kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
JAJI Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema mahakama nchini ziko huru, hazipendelei upande wowote wala kushinikizwa na mtu tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiri au wakati mwingine kupotosha.
Katika mahojiano ya kwanza tangu astaafu aliyoyafanya na magazeti ya Daily News na HabariLeo hivi karibuni, Jaji Othman alitoa mfano wa jinsi Mahakama ilivyoshughulikia kwa haraka kesi za uchaguzi wa mwaka 2015 uliokuwa na mvutano mkubwa.
Jaji huyo aliyefanya kazi za sheria nje na ndani ya nchi pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa, alieleza kuwa kesi za uchaguzi za ubunge na udiwani zimemalizika bila malalamiko ya upendeleo.
Hata hivyo, anasema bado mahakama ina changamoto nyingi ikiwamo kila mkoa kuwa na Mahakama Kuu, kuongeza idadi ya mahakama za mwanzo na uboreshaji wa miundombinu huku akisikitishwa na baadhi ya mahakama kutokuwa na umeme.
Jaji Othman ambaye alisoma sheria darasa moja na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, angependa kuona watendaji wa mahakamani wakipambana ili kuhakikisha wanamaliza kabisa mlundikano wa kesi.
Ukimuliza kitu anachokikumbuka zaidi, Jaji Chande anasema katika utumishi wake mahakamani hatosahau kesi ya mtoto aliyechunwa ngozi mkoani Mbeya iliyofikishwa mbele yake.