Jaji ramadhani-uchaguzi mkuu 1995 ulihujumiwa

Jaji ramadhani-uchaguzi mkuu 1995 ulihujumiwa

joka57

Senior Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
138
Reaction score
49
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyosimamia uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa wa vyama vingi vya siasa wa mwaka 1995, Jaji Augustino Ramadhani, amesema kwamba uchaguzi huo katika jiji la Dar es Salaam ulihujumiwa.

Jaji Ramadhani alibainisha hayo katika mahojiano maalum na NIPASHE nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, baada ya kuulizwa kile ambacho hatakisahau katika kipindi chake cha utumishi alipokuwa NEC.

“Kitu ambacho sitakisahau nilipokuwa makamu mwenyekiti wa NEC ni ule uchaguzi wa kwanza wa Multipartism (vyama vingi) Dar es Salaam, mwaka 1995,” alisema.

Jaji Ramadhan alisema wote waliokuwa katika tume hiyo hawatausahau uchaguzi huo kutokana na kwenda kinyume cha walivyokuwa wamepanga.

“Tuliamka asubuhi na mapema kwenye kama saa kumi na mbili, tukaenda kwenye vituo vyetu tukapiga kura na baada ya kupiga kura tukakutana na kugawana majimbo kwa ajili ya kwenda kuyasimamia,” alisema Jaji Ramadhani.

Alisema jimbo lake lilikuwa Ukonga, huku viongozi wengine wa tume wakienda katika sehemu nyingine za majimbo saba ya mkoa wa Dar es Salaam.Alisema mpaka alipofika Ukonga hadi saa nane mchana Magereza Shule ya Msingi palipokuwa na vituo saba, alikuta hata kituo kimoja hakijafunguliwa kufanya kazi kutokana na kutowasili kwa vifaa.
“Nilikuta wengine kwenye vituo hivyo wana wino, wengine wana kalamu, wengine wana mihuri na hakuna hata kituo kimoja kati ya vituo saba kimefunguliwa pamoja na kwamba pale si shamba,” alisema Jaji Ramadhani.

Alisema baada ya kukuta hali ikiwa hivyo, waliwasiliana na kukubaliana kukutana kwenye ofisi ya tume na kuichambua hali hiyo na baadaye kugundua kuwa ilikuwa hivyo hivyo karibu jiji lote la Dar es Salaam.

“Tukakubaliana pale pale tufute uchaguzi wa Dar es Salaam, tulikaa pale mpaka saa nane za usiku huku tukinywa kahawa na biskuti tu, hata kule kuagizia lunch box hatukuagizia,” alisema.

Alisema walikubaliana wakapumzike ili wakutane tena kesho yake saa mbili ambapo walikubaliana kuufuta uchaguzi kwa majimbo yote ya Dar es Saalam.Alisema baada ya kuufuta uchaguzi huo, kazi yao ilibakia kuwa ni kuita mabalozi wa nchi mbalimbali ili kupata msaada wa kugharimia uchaguzi wa marudio kwa jiji la Dar es Salaam.

“Tukamuita Balozi wa Denmark ambaye yeye alitusaidia sana wakati wa maandalizi ya uchaguzi, akasema hana pesa, tukamuita Balozi wa Uingereza aliyetusaidia kupiga mashine ballot papers (karatasi za kura), ambaye alikubali kutoa msaada.

Alisema, Balozi wa Uingereza alitoa fedha za kuchapa karatasi za kura za udiwani, ubunge na rais.

“Nikasema alhamdulillahi sasa ikabaki sisi na serikali yetu tugombane kupata fedha za mambo mengine ndipo tukarudia ule uchaguzi, lakini siku ile kabisa sitaisahau na naamini ilikuwa ni hujuma,” alisema Jaji Ramadhani, ambaye hata hivyo, hakudokeza mtu au kikundi chochote walichohisi kufanya hujuma hiyo wala lengo lao.

Alisema hajui ni nani alifanya hivyo kwa sababu mwenzake aliyekuwa kwenye jimbo lililokuwa likijumuisha maeneo ya Magomeni, Kinondoni mpaka Ubungo, alikwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ambapo napo alikuta hakuna kinachofanyika.

Alisema baada ya kuamua kuuvunja ule uchaguzi, siku ya pili walikwenda kwa DC Magomeni pembeni wakakuta kuna karatasi za kura, si moja na kushangaa kwani siku ya uchaguzi karatasi hizo hazikuwapo.

Alisema hajui aliyehujumu na sababu zake na kuwa waliwaita wasimamizi wote wa uchaguzi na wakahojiana nao, lakini hakuna majibu ya maana waliyowapa.
“Wengine walisema ooh gari sijui ilikwenda ikapata pancha na yuko mmoja mwanamama alisema Jumamosi alikuwa kwenye harusi ya mtoto wake, kwa hiyo Jumapili akaamka na uchovu wa harusi, hatukuwa na la kufanya,” alisimulia Jaji Ramadhani.

