Jamani Mnakumbuka Hii Kitu, Dah.

Teknolojia ilikuwa bado changa sana,nowadays you simply text by your phone,AND sometimes you can only use Emoji na kila kitu kinakwenda sawa..
 
duuh wakati ukuta kweli enzi hizo ndio njia kuu ya kuwasiliana
 
Na Stampu yenye picha ya malkia wa uingereza[emoji3]

Ilikuwa ni lazma uende posta aisee ukitaka barua au simu acha tu.

Halaf kuna ile telegram unalipa kutokana na maneno utakayoandika wingi wa maneno ndio wingi wa hela utakayolipa aisee.

Hiyo ndio ilikuwa inaenda kwa haraka kuliko barua au ukitaka upige simu ila je uko unapotaka uwasiliane nao simu ipo...?

Hatari Sana Aisee.
 
Nakumbuka hii teknologia ilidumu mpaka mid 90. Sababu mzee wangu alikuwa akiniandikia barua akiwa london Reading University. Nilikuwa nachukulia barua pale haspitali ya kcmc. Private bag. S.L.P kila jumapili nikienda ibadani lazima nipitie pale kuangalia kama kuna barua toka mbele.

Kitambo sana.
 

Ilikuwa ukionekana na funguo ya sanduku la posta unaonekana ni mtu muhimu sana kwa kweli tumetoka mbali sana kiongozi. Hahah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…