Jamani mmeyasikia haya!!!!!?

duda

Senior Member
Mar 23, 2011
113
25
Asubuhi nikiwa naelekea kazini, nikaona magazeti mengi tu moja wapo likanivutia na gazeti hilo ni RISASI nikaona KIAMA nikataka kujua kulikoni??????????

Niliyoyakuta huko ndani wana JF huwezi amini macho yako. Kuna muumini mmoja wa dhehebu la EAGT ameoteshwa na Mungu kuwa tarehe 21 May ni siku ya KIAMA, hivyo watu tujiandae, pia ameeleza kuwa ndio maana babu wa Loliondo katumwa ili kuwaponya watu. nae baada ya kuoteshwa akaamua kumsimamisha binti yake shule ili ajiandae vema kwenda katika ufalme wa Mungu.

hakuishia hapo amesema kama hii haitatokea basi apigwe mawe mpaka afe kama manabii wengine wa uongo walivyofanywa.

jamani twaenda wapi???????? Tafakari!!!!
 
inawezekana sio mzima. akimbizwa hospitali ya wagonjwa wa akili haraka mno kabla hajaeneza hiyo sumu yake.
 
MMMh kila mtu sasa anaoteshwa na mungu Duh, nakumbuka mwaka 1984 uvumi wa mwisho wa dunia ulienea saaana na watu walitishika mnoooo naona mambo yale yanajirudia sasa
 
inatisha sana na kusikitisha, yn aliposema apigwe mawe mpaka afe, nilisikia kusisimka mwili. jamani lbda kweli??????? mh!!
 
Nyinyi hayo mwayaona mapya? Mbona hawa jamaa wanaitangaza hiyo siku tangu kitambo? Kamaunatoka ubungo bus terminal upande wakulia karibia na geti kuna bango kubwa lipo zaidi ya mwaka sasa lina tangaza hiyo siku. Wanakanisa lao ambalo limefanya huo mjadala kuonekana mkubwa huko kenya, niliona kwenye kipindi kimoja cha KBC.
 
Asubuhi nikiwa naelekea kazini, nikaona magazeti mengi tu moja wapo likanivutia na gazeti hilo ni RISASI nikaona KIAMA nikataka kujua kulikoni??????????
niliyoyakuta huko ndani wana JF huwezi amini macho yako. Kuna muumini mmoja wa dhehebu la EAGT ameoteshwa na Mungu kuwa tarehe 21 May ni siku ya KIAMA, hivyo watu tujiandae, pia ameeleza kuwa ndio maana babu wa Loliondo katumwa ili kuwaponya watu. nae baada ya kuoteshwa akaamua kumsimamisha binti yake shule ili ajiandae vema kwenda katika ufalme wa Mungu.

hakuishia hapo amesema kama hii haitatokea basi apigwe mawe mpaka afe kama manabii wengine wa uongo walivyofanywa.

jamani twaenda wapi???????? Tafakari!!!!
Bahati mbaya haya magazeti ya udaku huwa siyasomi
 
Halafu wana jamii hivi tunajiuliza kweli " kwa nini haya madai ya kuoteshwa na mungu, ama kuwa mwisho wa dunia unakaribia au mti fulani dawa ya magonjwa sugu" yanatokea upande mmoja tu wa Imani? (kama si KKKT, basi EAGT, au RC) lakini si Muslims??(Shia, Ahmadiya, Sunni, Ibaadhi)??? Hebu tutafakari jamani???
 
Ina maana wewe unajifanya ni kipofu au ni kiziwi kwamba humwonagi sheikh Yahya akitabilia watu vifo, na ndio anaempa majini Rais wetu ili yamlinde? unajifanya ulijuwi hili? na hawa wanaosema wanatibu kisunna ni kina nani? usipende kuongea kama kasuku, kabla ya kupost kitu ni vyema ukaushirikisha ubongo wako kwanza.
 
Ningepata nafasi ningemuuliza hivi, kabla ya hiyo May, Jesus atashuka lini? Kwani kabla ya kiama Jesus si atakuja duniani?
Sijui uso wake atauficha wapi baada ya hiyo tarehe yake kupita.
 
Halafu wana jamii hivi tunajiuliza kweli " kwa nini haya madai ya kuoteshwa na mungu, ama kuwa mwisho wa dunia unakaribia au mti fulani dawa ya magonjwa sugu" yanatokea upande mmoja tu wa Imani? (kama si KKKT, basi EAGT, au RC) lakini si Muslims??(Shia, Ahmadiya, Sunni, Ibaadhi)??? Hebu tutafakari jamani???

