikamuuliza tena je,alikuwa tayari kugeuzwa chombo cha starehe!? Akabaki mdomo wazi la kuniambia hana,nikamuuliza tena alikuwa na malengo gani na jamaa!? Hakuwa na jibu.

NAOMBA NISIWACHOSHE:
Mwisho wa siku nikaona ngoja nishirikishe mama yangu mie tukayaongea yakaisha na kasema harudii na amekoma na ananishukuru kwa jinsi nilivomuokoa kutoka mdomoni mwa mamba,hiyo ikaisha.

Juzi nikiwa ofisi moja hivi kukutana na mkubwa mmoja wa ofisi hiyo akawa anaongea dakika moja mara kanyeyuka kwenda nje kujibu simu na katika kufuatilia maongezi alikuwa analalamika kuwa mke wake ka-cheat na mwanaume mwingine,wiki mbili nyuma kuna dogo nusra apigwe hapa kitaa kisa aatoka na mke wa jamaa mwingine,na katika kufuatilia zaidi nimegundua michepuko imekuwa fasheni.

Sasa swali ni je,KWANINI KUCHEPUKA KUMEZIDI SANA SIKU HIZI!? KWANINI UMDANGANYE MKEO/MMEO KWA KU-CHEAT NJE!? KWA MDADA JE,UMEKUBALI KUGEUZWA TAMBALA LA DEKI KWA KUKUWA NA MCHEPUKO!?

Naomba tujadili hili na nini kifanyike

Asanteni
 
Pole sana, hongera kulitatua bila ya madhara makubwa.
Pia umelichukulia kwa mtizamo tofauti mbao ni funzo pia kwa wengine maana sijaona ukimlaumu wala kumtukana wala kumuondolea mkeo utu wake kwenye post yako (ulichoposti na ulichomwambia mkeo). Hongera sana.


Hili swala ni ni Tamaa tu Mkuu na kutokujua wapi pa kusimamia. Kwa maana
Mkuu Kitu chochote kinakuaga na THAMANI kabla ya KUKIPATA na baada ya KUKIPOTEZA. So mwanadamu anatamani sana asichonacho always na inahitaji juhudi binafsi kuushinda mwili wako. vinginevyo wengi wataanguka tu.

NB: Usisahau kuweka paragraph mkuu utakapousoma tena uzi wako
.
 
Mkuu pole sana.. Najua bado una majeraha..pole sana... vipi dogo amepona mapunye? Suala la kuchepuka yaani hakuna suluhu kabisa,, unaweza kuwa umetulia kabisa.. mwenzio ndo balaa... na hii mitandao.......binadamu tu wadhaifu sana...
 
Pole sana, hongera kulitatua bila ya madhara makubwa.
Pia umelichukulia kwa mtizamo tofauti mbao ni funzo pia kwa wengine maana sijaona ukimlaumu wala kumtukana wala kumuondolea mkeo utu wake kwenye post yako (ulichoposti na ulichomwambia mkeo). Hongera sana.


Hili swala ni ni Tamaa tu Mkuu na kutokujua wapi pa kusimamia. Kwa maana
Mkuu Kitu chochote kinakuaga na THAMANI kabla ya KUKIPATA na baada ya KUKIPOTEZA. So mwanadamu anatamani sana asichonacho always na inahitaji juhudi binafsi kuushinda mwili wako. vinginevyo wengi wataanguka tu.

NB: Usisahau kuweka paragraph mkuu utakapousoma tena uzi wako
.

nimekuelewa ndugu ila nawaogopa sana hawa viumbe kwa sasa maana nilimuuliza mama mtoto unakosa nini? hana jibu, sikuridhishi anajibu naridhika sasa shida nini!? kimya.Ujue ukiwa na hasira za karibu unaweza kuua mtu
 
hakuwahi kujiunga mitandao ya kijamii awali akaijulia kwenye ndoa. ile inawazingua wengi hasa wasio wazoefu unaweza kuta mtu ana wapenz kama 5 na zaidi wa mtandaoni na ikitokea amekutana na mmojawapo lazima wazini! Chunga sana
 
Ndg yng pole sana,hao wt yapasa kuishi nao kwa akili,hekima na busara ya hali ya juu
 
Pole sana mkuu umesuluhisha kistaaraabu.......kuchepuka ni tamaa ya mwili japokuwa wapo wengine wanaosababisha mchepuko kuwepo kwa mke au mume
 
duuh poole saan lakin naimani umejifunza kitu kutokana na hayo yote yaliyo kupata
 
hakuna companion katika ndoa nyingi...mna external factor nyingi zinawasukuma kuoa au kuolewa jambo amabalo si swa......

tamaa na story...

kujaribu

ugomvi na mivutano ya hapa na pale.

kuchokana
 
1. Kila binadamu akiingizwa majaribuni mara nyingi hawez kuyashinda ( Kumnunulia smart phone ni kumweka majaribuni) kule whatsapp, facebook, badoo, etc ni kutongozwa na kutongoza kwa kwenda mbele) sasa hayo ndiyo nasema ni majaribu
2. Kwa kweli ukifanya utafiti wanaume wangapi waliyoowa wanaoaridhisha wake zao kimapenzi utashangaa idadi ilivyo ndogo. Wengi wa wanaume wanajijali peke yao tu, mboo imesimama anamrukia mkewe dk 2 amepizi anajilaza, hajui ndio kaamsha mhemko wa mwenzie na kumwacha, kesho tena hivyo hivyo, Mwanamke atavumilia atachoka, usipomridhisha mkeo atatafuta kwa kuridhishwa (anachepuka). Wengi waliyoo wanapiga wake zao bao moja tu wakati wakichepuka wanapiga hata 4-5
3. kuzoeana sana, kunamfanya mwanaume asiwe na hamu ya mabao mengi kwa mke matokeo yake anachepuka
4. Wanaume/wanawake kutojiweka kwenye hali nadhifu ya kumvutia mwenzako kimapenzi nayo inasababisha kuchepuka (kikwapa kunuka, mdomo, miguu, uchi etc) inaondoa hamasa kwa mwenzio
5. maumbile kubadilika (mwamke/mwanaume) inaweza kuwa misuli ya uke kulegea (mwaume anamlaumu mwanamke kuwa anampwerepweta na pia mwanamke anadai uume umekua kidoti ), matumbo kuwa makubwa, inafanya mwenzako asifuraie utamu, na hatimaye anachepuka
Yaaan yapo mengi sana nisiwachoshe wanaJF
 
Pole sana mkuu... Umetumia hekma sana kutatua na kumaliza jambo hilo... Mshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kukujaalia subra hio na hekma....kila la kheri In Shaa Allah.
 
Pole sana mkuu... Umetumia hekma sana kutatua na kumaliza jambo hilo... Mshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kukujaalia subra hio na hekma....kila la kheri In Shaa Allah.

ujue mkuuu mpaka sasa haamini kama yameisha yuko na wasiwasi sana maana nashindwa hata kueleza mkuuuu
 
Michepuko ni kufuata mkumbo.
Michepuko ni tamaa zisizo na maana.
Michepuko ni kushindwa kucontrol mihemuko yako.
 
Watu wamepoteza kabisa hofu ya mungu ktk hii dunia,na hata kwenda kanisani/msikitini wengi wao ni kama fashen kwani kule haushi mwezi mahubiri ya uzinzi lazima yatagusiwa,kwa kifupi shetani amekemata sana maisha ya watu wengi,
 
labda umeacha kumuona kama mpenzi wako na unamuona kama mama watoto tu…
saingine ni ile mume anakua hana mda na mkewe, hamuonyeshi yale mapenz kama ya zamani alafu unakuta kuna mtu kando anaonyesha kumjali na vtu kama hivyo ko mwanamama lazima ataingia kwenye tamaa
Usemacho ni kweli ndugu lakini sio kwangu mie ndo maana nikawa namuuliza ulikosa nini!? maana sijawahi kupiga bao kabla ya yeye kumaliza najua sehemu zake za kumfikisha na sometime inabidi sauti ya t.v ama redio iwe juu maana ni mtifuano wa kufa mtu, kiwastani mie ni mwembamba na mwili wangu unaniruhusu kunyumbulika kwa kila mkao so huwa anafika ila sijui nini hasa kilichomkumba.
 
Duuuuh!! Ndoa hizi jamani, mie hata huwa sielewi kwanini watu huchepuka and what for!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom