Jamani kuweni wazazi wenye mapenzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani kuweni wazazi wenye mapenzi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jan 14, 2010.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Miezi kama miwili hivi iliyopita mzee mmoja jirani kajulikana kua amekua akimchezea(mchezo mchafu) mtoto wake wakumzaa. :(:mad:

  Amekua akimfanyia hivyo since she was 7 and the worst part ni kwamba kamtia mimba mwanae wa miaka 12.Imagine mtoto kumzalia baba yake mtoto!!!!!!

  Hiki kitu kimenifanya nikafikiria sana kuhusu mahusiano kati ya wazazi na watoto wao.(Kama huyu naona kaamua kumpenda mwanae all the way)hehheh jokes aside......!Jiulize huyu mzee kamfundisha nini mwanae,unaweza kupata picha huyu mtoto anaweza kuwa mwanamke wa aina gani hapo baadae??Sidhani kama atastahili lawama iwapo atawachukia wanaume maisha yake yote!!Na sio kama namaanisha kua wanaume wote wanastahili adhabu yakuchukiwa na huyu binti kwa kosa alilofanya baba yake no,ila anayo haki yakuwaona wote ni wanyama coz ndo picha atakayoishi nayo for the rest of her days.

  Wewe kama mzazi ndiye unayemtengenezea mwanao picha ya jinsi ambavyo ungependa awe mwaishani mwake.Kila unachokifanya ambacho mwanao anakisikia ama kukiona kina uwezo wakumwathiri iwe kwa uzuri au kwa ubaya.Tukana hovyo na yeye ataona ni sawa(atleast UDOGONI...kipindi ambacho anafuata na kusikiliza maelezo yako karibu yote).

  Newayz mwisho wa yote ni kwamba avoid tabia ambazo sio nzuri mbele ya watoto.Na kubwa zaidi WAONYESHE UNAWAPENDA maana hicho bado ni kitendawawili kwa watu wengi.Kuwapenda mnawapenda ila kuwaonyesha ndo inakua ngumu.Pay attention to them,just as much as you are demanding from your partners.Na tabia ya kunyanyasa au kuwatreat watoto ambao sio wetu(awe wa ndugu au la)TUACHE.Nyanyasa wa mwenzio na wewe uje kunyanyasiwa.:rolleyes:   
 2. American lady

  American lady Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Du! lilsun kwa hapo napata kigugumizi.ila ninachoweza kusema tu wengine baadhi yetu tumekuwa na miungu kibao na miimani michafu.so kwa uzoefu wangu nimewahi kushuhudia case chache za aina hii lkn ukijaribu kuchimba mara oooh, nimeagizwa na Mganga.Jamani hawa waganga watatutuma tukazae ht na mama\baba zetu kwa kutokujua kuwa wale nao wanatafutia familia zao chakula pia.so haina maana tuwalaumu wanaume tu la hasha tutafute na undani zaidi.hakuna matapeli wakubwa km waganga wa kienyeji.mfano hai mm kuna anaeniendea kwa mganga tangu ninasoma almost 6yrs sasa ili nivurugikiwe mambo yangu lkn matokeo yake hakufanikiwa.sasa sijui huyo mganga wake wa kimasai anamsaidiaje utapeli mtupu.ndo hayo sasa yanawageukia wadogo zetu wewe baba wewe ungekuwa mzazi mwenye busara mwombe mwanao msamaa.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  My God mungu aepushe mbali sana
  Kama ameanza akiwa na miaka saba ,,kwanza alianza kumuharibu Binti kisaikolojia ili aone hakuna ubaya juu ya mambo yake ya ufirauni ,,hivyo Binti akaona ni sawa
  Lakini Baba au mama inawezekanaje ukawa na mapenzi na mwanao wa kumzaa ?
  nakosa la kusema hapa ..
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hiai imani zingine tunaziendekeza tu iweje mganga akuambie ufanye kitu ambacho yeye hawezi kukifanya?
  sijui kwanini mpaka leo watu tunaamini ushirikina
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  LilSun,

  Wanaume wengi wanawapenda sana watoto wao. Hizo case chache ama ni wagonjwa au kama alivyosema American Lady inaweza kuwa mambo ya kishirikina.

