Jamani matokeo haya yataua watu!

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,933
1,294
Jana vyumba vingi vinavyotoa huduma ya internet vilijaa vioja na vituko ambavyo mwisho wake ulikuwa huzuni na vilio! Niliona ma sista du wakiongozana kwa mbwembwe,kuja kuona matokeo yao. Wengi walivaa vi suruali vimewabana makalio wakiingia kwa mbwembwe huku wakiwatolea maneno ya ukali watoa huduma ya internet wakidai wanataka matokeo yao haraka.. Cha kuchekesha na wakati wa kuondoka! Palikuwa hapatoshi! Wengine suruali ziliwapwaya wengine walizirai na kubebwa na wasindikizaji wao! Maringo yote kwiishaaa. Chejea matokeo weye! Usipime! Ilikuwa kama majibu ya ukimwi! Wengine wakitabasamu na wengiwao vilio!
 
full michosho letea chezo mama ndarichako wewe..
Ushauri kwa waliofeli kuna vile vyuo vinavyotangazwa wakati wa michezo na tamthlia ITV wajiunge navyo..
 
Ndo hivyo ukipanda mahindi unavuna mahindi usitegemee kuvuma maharage

wengine waliandika nyimbo za bongo fleva ktk majibu yao! Sasa hiyo ni akili au matope! Bora uache wazi kuliko kuandika ma bongo fleva!
 
hao waliochora chora vikatuni na kuandika mashairi pamoja na upuuzi mwengine kwenye karatasi za kujibia inapaswa watajwe majina yao au wazazi wao wajulishwe na hatua nyengine za kinidhamu zichukuliwe, ili iwe fundisho kwa watakofanya mithani mwaka huu. pumbavu zao hawa. mbona miaka yetu hapakuwa na utoto wa namna hii? wameniudhi sana hawa watoto. enzi zetu tulikuwa tukiskiliza miziki ya kihuni kweli kweli pamoja na kuangalia video zao ( american hip hop) lakini kwenye swala la shule tulikuwa makini, hawa bongo fleva ndo imewaharibu kiasi hiki? shenzi kabisa, ndalichako tutajie hawa watu mama
 
Ushauri kwa waliofeli kuna vile vyuo vinavyotangazwa wakati wa michezo na tamthlia ITV wajiunge navyo..

Sina hakika kama hivyo vyuo pia vitawapokea maana miongoni mwa sifa za kujiunga ni 'angalau wenye ufaulu wa daraja la nne pointi 26'.
 
hao waliochora chora vikatuni na kuandika mashairi pamoja na upuuzi mwengine kwenye karatasi za kujibia
Hawa wa Vikatuni sio mbaya wakiungana na Masudi Kipanya ili kuendeleza fani yao. Kwa upande wa mashairi si mbaya wakisaidiwa kumuona Master J, awape ushauri elekezi wawekwe kundi gani kati ya hip hop,taarabu,zouk n.k.
 
hao waliochora chora vikatuni na kuandika mashairi pamoja na upuuzi mwengine kwenye karatasi za kujibia inapaswa watajwe majina yao au wazazi wao wajulishwe na hatua nyengine za kinidhamu zichukuliwe, ili iwe fundisho kwa watakofanya mithani mwaka huu. pumbavu zao hawa. mbona miaka yetu hapakuwa na utoto wa namna hii? wameniudhi sana hawa watoto. enzi zetu tulikuwa tukiskiliza miziki ya kihuni kweli kweli pamoja na kuangalia video zao ( american hip hop) lakini kwenye swala la shule tulikuwa makini, hawa bongo fleva ndo imewaharibu kiasi hiki? shenzi kabisa, ndalichako tutajie hawa watu mama

kweli kabisa, enzi za akina Tupak na boby brown! Ujiko ilikuwa lazima kichwa chako kiwe kinachaji, na umwage ngeli ya nguvu ndo upate mpenzi! Haya ya siku hizi majinga sijaona! Kutwa yanaangalia video za kibwege, mara daimondi,mara tunda mara suma mara dushelele mbaya kabisa hata movie ni za akina kanumba! Bora waangalie za nje wajifunze hata lugha! Imekula kwao!
 
Back
Top Bottom