Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.

=======

LEO TOKA MAGAZETINI (16th April, 2016)


20160416_042439.jpg
 
Tatizo mnaingiza uwongo mwingi na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wenye fikra pana wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.

Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea uwongo na udaku kwa faida ya ajenda zako;
Hivi huwa mnapata faida gani mnapoleta thread zenye hoja za uwongo au udaku?
 
Kwenye eneo la majeshi ni ngumu sana kutumbua majipu ndiyo maana hata CAG huwa hakagui sana kwenye eneo hilo na hasa JWTZ
 
Chonde chonde Magufuli kama unataka kuendelea na nafasi yako ya urais wa nchi hii, achana na mpango wako wa kuanzisha mahakama ya majizi kwani utaingia kwenye mgogoro na chama chako bure kwa kuwa majizi wote hutokea huko. Utakiua chama ama watakufukuza uanachama.
 
Tatizo mnaingiza uwongo na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.

Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea udaku kwa faida ya fikra zako;

Hivi huwa mnapata faida gani?

Unafahamu mkuu, kuna watu hivi sasa wanahangaika sana mara huku mara kule.
 
Thubutu! mkataba unaohusu familia ya mfalme na mtoto wake uwekwe wazi? lile limshamba toka Magu limeshasepeshwa
 
Nadhan mkataba unajulikana, " umesainiwa 2011 kusambasa vifaa vya alama za vidole katika vituo vya polis zaid ya 100, kwa jumla tsh billion 37"

Kama hataki uonyeshwe, basi ajibu maswali ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi, kwanin zimeshatumika billion 34 kwa vituo 14 pekee..?!
 
Back
Top Bottom