  Kila jamii ina jinsi ya kuwatendea watoto ambayo inadhihirisha kuwa wazazi wanawapenda hata kama hawawambii kizungu feki "I love you honey/sweetie". Lakini kuna watu hasa wa Mjini wamezidisha kile wanachoita mapenzi kwa watoto hadi inakuwa kama usanii. Baadhi ya wazazi wanajidai kuwaonesha watoto kuwa wanawapenda kiasi cha kuwaharibu. Tunahitaji balance ya kuwaonesha watoto kuwa tunawapenda na pia kutumia busara kuwalea ili wasiharibikiwe! Huu uchafu na ukatili kwa watoto ni vitu ambavyo vinatakiwa kushughulikiwa na vyombo vya dola na kila mtu kwenye jamii.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1, unawajuwa waganga wewe? Siku zote anakueleza kitu ambacho anajua kuwa ni chizi tu anaweza kufanya. Lakini kwa kuwa watu wanaoenda kwa waganga nao wana matatizo ndo maana wanafanya. Kuna kijana aliambiwa kuwa ili apate dhahabu machimboni basi amletee mganga jicho la mama yake mzazi. Mganga alijua kuwa kijana hatafanya. Kumbe kijana aliamua kumuua mama yake na mataokeo yake dhahabu akazifuata jela!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1, mwanaume hana haja ya kuwa na mapenzi na mwanamke kabla ya kufanya naye ngono. Akihitaji tendo la ndoa anatafuta kwa yeyote na ndo maana hata vichaa wanaolala kwenye mitalo wanazalishwa; tena na watu wenye heshima zao kwenye jamii. Akina mama wanatakiwa kulijua hili ili kuhakikisha watoto wao hawanajisiwi na baba zao au ndugu wa karibu.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  oooh my god inatisha
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  na nyie wanaume mnatisha kwa staili hiyo
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mi staki jamani
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndio maana tunaitwa wanaume na nyie ni wanawake! Kitu cha msingi ni kuuelewa huo ukweli na kuufanyia kazi. Binafsi najiamini lakini kila mara namsisitiza wife kuwa asimwamini mtu kwenye suala la boys wetu. Kwa hiyo awe macho na hata tabia zangu aziangalie kwa karibu. Binadamu ni mnyama wa ajabu sana. Kwenye suala la kutunza watoto hata mimi sitabweteka boys wangu wakishakuwa wakubwa kwani zipo cases za mama kuwaingiza watoto wao majaribuni. Inatia kinyaa ila ndo ukweli.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Huyo si mtu,
  hata ng'ombe hatembei na mwanawe wa kumzaa.
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  TRUE lakini its about time watu tujifunze.Utakua na akili gani kuamini kwamba mtu anaweza kukusaidia kupata kitu ambacho yeye kashindwa kujipatia???

  Huyo mzee ilivyofahamika bintiye ana mimba alianza kwakusema eti kuna mtu kamlogea hiyo mimba!!!!Baada ya mtoto kubanwa sana ndo akasema ukweli na mzee alivyoona moto umewaka akakubali.So hata hao wanaosingizia waganga utakuta ni ukatili 2 na upungufu wa akili ndo unaowaongoza!!!
   
 14. M

  Mende dume Member

  #14
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dark City, seconded! tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanabakwa na kunajisiwa na watu wanaowategemea kwa ulizi. baba, kaka, wajomba na walimu wao na hata rafiki za familia zao- rank ya baba, mjomba etc.

  FL1, Amrican Lady etc, kisaikolojia ni kuwa wanaume ni victim wa hate and limited love na impact yake ndo hii ya watoto, wanyama na vichaa kubakwa. haya matukio hayajitokezi au hujitokeza kwa nadra sana katika familia zenye upendo halisi. a slight hatred in ur family, ladies, is dangerous to the security of everybody in family- ndo haya mambo ya beheading a wife, rap, excessive beating, abusive languages. it is said that the impact can be generational. TUHUBIRI NA KUONYESHA UPENDO KTK FAMILIA ZETU, IT PAYS!
   
Loading...