Jakaya Pilato! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya Pilato!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 28, 2012.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba ile kazi ya kubeba karai la maji, sabuni na taulo ili mtawala wetu Jakaya Pilato aendelee kunawa mikono na kukwepa lawama na kuacha kutimiza wajibu wake wa kufukuza watu kazi, kukaripia, kugombeza na kuhakikisha ufanisi na uawjibikaji unafanyika.

  Hii si mara ya kwanza kwa Kikwete kukimbilia "demokrasia" katika kufanya maamuzi ya ulazima kuinusuru nchi.

  Najiuliza, je siku tukiwa na janga la kutisha hata kuvamiwa, huku Uhuru na usalama wetu tunaojivunia kuwa ni murua je atafanya kazi yake na kuchukua uamuzi mgumu, ama kama kawaida yake atasakizia wengine wafanye uamuzi ili asilaumiwe?

  Yeye kuitwa Msanii, si kichekesho, yeye kuitwa mtalii si fahari, ni aibu kwa sisi kama Taifa kukubali kuwa na Rais na Mtawala asiye na utashi wa kufanya kazi yake na hasa pale inapobidi kuingilia kati kwa ajili ya manufaa ya Taifa.

  Suala la vidole gumba sabini pamoja na utata wake wa nia halisi na hata matokoe yake, bado limetuonyesha kwa mara nyingine udhaifu wa hali ya juu wa Rais aliyekuja kwa mbwembwe za Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya! Rais ambaye alijipatia nafasi ya kupigiwa kura kwa kutumia mfumo mchafu wa mtandao ambao badala ya kufanya kazi kwa kumuuza kama mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi na ndiye atakayeleta mapinduzi mapya, ukakimbilia kutumia mbinu chafu za hujuma na hata uharamia ulioandamana na ufisadi kumpa uwezo wa kuwa Rais.

  Je najiiuliza, hawa Mtandao walifanya makusudi wakijua kuwa wanampa kazi Pilato, ili lolote litakalotokea atanawa mikono na kutabasamu na kudai wengi wape?

  Ni aibu ya hali ya juu kuwa katika miaka 7 ya uongozi wake, Pilatro wetu hajawahi kufanya uamuzi wake binafsi wa makini na kwa manufaa ya Taifa.

  Alitamba na kujitapa kuwa yeye ni Rais wa Kwanza kuifanya ripoti ya ukaguzi wa mahesabu unaofanywa na CAG kuwa uko wazi kwa jamii na Taifa zima kuiona, lakini miaka 6 sasa tangu ripoti hiyo ijulikane machoni na masikioni mwetu, kila mwaka tunaambiwa ubadhirifu na ukosefu wa nidhamu wa hail ya juu katika matumizi ya serikali, lakini badala ya kufanyia kazi ripoti na kuhakikisha kuna nidhamu ya matumizi na mianya ya uhujumu na rushwa inaozaa ufisadi inazibwa, Pilato wetu kageuka mtalii kutembelea dunia kuitangaza Tanzania kwa wawekezaji.

  Kinachoudhi ni tabia yake ya kukaa kimya ama kwa makusudi au kukwepa kuonekana mbaya, pale inapodhihirika wazi inabidi aingilie jambo kwa nguvu zake zote.

  Mfano, wakati wa mgomo wa Madaktari mwanzoni mwa mwaka, hakuona jambo hili ni la muhimu kuwa maisha ya watu yalikuwa hatarini, maisha ya wale waliompigia kura na kumpa ridhaa na hatamu za kuongoza nchi. Yeye akaacha mpira ukidundadunda weee, bila kuingilia kati wala kuwaita madaktari ama hata kuwasihi na kuwaomba warudi kazini na kuwa atafanya mchakato nao ili kufuatilia malalamiko yao.

  Pilato akakaa kando kwa wiki kadhaa, hakujihusisha. Lakini kwa kupenda kusifiwa kwa yale ambayo kwangu si ya ulazima wa wajibu wake kama Rais, palipotokea msiba wa Msanii Kanumba, alikuwa mstari wa mbele kwenda kwenye msiba na kuwafariji wafiwa.

  Sasa jiulize, ya muhimu anayaweka kando na kuyapuuzia, miaka nenda miaka rudi, lakini yale yasiyo ya msingi kama kutembelea mashamba ya nyanya Brazil, huyapenda na hafikirii mara mbili kupanda ngalawa na kwenda kutalii!

  Sasa kama huyu si mhujumu wa cheo na dhamana ya Urais wa Jamhuri yetu, je yeye ni nani? mwanasesere, kikaragosi, kinyago au ni kitu gani?

  Lakini haiba yake nilishaiona awali na kuandika sana. Lakini kinachonishangaza ni jinsi Watanzania wanavyoendelea kuwa na Imani naye kuwa iko siku atafanya lile la msingi na maana!

  Lowassa hakufukuzwa kazi, alijiondokea! Hata msukumo wa kumfanya Lowassa aache kazi haukutoka kwake, bali ulitoka kwa Wabunge. Karamagi, Chenge, Msabaha, Meghji na wengine wengi ambao inajulikana walishindwa kazi, hakuwafukuza, bali waliondoka kwa hiari yao na wanaendelea kuwa Wabunge an wajumbe wa Halmashauri kuu na kamati kuu za CCM.

  Tulipobaini wizi na hujuma ya hali ya juu imefanyika Benki Kuu, hakuamka na kukasirika, bali ni msukumo wa Wananchi na wabunge ndio uliosababisha kukafanyika uchunguzi.

  Wananchi walipoanza kuhoji dhahabu yetu na mikataba ya madini si kwa manufaa ya Taifa, alikaa kimya mpaka pale alipoona maji yanakaba koo na badala ya kufanya uamuzi, akaunda tume imshauri!

  Sasa najiuliza, je CCM ni chama makini kweli kwa kuwa na Mwenyekiti na Rais ambaye anakwepa wajibu wake? Je atamkaripia nani kama yeye ni mzembe na mvivu?

  Itawezekanaje kwa Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM au Rais wa Tanzania kuongoza na kuvuna ufanisi na uwajibikaji kwa anaowaongoza ikiwa yeye ni mkwepa kuchafuka na anakaa kizembezembe na kuonekana anakwepa wajibu?

  Basi fagio la chuma limpitie yeye, maana hawajibiki!

  Nami nanawa mikono!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,547
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  ...Umepotea sana Rev, natumai umzima wa afya. Sidhani kama kuna la maana lolote litakalotokea hata baada ya kutangazwa baraza jipya la Mawaziri kwa sababu tatizo kubwa la Serikali hii ni Kikwete. anawaeza kubadilisha baraza la mawaziri hata kila mwezi lakini kama yeye mwenyewe ataendeleza usanii na kutowajibika kkama kiongozi wa nchi basi hakutakuwa na jipya.
   
 3. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawana jipya hawa jamaa wa magamba
   
 4. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  Siku zote huwa najiuliza; Kikwete ni Dk. wa nini? Kama utawala kwa kweli hapa ni ziro pengine wangesema utawala mbovu, porojo, uzembe, kucheka bila sababu, sawa hapa nakubali!
   
 5. C

  Christ Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Katika vitu vyote kikubwa sana kilichonishangaza ni pale mkuu wa nchi aliporudi toka Brazil(ziara ya kikazi)akawahi msiba wa Major Jenerali.Baada ya kuuaga mwili tu akapanda pipa kuelekea Blantyre kumzika Raisi Bingu.
  Hapa sasa:Je haikuwa busara kumtuma veep akamwakilishe msibani?Bunge wakati huo lilikuwa limewaka moto kwelikweli.Maswala yaliyokuwa yanajadiliwa ni nyeti na yenye kuhatarisha usalama wa taifa!
  Raisi wangu jaribu kuangalia ni lini utoke nchini na ni lini usitoke.Wananchi wanakutafsiri visivyo au vilivyo.Unapaswa kuwaonyesha kwamba wewe uliwaomba kura uwatumikie na sio wakutumikie,uwafikirie na sio wakusaidie kufikiria.
  TUNAKUPENDA ILA TAFADHALI BADILIKA.
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Sikio la kufa, lilishakufa hata dawa hakuna haja kumpa!
   
Loading...