Jamani mwenzenu DSTV imenishinda

Sijaelewa hapa tatizo ni nini ?? Hawarushi matangazo au yana scratch sana au vipi kwani. Inakuwaje kila mtu analalamika sana tatizo nini
 
At the first time mi waliniambia shilingi ya tz imeshuka vs Dola imepanda, so nashangaa Jana tena wanantumia email kwamba gharama za vifurushi zinapanda, sasa sijui hawa jamaa wanatuona Ss ndio mitaji yao?
 
Hamasisha wengine tugome kulipia. Mimi niliacha kulipia miezi mitano iliyopita. Gharama zao kwa mwezi zinamtosha kumsomesha mtoto shule ya private kama marian. Tuachane nao.
 
VP bei digitec? Anijuze mi nilipo Nina ugomvi na watu wa cable? Huduma mbovu wao no kudai mapesa
 
multi choice kuna siku watajuta kwa hiki kiburi wanachokofa sasa, technology inakua kwa kasi sana inayomwezesha mtazamaji kujipatia chanell nyingi na zenye ubora wa vipindi na picha, wao badala ya kuweka bei rafiki kwa subscribers wanafanya kama vile wanatukomoa, mimi niliahamia kwenye iptv na ninaona kila ninachotaka in hd!
 

Nieleweshe mkuu kuhusu hiyo IPTV
 
Kila kukicha wanapandisha hvi wanajua hz hella sisi tunaokota au
 
Kiburi kikubwa kinatokana na monopoly Katika Ligi ya Uingereza. Akipatikana provider mwingine akaonesha ligi ya Uingereza basi wamekwisha kabisa.
 
Dah! Kuna watu ni matajiri sana...
 
Napendekeza tuunde chama cha subscribers wa Dstv ili tutafute jinsi ya kujitetea maana this is too much.
 
Dstv nami imenishinda, leo mwisho hizo 217,000 bora nimpe mama yangu zimsaidie. Nimewasha azam only 20k
 
tatizo sio GHARAMA ZA DSTV...

tatizo ni uwezo wako wa kifedha umekuwa mdogo!!, au haukuruhusu tena kuendelea kuwepo kwenye hiyo status!!

hii ndio reflection ya kudorora kwa uchumi!!!...sio Gharama za DSTV.

unatakiwa uwe na vyanzo vilivyo stable vya kukuwezesha kuendelea kuisha maisha yanayoendana na Gharama mbalimbali zinazotokana na mahitaji husika...

kwa msaada zaidi CHAGUA CCM, CHAGUA MAGUFULI.... maisha bora kwa kila mtanzania.........ARI MPYA, KASI MPYA NA NGUVU MPYA....... HAPA KAZI TU........













 
Kwa mwaka huu Dstv wamepandisha gharama zao Mara mbili.lkn cha ajabu content ya channel zake imepungua ubora mfano African magic channels(mnet magic showcase,urbun nk) hazina movie zenye mvuto kama zamani....mtv base,fox,fx wao ni premium wakati Azam na startimes ni channel ya kawaida tu,content zilizopo kwenye Sony max unazipata mbc4 kama sijakosea.kinachowabeba Dstv epl tu na ndio maana wakaamua kuitoa ss3 kwenda ss5 ili watu mlipie kifurushi kikubwa......kinachonishangaza kwann beinsport ambayo inapatikana middle east na baadhi ya nchi za kiarabu za Africa iwe bei rahisi na inaonyesha ligi zote za ulaya,America kusini,kaskazini,japan,china nk na michezo karibu yote dunian?
 
Kwa kweli wahanga wa hiyo kitu tuko wengi maana ukiwaza 219 halafu una ujenzi,ada za watoto,bora azam tv tu,kwani hata ukiangilia DSTV zaidi ya premier league kuna kipi cha ziada?Movie huwa mara nyingi wanarudia.
 
ni kuhusu gharama kwamba ni kubwa sana.

Hapo kwenye gharama kuna mambo mawili. La kwanza unanunua kifuruahi saizi yako. Tanua mbavu mpaka pale unapopaweza. Na la pili mnaruhusiwa kutoa maoni yenu. Unawaandikia e mail watakujibu na au kukuelewesha. Maana hicho unachokilalamikia ghali ndicho wanachokiuza. Na wameona ni wao pekee wenye bidhaa hiyo. Kama vile Tanesco. Wanaamua watakavyo sababu hawana mshindani kwenye hilo.
 
ngoja tukaangwe mpaka tutakagozinduka kutoka usingizini. haya ndio madhara ya kuishobokea CCM ambao mkada wao ndiyo wamiliki wakubwa wa haya makampuni ya kinyonyaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…