jamani Hospitali Mount Meru Arusha ni Hatari!

the-true-wash

Senior Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
142
Reaction score
109
Sikuwahi kukanyaga hospital hii tangu nizaliwe, leo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza. Hospital ni chafu, ya kizamani, vitanda na neti ni chafu sana, harufu mbaya ukiwa wodini, wagonjwa wamebananishwa na wengine wanakohoa na kutapika wanaangaliwa tu: mbaya zaidi kuna matangazo meengi ukutani wameandika TB inaenezwa kwa njia ya hewa! Ningekuwa na uwezo ningemuamisha mgonjwa niliyeenda kumtembelea. Hapa nilipo hata hamu ya kula imepotea. Pls pls pls serikali yetu fanyeni kitu juu ya hii hospital, pamoja na kwamba inaangaliana na majengo ya AICC na EA community lakini hali ni mbaya mbaya saaaana.
 

serikali ni nani?tatizo kila kitu lawama kwa serikali,je umeenda kwa uongozi wa hospital kuuliza shida ni nini?je wajua serikali inatoa fedha za ukarabati kwa hospital kila mwaka?makusanyo ya fedha ya kila siku ya hospital yanatumikaje.
fatilia kwa makini shida inaweza isiwe serikali ila watu wachache tu wasio waaminifu kwa rasirimali za nchi.
inabidi ujitahidi kula ili upate nguvu ya kwenda kuhoji kuhusu ili suala kwa uongozi wa hospitali.
 
kwa mtazamo wako unafikiri ni nani anapaswa kulaumiwa au kuwajibika kwa hilo!
 
mkuu mbona sasa hivi kuna mabadiliko makubwa sana,ungekuja mwaka juzi uone.
all in all mambo ya quality improvement katika hospitali yetu ni machanga mno hivyo tusilaumu sana.isitoshe kuna tatizo la fedha espicially katika hospitali za mikoa ni kama vile hazina mwenyewe.
 

mkuu ulifanikiwa kupita maeneo yote ya mt meru?nahisi kama umechora mstari kwa point moja!
 
Tanzania hatuna serikali. Tuna genge la wezi, wanyang'anyi, na wauwaji. Kazi yao ni kuiba, kufuja raslimali za nchi, kuonea wanyonge, na kujilimbikizia mali zisizo halali. Serikali hii imeshindwa kusimamia matumizi ya raslimali, idara maalumu na za msingi kama vile afya, elimu, ulinzi na usalama, mazingira, nk. Yuko wapi Kikwete anayechecheka wakati nchi inaangamia mchana kweupe? Polisi wamekidhiri hadi wanaanza kuchinjwa mitaani kama kuku. Iko wapi serikali? Madaktari walisema wanafanya kazi katika mazingira hatarishi bila dawa wala vifaa muhimu. Hawakusikilizwa wakagoma. Serikali ilimfanyia nini kiongozi wao? Je ni nini kimebadilika kuanzia wakati ule? Watu wangapi wanafia majumbani hasa kina mama na watoto kwa kushindwa kujifungua, kutoka damu nyingi kupita kiasi, kucheleweshwa kumwona daktari nk. Nchi imebaki siasa. Elimu, usafiri, matibabu ni siasa tu tena bila vitendo. Tanzania imegeuzwa kiwete kama sii dhaifu. Ole wake raisi wa awamu ya nne na serikali yake. Ole wao wanaowadhulumu na kuwaua raia wasio na kosa mchana kweupe kwa kuwanyima matibabu au kuwadhulumu haki zao kwa kuwa hawana mtetezi. Siku yaja na wote tutakufa tu. Hata wale wanaokomba kodi yote na kujitibu India, Ujerumani, Marekani, na kwingineko watakufa tu hiyo siku itakapowadia hapo tutawatangulia kwa kukosa matibabu. Mundu ibariki Tanzania.
 
kwa mijibu wa takwimu zilizopo wizara ya afya ni kuwa kati ya hospitali za mikoa mt meru iko juu katika suala zima la QI na QA(quality improvement and quality assuarance)
kama sasahivi umejionea haya hebu jiulize enzi za kinana!
 
kwa mijibu wa takwimu zilizopo wizara ya afya ni kuwa kati ya hospitali za mikoa mt meru iko juu katika suala zima la QI na QA(quality improvement and quality assuarance)
kama sasahivi umejionea haya hebu jiulize enzi za kinana!

Acha kudanganya watu..... ulishawahi fika Hospital ya ALMC? hakuna harufu.....hakuna Mbu.......hakuna mende.....huduma za ukakika hii utasemaje??
 
Acha kudanganya watu..... ulishawahi fika Hospital ya ALMC? hakuna harufu.....hakuna Mbu.......hakuna mende.....huduma za ukakika hii utasemaje??

ALMC sio hospitali ya mkoa!acha kukurupuka ndugu.......
 
Hii kero kubwa sana madaktari hawana morali wa kufanya kazi kutokana na mazingira vivyo hivyo kwa manesi ,vitendo vya rushwa ndio vimechukua nafasi bila kujali viapo ,na wadhifa ,ona wazazi wanaojifungua inafika mahali mgonjwa hana jinsi anaulizwa una shilingi ngapi tukupe maji ya uchungu usiteseke hushindwa kutamka ila vikizidi hutamka nesi njoo nina elfu tano nisaidie ,aidha apate msaada au akose hii ndio hali halisi kwenye hospitali nyingi ,tunahitaji kiongozi atakayeona hili na kulifanyia kazi na kuamsha morali wa kazi uliokufa wa wafanyakazi wengi wa serikali.tunahitaji kiongozi anayeona hali halisi ya watu wake na kukereka nayo ,na atakaye thubutu kuchukua hatua dhabiti na kwa wakati sahihi .
 
Yaani hiyo siyo hospital. bora uende kaloleni kuliko mt meru. kama aliejenga mzungu nadhani tangu ameondoka haijakarabatiwa.
 
Nilienda Mt.Meru wiki iliyopita wodi 6 ya wanaume,hali ni mbaya mnooo,nahisi mgonjwa anaweza kufikishwa hapo akazidiwa kutokana na mazingira yalivyo,nilivyorudi nyumbani nilioga kwanza maana nilihisi nina harufu kila mahali,kama mzalendo nitashawishi uchangiaji wa ukarabati,iliniuma saana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…