Alisema baada ya kuamua kurudia uchaguzi huo mkoani Dar es Salaam baada ya wiki mbili, walitumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo ndilo lililotoa magari na walipeleka vifaa na kufanikiwa kwa sababu Jeshi lina nidhamu.
CHANZO: NIPASHE
 
huko ni kuhujumiwa au ni uzembe wa tume yenyewe?
 
Siku zote mlikuwa wapi hata leo mnajikosha kwenye kadamnas ili iwe nini na maji yakimwagiga hayazoleiki lakini yote kheri
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa
 
Nani Anaweza Kuhujumu Uchaguzi Mkuu Na Kuisababishia Serikali Hasara Isipokuwa Bingwa Wa Ujambazi Ccm?Nakumbuka Brig Nnauye Alikuja Kunduchi RTS Kuomba Recruits Waandikishe Wapigakura Kwa Sababu Watu Hawakulipwa Posho Wakatoroka Na Vifaa
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa

Umekunywa viroba vingapi leo? Siyo lazima ukomenti hasa ukiwa umelewa!
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa
Wewe ni mdini na mkabila, kwahiyo unataka vyombo vyote vya habari za zinazopendeza ccm tu, we utakuwa mchawi make una wivu na wachaga, utafikiri wao ndio wamefanya uwe mjinga Wa akili!
 
mwaka huo nilikuwa udsm mwaka wa mwisho....masanduku ya kupigia kura yaliletwa na wasimamizi wa vituo kwa miguu kutoka Magomeni mapipa. CCM haikuleta wasimamizi wa kura zao hapo chuoni, na kura zilianza kupigwa saa saba mchana. kulikuwa na upungufu mchubwa wa vifaa kama vile karatasi za kupigia kura, fomu za kujazia matokeo nk. Naikukbuka kauli ya Prof. baregu tulipokuwa pale utawala ."....kama chuo kikuu hali ni hii na kipo kilomita 15 tu kutoka ofisi za tume ya uchaguzi, je nyumbani kashozi hali iko vipi".

Jaji Ramadhani hataki kusema ukweli wote aliye hujumu uchaguzi huo ni serikali yenyewe kwa kushirikiana na wakurugenzi wa wilaya pamoja na ccm. Kwanini ccm? Siku moja kabla ya uchaguzi wenyeviti wa ccm wa vijiji (nazungumzia kata yetu huku kwetu) walizunguka katika familia zote za wanaccm na kuwaambia wawahi alfajiri na mapema kupiga kura kwani karatasi ni chache. wenyeviti walipeleka tathmini ya idadi ya wanaccm waliojiandikisha kwa WEO na WEO walipeleka makaratasi kulingana na idadi hiyo na ziada kidogo. Hivyo siku ya kupiga kura wanaccm walikuwa mbele wakapiga kura na karatasi zikaisha, wengine wakaambiwa wasubiri karatasi zinakuja kutoka wilaya...watu walikata tamaaa na kuondoka na mchezo ukakamilika.

Marudio ya Uchaguzi wa Dar, ilikuwa ni vitimbwi kwa kwenda mbele...ITV ilikwa ndo ina kama mwaka mmoja na ziada, ilianza kampeni ya kuogopesha watu kuwa wapinzani wataleta vita. kikaanzishwa kipindi maalum cha mauaji ya Rwanda hapo watu wazima tukajuwa kinacho tafutwa ni nini...Lwamwai alipita kwa sababu ya Wanafunzi wa udsm.....kuna mengi mno nyuma ya pazia, sa baadhi ya wazee wanatuambia ulweli kwa kutumia njia za kikubwa...Hivi nani anayeweza hujumu uchaguzi kwa kiasi kile na asichukuliwe hatua kama sio serikali na taasisi zake yenyewe? Hapa ni TISS na POLICCM wanahusika kwa karibu
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa

usilaumu ippmedia hi yo ndivyo ilivyokuwa !
 
Habari ni habari lakini habari hii haitusaiidii kwa sasa, angeitoa mwaka 1996 ingesaidia kuzuia hujuma mwaka 2000!
 
Jaji Ramadhani hataki kufa na kinyongo moyoni anatukumbusha kuwa CCM watahujumu uchaguzi huu wa serikali za mitaa na ule mkubwa, la kujiangalia ni sisi wananchi tumejiandaaje kuhakikisha tunaishinda dhuluma sasa hivi kuna hadithi kila siku eti kuandikisha sijui lini mwingine kesho mwingine kesho kutwa yote hii ni kukatisha tama wananchi
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa
we kama mwanaume basi shoga kama demu basi msagwaji
 
kwa maelezo hayo Sijaona hujuma , ni muendelezo tu wa IPPMEDIA kuishambulia serikali ya CCM na kudhani kufanya hivyo kunaweza kuiweka madarakani serikali ya kichagga , mambo kama haya hayana tija kwa taifa
Ndugu uko karne gani? Mbona bado unaendekeza ukabila? Wacha upuuzi.
 
Back
Top Bottom