Jaji wa New York amesema Trump arudishe dola milioni mbili alizochukua kwa ajili ya Kampeni za 2016

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Jaji wa jimbo la New York ameamuru Rais Donald Trump azirudishe dola milioni mbili alizozichukua kwa matumizi yanayotajwa na mahakama kuwa ni kinyume cha sheria.

Fedha hizo ni kutoka mfuko wa misaada wa 'Trump Foundation', ambapo inadaiwa kwamba alizichukua na kuzitumia katika kampeni zake kwenye uchaguzi wa mwaka 2016 uliomuingiza madarakani.

Uamuzi huu ni sehemu ya mashitaka yaliyowasilishwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Jimbo la New York dhidi ya mfuko wa misaada wa 'Donald J Trump Foundation' akiwemo rais mwenyewe na watoto wake watatu Donald Junior, Ivanka na Eric.

Mahakama pia imeelekeza watoto wa rais Trump wanaosimamia uendeshaji wa mfuko huo kupatiwa mafunzo ya uongozi na kujua namna ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha kwa misingi inayokubalika kisheria.
"Donald Trump Jr, Eric Trump na Ivanka Trump - ambao pia walikuwa wakurugenzi wa Trump Foundation - wanapaswa kupata mafunzo ya lazima kuhusu majukumu ya kuwa watendaji na wakurugenzi wa mifuko ya misaada", mwanasheria mkuu wa New York Letitia James alisema.

Kutokana na uamuzi huo wa mahakama, rais Trump ametakiwa kukiri waziwazi juu ya matumizi mabaya ya fedha za mfuko huo na kueleza kwamba wakati mwingine atazingatia masharti ya matumizi ya fedha za mfuko huo.

BBC
 
So wewe una akili sana yakubishana na judiciary system ya Marekani sio?
huyu jamaa kawashika pabaya!!.
sio kuangaika uku!!!.
changamoto anazopitia DT zinanifundisha kitu kikubwa sana katika maisha yangu, trust me ilo nalo litapita na jingine litakuja na bado atashinda.
 
So wewe una akili sana yakubishana na judiciary system ya Marekani sio?
hakuna pahari nimesema ilo, ila nashawishika kuaimini kwamba"tuhuma nyingi zinazomlenga Trump zinapikwa na demo"..
mahakama ina sehem yake katika ili lakini ilo litapita kama tuhuma zingine zilivyopita.

Trump texers, unfit, racit, storm daniel, obstruction ets yameendelea kubaki kuwa hadithi za abunwasi.
acha tuone mwisho wake katika ili.
 
Trump anaendesha mambo kihuni. Mpaka sasa watu wengi sana waliojihusisha na Trump wapo jela au wana kesi zipo mahakamani. Tatizo sheria za marekani zinamkinga asiweze kushtakiwa na kutiwa hatiani. Ila Trump huenda atamalizia maisha yake mahakamani au jela kabisa. Time will tell.
 
Back
Top Bottom