Jamani huu ualimu mbona karaha namna hii?

Jamani huu ualimu mbona karaha namna hii?

goodhearted

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
1,021
Reaction score
1,268
Hizi mada za ualimu zimenigusa sana. ok mimi pia ni mwalimu katika halmashauli fulani. Mambo yanayonipata inafikia hatua natamani niachane tu na hii kazi

Ni hivi, baada ya kumaliza kujaza mikataba nilipostiwa kuanza kazi katika shule flani ya kata. Tulichokikuta huko sijawahi kukiona katika shule yoyote.

Aisee kwanza shule ilikuwa na walimu 7 tu ila maajabu mkuu wa shule ndo kila kitu, yeye ndo mtaaluma, mwl wa chakula na mengineyo mengi. Hakuna cha school balaza wala nini. Kwenye vikao yeye ndo msemaji mkuu na hakuna kupingwa.

Tumefight sana kuadjust lakini mwisho wa siku aligawa madaraka japo kwa shida sana lakini anapokupatia unakuwa huna full mandate na kitengo chako utafuatilia mpaka uone kero. Mfano mwl wa taaluma hana uwezo hata wa kwenda kuchapa mitihani yeye kazi yake ni kuandaa ratiba tu.

Mbaya zaidi amekaa muda mrefu kwa hiyo amewaaminisha wanafunzi na wazazi kuwa shule ni yake na hakuna mtu wa kumhamisha hivyo wanafunzi wanamheshimu yeye pekee, wanadharau walimu wengine utafikiri wanafunzi wenzao tu na ukiwaadhibu kama yeye hayupo basi akirudi watakusemea kwake na asivyo na busara utaitwa mbele yake kuhojiwa.

Hayo ni machache tu lakini kisa kikubwa kilicho nifanya niandike uzi huu ni hiki,,

Baada ya msuguano wa hayo yote walimu wote tulikubaliana kumwomba afisa elimu kuwa atuhamishie huyu mkuu ikiwezekana watuletee mwingine

Kwa shinikizo kubwa afisa elimu alituma "tume yake" kuja kuchunguza tulichokuwa tukipinga. Ilivyo ondoka tuliambiwa tutapewa feedback.

Cha ajabu ni kuwa siku ya kufunga mimi sikuwepo nilikuwa na matatizo hivyo nilikuwa na ruhusa. Habari waliyopewa ni kuwa mimi nimehamishwa kituo cha kazi na wengine watafuata. Na sitalipwa usumbufu wa aina yoyote ile kwa kuwa ni matatizo tumejitafutia sisi. Kwa hiyo gharama ya kusafirisha mizigo yangu itakuwa juu yangu, Mbaya zaidi aliwazuia walimu wezangu wasinipe taarifa hizi, japo kuna huyo mmoja kanipenyezia.

Yeye kama mkuu hajaniambia chochote hivyo ni kama chini ya kapeti.

Samahani kwa uzi mrefu wakuu, ila hapo nimejitahidi kufupisha na naombeni mchango wenu ,hivi ni kweli unaweza kuhamishwa kwa jeuri namna hiyo alafu ujigharamikie kwa uhamisho ambao hujauomba?? Kweli jamani??

Kama ni kweli nafikiria kuchukua maamuzi magumu...najua kitaa maisha ni magumu sana lakini.... HUU NI ZAIDI YA UONEVU

MAWAZO YENU TAFADHALI.
 
Pole ndugu yangu! Katafute Kazi private au njoo dar kajoin na wale jamaa wanaofundisha tuition mdogo mdogo mpaka unafungua tution Yako Ila target ni kua na Shule Yako ambayo finally kitakua Chuo! Mbona sisi wengine hatujaajiliwa serikalini na maisha yanaenda tu? Uoga wako ndo umasikini wako.
 
Hiyo mkuu wenu ni mjasiriamali tayari anajitambua bado nyie
 
Pole ndugu yangu! Katafute Kazi private au njoo dar kajoin na wale jamaa wanaofundisha tuition mdogo mdogo mpaka unafungua tution Yako Ila target ni kua na Shule Yako ambayo finally kitakua Chuo! Mbona sisi wengine hatujaajiliwa serikalini na maisha yanaenda tu? Uoga wako ndo umasikini wako.

ahsante kwa ushauli mkuu
 
Ulivokuwa unautafuta ualimu ulikuja kutuuliza!? Yakikushinda we ondoka kimyakimya mkuu, msipende kudhalilisha kaz za watu, maana wengine tumekuja mjini kwa kazi hii ebo!!
 
