Ruhazwe kwanza nashukuru kwa ushauri wako na maombi yenu nyote maana mpaka leo asubuhi tumeweza kuona miujiza ya Mungu,jana mchungaji alikuja na tukafanya maombi ya pamoja kwa zaidi ya masaa manne na kunyunyizia maji ya baraka huwezi amini hazikupita hata dakika kumi akaja jirani yetu ambaye hakuwahi kuja kwetu hata mara moja,baada ya kumkaribisha alianza kuomba msamaha kuwa kama kuna kosa kafanya basi tumsamehe na tusameheane,wote tukabaki kushangaa na nikasema mbona hatukuwahio hata siku moja kuongea au hata kuwa karibu?Mchungaji akatuambia huyu ndiye mbaya wenu na ndiye aliyekuwa anawachezea,ukweli nilitaka kumpiga ila mke wangu akasema mwache na mchungaji akamwambia kuwa vitu vibaya anavyofanya kwetu havitawezekana ana akirudia atajuta.mkuu Joseph ninahakika hayo ni majaribu tu inabidi mzidishe maombi mtashinda,kama mlikua mnasali kabla ya kulala sasa anzisha mchakato wa kulala mapema then amkeni na familia yenu yote kuanzia saa saba msali hata kwa masaa mawili then wewe na mkeo salini mara kwa mara hata mara tatu kwa usiku mzima.naamini hayo ni majarbu ukifanya kwa mfululizo utamjua nani kafanya hvyo ndani ya mwezi.mwambie Mungu sifi mpaka nimeuona utukufu wako,siogopi lolote kwakua najua upo nami wakati wote,fanya muujiza kabla hakujapambazuka....nipe feedback
Nashukuru sana kwa ushauri na tutaufanyia kazi kwani tunaamini maombi pekee ndio yatakayotuvusha katika hili,naomba pia utujumuishe katika maombi yako maana kwa sasa tunahitaji msaada wa kuunganisha nguvu pamoja na wengine kama wewe ndugu.