Hawa jamaa wananikera sana jamani,mchana kutwa ni kelele kiasi kwamba ukifika home jioni unasikia masikio yanatoa mwangwi wa sauti.ila kuna kitu naomba kuuliza wana JF,Hapa ninapofanyia shughuli zangu kuna kijana anafanya hizo kazi za kuingiza miziki kwenye simu.tangu aanze kazi hii kuna miezi 2.sasa huyu kijana namuna anabadilika siku hadi siku(kuchanganyikiwa)sijajua ni bangi au kuna uhusiano wa kutumia computer na kupiga mziki wa juu zaidi ya masaa 14 kila siku.naomba mwenye kujua hii kitu anisaidie ili nami niweze kumsaidia huyu dogo kabla hajawa "kichaa"kamili.