Jamani Ninaomba kukaribishwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Ndugu, WanaJF'

YAH: OMBI LA KUOMBA KUKARIBISHWA SIKUKUU YA LEO.

Tafadhari husika na kichwa cha habari hapo juu. WanaJF Mimi ni ndugu yenu wa karibu sana kwa kila mwanaJF. Mpaka sasa sijapata mwaliko wowote. Ni Mtanzania halisi na mshiriki mzuri hapa JF. NINAOMBA KUKARIBISHWA MAJUMBANI KWENU NA MITOKO YA LEO NA KESHO.
Nina uzoefu wa kula vizuri UBWABWA' hasa pilau pasipo kudondosha hata punje, kwa zaidi ya miaka ishirini (20) kwa sasa, nina uwezo mkubwa sana katika hili na nina HOTPOP maalum ya kubebea na kuchukua vyakula vitakavyo bakia.
Sina aleji na chakula chochote. Wengi walionikaribisha kwao wamenifurahia sana ulaji wangu. Pia nina uzoefu wa muda mrefu wa kunywa vinywaji vya kila aina, vyenye chachu na visiyo na chachu, vikali na vya kawaida, vyenye ugwadu na visiyo na ugwadu, pasipo kulewa.

Nitafurahi sana kama mtajitokeza WanaJF kwa wingi kunikaribisha siku ya leo na kesho.

Nategemea OMBI langu litakubaliwa na wanaJF wote.

Ni mimi ndugu yenu Mtiifi sana katika kila jambo.

Wenu katika ujenzi wa taifa na ushirikiano katika mahusiano hapa JF.

Asanteni.

kbm
 
Hujaeleza kama we ni mwanamke au mwanaume.Tafadhari kama we ni mdada njoo upike mwenyewe maana mi ni junior bachelor.
 
... Duh! Mkuu, Kumbe kukaribishwa mpaka utaje jinsia?
..., mbona wapishi (chefs) wa mahotelini wengi ni wanaume?
 
.., mkuu asante sana, lakini nina wasiwasi na Mkoa wako' bado ni mpya, bilashaka hata mapochopocho siyo mengi.
 
..., mkuu KUNGURUHAFUGIKI, kunikaribisha kwa siku moja au mbili, siyo tatizo sana' si ulitayarisha bajeti ya sikukuu!
 
acha uvivu, fanya kazi na wewe uwe unakaribisha wengine. usibweteke kama dada wengi wa tz wanaodhani kila kitu wanapaswa kutimiziwa na wanaume. Uvivu ni nyumba ya mwenye njaa.
 
acha uvivu, fanya kazi na wewe uwe unakaribisha wengine. usibweteke kama dada wengi wa tz wanaodhani kila kitu wanapaswa kutimiziwa na wanaume. Uvivu ni nyumba ya mwenye njaa.

.., mkuu, siwezi pingana na mawazo yako' kwa taarifa yako mimi ni mchapa kazi sana' kuliko unavyofikiri.
Leo ni siku ya kupata good time na jamaa, siyo kwamba kuomba kukaribishwa ndiyo uvivu' pia naona hisia zako potovu zinakudanganya kuwa wote wanao omba kukaribishwa ni wadada, inaonyesha kiasi gani ulivyotawaliwa na mfumo dume katika akili yako' pole sana! Jitahidi kufikira kabla ya kutenda!
Nakutakia Pasaka Njema.
 

Ulivyoanza na ulivyondelea ni sawa na wabunge wengi kuanza kwa kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja kisha ktk kuchangia anaikosoa hoja aliyoiunga mwanzo hadi mwisho. sijui ndio kufikiria zaidi ya umakini au kuna tatizo ktk kupanga mawazo kimantiki? tusaidiane ktk hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…