Ulivokuwa unautafuta ualimu ulikuja kutuuliza!? Yakikushinda we ondoka kimyakimya mkuu, msipende kudhalilisha kaz za watu, maana wengine tumekuja mjini kwa kazi hii ebo!!
Kumbe we bhang eee! Kweli kuna watu wapumba****v
 
Kama vipi acha kazi,kuna mtu alikufunga kamba ukasomee ualimu?,ualimu ndo unaniweka mjini mimi,we inaonesha ni mtu wa majungu sana
 
Haikosi wewe ni miongoni mwa wale walim wanaitwa "vodafasta", kijana acha kukurupuka ktk maisha, utakuja kuumbuka!
 
mkataba unasema ukihamishwa kituo cha kazi ni lazima wakupe hela ya kuamsha mizigo regardless any reason for transfer.... Dai chako mapema ......kama hawana nenda ngaz za juu kudai malipo yako
 
Yawezekana si ww si mkuu wako hamjui sheria ya kazi na mahsiano kazn so is better ukhama halafu anza kutafta y uhame
 
Mkuu pole kwa yaliyokukuta

Huko unakoenda fanya yafuatayo;

Using'ang'anie cheo sijui academic master au discpline master,kuwa ticha wa kawaida

Muda wako wa ziada utumie kufanya ujasiriamali,usipende pende sana kujikalisha maeneo ya shule.Kama hauna kipindi hiyo siku na kam hauko zamu usiende

Komaa na ujasiriamali katika eneo ulilopo na wala usiufanye ualimu kama baba au mama yako

Ukishaanzisha msingi imara,achana na hiyo kazi amabayo unaiona ni a kitumwa

Good luck
 
usihame bila kulipwa haki zako utakuwa umekubali kunyanyaswa . unatakiwa ulipwe kwanza ela ya kufunga mizigo ( disturbance allowance ) kabla ya kuondoka hapo ulipo na sheria inakutaka ulipwe wiki mbili kabla ya tarehe ya kuja kukuchukua . halafu subsistance allowance utalipwa pindi ukiwa kwenye kituo chako cha kazi kipya.
 
hizi mada za ualimu zimenigusa sana. Ok mimi pia ni mwalimu katika halmashauli fulani. Mambo yanayonipata inafikia hatua natamani niachane tu na hii kazi

ni hivi, baada ya kumaliza kujaza mikataba nilipostiwa kuanza kazi ktk shule flani ya kata. Tulichokikuta huko sijawahi kukiona katika shule yoyote.

Aisee kwanza shule ilikuwa na walimu 7 tu ila maajabu mkuu wa shule ndo kila kitu, yeye ndo mtataalu, mwl wa chakula na mengineyo mengi. Hakuna cha school balaza wala nini. Kwenye vikao yeye ndo msemaji mkuu na hakuna kupingwa.

Tumefight sana kuadjust lakini mwisho wa siku aligawa madalaka japo kwa shida sana lakini anapokupatia unakuwa huna full mandate na kitengo chako utafuatilia mpaka uone kero. Mfano mwl wa taaluma hana uwezo hata wa kwenda kuchapa mitihani yeye kazi yake ni kuandaa ratiba tu

mbaya zaidi amekaa muda mrefu kwa hiyo amewaaminisha wanafunzi na wazazi kuwa shule ni yake na hakuna mtu wa kumhamisha hivyo wanafunzi wanamheshimu yeye pekee wanadharau walim wengine utafkiri wanafunzi wenzao tu na ukiwaadhibu kama yeye hayupo basi akirudi watakusemea kwake na asivyo na busara utaitwa mbele yake kuhojiwa

hayo ni machache tu lakini kisa kikubwa kilicho nifanya niandike uzi huu ni hiki,,

baada ya msuguano wa hayo yote walimu wote tulikubaliana kumwomba afisa elimu kuwa atuhamishie huyu mkuu ikiwezekana watuletee mwingine

kwa shinikizo kubwa afisa elimu alituma"tume yake" kuja kuchunguza tulichokuwa tukipinga. Ilivyo ondoka tuliambiwa tutapewa feedback

cha ajabu ni kuwa siku ya kufunga mm sikuwepo nilikuwa na matatizo hivyo nilikuwa na ruhusa. Habari waliyo pewa ni kuwa mimi nhmehamishwa kituo cha kazi na wengine watafuata. Na sitalipwa usumbufu wa aina yoyote ile kwa kuwa ni matatizo tumejitafutia sisi. Kwa hiyo gharama ya kusafirisha mizigo yangu itakuwa juu yangu, mbaya zaidi aliwazuia walimu wezangu wasinipe taarifa hizi, japo kuna huyo mmoja kanipenyezia.

