Jamani hebu nisaidieni huyu baba anataka kugombea ubunge

Da Sophy

JF-Expert Member
May 12, 2010
388
162
Nimemshauri hadi nimechoka. Namwambia aachane na biashara hiyo hanisikii. Kama jana almanusra nimmwagie maji ya deki kwa hasira alipoanza kunitajia eti sijui mambo ya elimu kwamba napishana naye kwa sababu ya elimu.

Nikamwambia rudi kwa mkeo akaufyata loh. Kwani anataka hata kumsikia?Jamani tuacheni masihara nisaidieni namna ya kumshauri aachane na mawazo haya nayaona ni ya hatari.
 
Mtu akisha aamua kujiingiza kwenye siasa ni ngumu kumshawishi aache. Cja msingi msupport na jitahidi kufanya kila uwezalo ili afanikiwe. Lakini angalia asitumie resources nyingi. Aepuke wapambe.
 
Mbona kama sijakuelewa, Tatizo ni yeye kugombea ubunge au Kuna jingine. Kama ni ubunge Kuna Tatizo gani maana hata shule tulienda bila kujali kama Kuna wengine walishindwa.
 
Kama anataka kufa kwa bp basi mwambie ajitose kwenye siasa ile ni kamari. Akawaulize waliotangulia akina masumbuko lamwai
 
Da Sophy

Huyu unayemshauri ni nani wako? Na anataka kugombea kupitia chama gani? Na unapoandika kitu jaribu kuwa makini ili ueleweke.Mtu ambaye hajawahi kuferi maana yake hajawahi kujaribu jambo lolote jipya, successful is always for risk takers with big heart.
 
Last edited by a moderator:
Huu mchepuko unaweza kukutia hasira mpaka ukaenda kushtaki kwa njia kuu.
Yaani ww ni shida
 
Nimemshauri hadi nimechoka. Namwambia aachane na biashara hiyo hanisikii. Kama jana almanusra nimmwagie maji ya deki kwa hasira alipoanza kunitajia eti sijui mambo ya elimu kwamba napishana naye kwa sababu ya elimu. nikamwambia rudi kwa mkeo akaufyata loh. Kwani anataka hata kumsikia?
Jamani tuacheni masihara nisaidieni namna ya kumshauri aachane na mawazo haya nayaona ni ya hatari.

Hii story Mbona kama imeanzia kati?
Au ni muendelezo wa ingine?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom