Jaman, jaman, jaman jf mambo??

Logo wako umalenga,umepuliza kipenga
vina mizani napinga,havikukaa kihenga
jaribu tena kupanga,kimaneno kuyalenga
karibu logo mpunga,tule sote tukiringa

Jidu hapo umenena, mizani yake sunami,
Malenga chekini vina, Logo mikono shavuni,
Kizazi kipya hakuna, ujapo umalengani,
Karibu Logo chumbani, Jamvi matata hakuna.
 
Naingia kwa furaha, ukumbini nakaribia.
Nimechungulia kwa karaha, nikiwa nje nilikaribia.
Sikuweza kula raha, nilipotaka kukoment sikuruhusiwa.
Lakini leo naingia, chochote naweza kuandika!

Kuna matatizo yalitokea, ofisini kwetu kuzozana.
Mwenzetu alifumaniwa, akifungua jamvi la JF.
Makamba alitupa, bila huruma kumwachisha ajira.
Iliniuma sana, ila leo nimeamua kuingia mwenyewe!

Nafurahia kitu kimoja, busara na hekima za JF.
Watu wenye uwezo wa kufikiri, na kujadili hoja mbalimbali.
Ukiwa na hasira utacheka, hasa ukiingia jukwaa na Jokes,
JF ni msaada hata kwa watafuta ajira!

Chamwisho wapendwa, naombeni mnipokee.
Nimo ndani ya nyumba, mengi nitayaeleza.
Vigogo wote wa serikali, hapa ndio kwao.
Nashukru kwa maana, wote wanaafahamu.
Mnipokeeeeeeeee Logoooooooooooooooooo naingiaaaaaaaaaaaaa.

..................logo karibu,..karibu hadi ndani.Mimi naitwa Mwenzetu
 
Back
Top Bottom