Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Mimi ni mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu hasa ligi mbali mbali duniani.
Nilikuwa nalipia DSTV Premium 139,000 wakapandisha mpaka 199,000, na sasa hivi wamenitumia ujumbe kuwa kuanzia kesho yaani Octoba 1, itakuwa 219,000. Nimekata tamaa kabisa kwani hiyo bei ni kubwa sana.
Nimeiangalia hiyo bei nikaona mpangaji wangu analipa 30,000 kwa mwezi, hivyo kwa bei hiyo atalipa kodi ya miezi 6 yaani 180,000 na atabaki na chenji ya umeme 39,000.
Uchunguzi wangu umegundua kuwa wengi wameacha kulipia kifurushi cha juu na kile cha kati kwasababu hata ukitoza kwa watazamaji wengine hutapata hiyo hela ya kulipia.
Wenyewe wanajitahidi kupiga simu kukumbushia malipo lakini ukweli wengi wetu tutakwama, labda wafikirie upya bei zao. Sasa hapa Azam ndio wangechangamka mapema ili tuachane na hawa Multichoice.