Ina maana wewe unajifanya ni kipofu au ni kiziwi kwamba humwonagi sheikh Yahya akitabilia watu vifo, na ndio anaempa majini Rais wetu ili yamlinde? unajifanya ulijuwi hili? na hawa wanaosema wanatibu kisunna ni kina nani? usipende kuongea kama kasuku, kabla ya kupost kitu ni vyema ukaushirikisha ubongo wako kwanza.
 
Apimwe akili kwa hospital halafu akanywe kikombe kwa babu
 
Asubuhi nikiwa naelekea kazini, nikaona magazeti mengi tu moja wapo likanivutia na gazeti hilo ni RISASI nikaona KIAMA nikataka kujua kulikoni??????????
niliyoyakuta huko ndani wana JF huwezi amini macho yako. Kuna muumini mmoja wa dhehebu la EAGT ameoteshwa na Mungu kuwa tarehe 21 May ni siku ya KIAMA, hivyo watu tujiandae, pia ameeleza kuwa ndio maana babu wa Loliondo katumwa ili kuwaponya watu. nae baada ya kuoteshwa akaamua kumsimamisha binti yake shule ili ajiandae vema kwenda katika ufalme wa Mungu.

hakuishia hapo amesema kama hii haitatokea basi apigwe mawe mpaka afe kama manabii wengine wa uongo walivyofanywa.

jamani twaenda wapi???????? Tafakari!!!!

sishangai sana,coz kuna wale wasabato masalia walitabiri hvyo!ila nafarijika sana kuona watanzania wenzangu wakimpangia yesu siku ya kurudi!
 
dah! Ukstaajab ya musa, utaona ya firauni! Hawa wana2ona akil ze2 ni km za kwao??. Hv huyo mungu kw nn acjtokeze kw kla m2? Ina mana wngne ha2sal au??
 
yaleyale ya kibwetere aliwachoma waumini wake akidai ni mwisho wa dunia, wafe waende mbinguni wapii hadi leo? hivi inakuaje binadamu mwenzako anakushika akili kiasi hicho?kiama kipo lakini kwa siku anyoijua mwenyewe Mungu si binadam,km huyo babu anayetangaza kiama ni 21 May,nadhani nati nyingi tu za ubongo wake zitakua zimekatika...
 
Asubuhi nikiwa naelekea kazini, nikaona magazeti mengi tu moja wapo likanivutia na gazeti hilo ni RISASI nikaona KIAMA nikataka kujua kulikoni??????????
niliyoyakuta huko ndani wana JF huwezi amini macho yako. Kuna muumini mmoja wa dhehebu la EAGT ameoteshwa na Mungu kuwa tarehe 21 May ni siku ya KIAMA, hivyo watu tujiandae, pia ameeleza kuwa ndio maana babu wa Loliondo katumwa ili kuwaponya watu. nae baada ya kuoteshwa akaamua kumsimamisha binti yake shule ili ajiandae vema kwenda katika ufalme wa Mungu.

hakuishia hapo amesema kama hii haitatokea basi apigwe mawe mpaka afe kama manabii wengine wa uongo walivyofanywa.

jamani twaenda wapi???????? Tafakari!!!!

Huyu mtu ana tofauti gani na wale jamaa waliopiga kambi pale JKNA wakisubir safari ya ulaya bila ya visa?
 
Haya mambo hayajaanza leo, aliyafanya Kibwetele wa Uganda akaua watu, maisha ni magumu sana, so hayo ni ya kawaida sana:angry::angry::angry:
 
Asubuhi nikiwa naelekea kazini, nikaona magazeti mengi tu moja wapo likanivutia na gazeti hilo ni RISASI nikaona KIAMA nikataka kujua kulikoni??????????
niliyoyakuta huko ndani wana JF huwezi amini macho yako. Kuna muumini mmoja wa dhehebu la EAGT ameoteshwa na Mungu kuwa tarehe 21 May ni siku ya KIAMA, hivyo watu tujiandae, pia ameeleza kuwa ndio maana babu wa Loliondo katumwa ili kuwaponya watu. nae baada ya kuoteshwa akaamua kumsimamisha binti yake shule ili ajiandae vema kwenda katika ufalme wa Mungu.

hakuishia hapo amesema kama hii haitatokea basi apigwe mawe mpaka afe kama manabii wengine wa uongo walivyofanywa.

jamani twaenda wapi???????? Tafakari!!!!

Kama unaamini kuwa kikombe cha babu kinaponya kwa nini ushangae mtu kuoteshwa kuwa kiama kinakuja??? Waumini wa babu mwaminini pia huyo
 
Back
Top Bottom