Yeye kama mkuu hajaniambia chochote hivyo ni kama chini ya kapeti

samahani kwa uzi mrefu wakuu, ila hapo nimejitahidi kufupisha na naombeni mchango wenu ,hivi ni kweli unaweza kuhamishwa kwa jeuri namna hiyo alafu ujigharamikie kwa uhamisho ambao hujauomba?? Kweli jamani??

Kama ni kweli nafikiria kuchukua maamuzi magumu...najua kitaa maisha ni magumu sana lakini.... Huu ni zaidi ya uonevu

mawazo yenu tafadhari.

subiri barua ije kwanza ili uwashughulikie kisheria.
 
Mkuu pole kwa yaliyokukuta

Huko unakoenda fanya yafuatayo;

Using'ang'anie cheo sijui academic master au discpline master,kuwa ticha wa kawaida

Muda wako wa ziada utumie kufanya ujasiriamali,usipende pende sana kujikalisha maeneo ya shule.Kama hauna kipindi hiyo siku na kam hauko zamu usiende

Komaa na ujasiriamali katika eneo ulilopo na wala usiufanye ualimu kama baba au mama yako

Ukishaanzisha msingi imara,achana na hiyo kazi amabayo unaiona ni a kitumwa

Good luck

Bonge la ushauri.Thanks
 
Pole mkuu Tanzania ni yetu ingawa imezunguwa na uozo uliokidhiri.
Unachotakiwa kufanya ni kupaza sauti popote ulipo lakini pia naamini Siku moja sauti yako itasikika.
Nakushauri usiache kazi kwani mhanga mkubwa ni mtoto/mwanafunzi.
 
Nenda CWT hapo ulipo wape madai yako ukitoka ingia TSD wape madai yako na utapewa taratibu za kufata ila kifupi huwez hamishwa bila kulipwa! Komaa tsd mpk kieleweke wakikusumbua zaid tafuta namba ya katibu mkuu CWT taifa mpigie na mweleze! Kwakuwa wameamua kupambana na weww na we pambana nao! Tatzo walim wengi huwa hamjui sheria za kazi zinazowalinda! Nakuapia ukikomaa watatengua uhamisho wako kwani hawana pesa za kuchezea kukulipa! Ukishindwa nifate private nikusaidie! Niko Tamisemi
 
Ushauri mzuri sana!
Ila.walimu punguzeni majungu kazini!
Acheni ulafi wa madaraka, madaraka hayaji kwa majungu!
Hiyo ndo shida alonayo.huyu mleta uzi!
 
kwanza pole sana ndugu yangu! hata hivyo kuna kitu kinaitwa "ugatuaji wa madaraka" nowdays wakuu wa shule wamepewa mamlaka kubwa na wanasikililizwa sana huko "halmashauri" jambo jingine ni kuwa HAKUNA UHAMISHO WOWOTE UNAOPEWA HALAFU UJIGHARAMIE MWENYEWE! labda uwe umeomba mwenyewe, kwa maana hiyo hata uhamisho wa adhabu unapaswa kulipwa stahiki zako ZOTE ikiwemo NAULI kabla hujahamia kituo kipya... usikubali narudia tena USIKUBALI kuhama bila kulipwa chako..... halafu pia usiache kazi maana ni kazi sana kupata kazi..... asante
 
Nenda CWT hapo ulipo wape madai yako ukitoka ingia TSD wape madai yako na utapewa taratibu za kufata ila kifupi huwez hamishwa bila kulipwa! Komaa tsd mpk kieleweke wakikusumbua zaid tafuta namba ya katibu mkuu CWT taifa mpigie na mweleze! Kwakuwa wameamua kupambana na weww na we pambana nao! Tatzo walim wengi huwa hamjui sheria za kazi zinazowalinda! Nakuapia ukikomaa watatengua uhamisho wako kwani hawana pesa za kuchezea kukulipa! Ukishindwa nifate private nikusaidie! Niko Tamisemi
hivi mkuu bado una imani na hawa wahuni CWT? kuna mwalimu yeyote unayemjua ambaye amesaidiwa na CWT?
 
ungeunga nae urafiki ungekula matunda ya kazi, sehemu yoyote ya kazi inachangamoto zake" kibaya ni pale mtu anapofatilia maisha yako tu ila haya mengine ni kutupa kule tu.
 
Back
Top Bottom