Jaji Mwesiumo asema Bunge limepoteza hadhi..!

Jaji Mwesiumo asema Bunge limepoteza hadhi..!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803




Mbunge wa zamani wa Kilombero, Jaji mstaafu Edward Mwesiumo, amesema Bunge la sasa limepoteza hadhi na mvuto wake kutokana na vitendo vya baadhi ya wabunge wanaolitumia kujitafutia umaarufu badala ya kulitumia kutatua matatizo ya wananchi.
​

​
​
​
​
​
​

Aidha, alisema lazima wabunge watambue kuwa uhuru na demokrasia iliyopo nchini haiwapi kibali cha kutoleana lugha za kejeli na kudhalilishana wenyewe kwa wenyewe bungeni kwani kufanya hivyo ni kujivunjia heshima mbele ya wananchi.​
​
​
​


​
​

Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanyika jana kwenye ofisi za gazeti hili, Mikocheni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Jaji Mwesiumo alisema kauli na vituko vinavyofanywa na baadhi ya wabunge bungeni inalipunguzia mvuto na heshima chombo hicho.


Jaji Mwesiumo ambaye pia aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alisema kwa mtazamo wake, hivi sasa wabunge wamekuwa wakitumia chombo hicho ambacho ni mhimili wa pili wa Tanzania kama ‘kijiwe’ cha kujitafutia umaarufu na sio kuwasilishia matatizo ya wananchi.


“Wabunge wa sasa wamekuwa wakilitumia Bunge kama sehemu ya kujitafutia umaarufu hivyo kutamka au kufanya kituko kwa kuamini watasikika na kuonwa badala ya kuwafikishia wananchi wao matatizo ili yatatuliwe na serikali,” alisema Mwesiumo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Wakulima Tanzania (Taso).


Alisema hata lugha ya kibunge kwa sasa imesahauliwa na baadhi ya wabunge na ndio maana imeshuhudiwa wakitukanana na kukejeliana kama watu wasio na heshima tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.


Aliongeza kuwa hata kama ni uhuru na kushamiri kwa demekrasia, bado wabunge wanapaswa kujiheshimu na kukiheshimu chombo hicho kwa kupingana kistaarabu na kubwa kuhakikisha matatizo ya wananchi wao yanawasilishwa na kutautiwa ufumbuzi kwa njia za kiungwana.


“Inapofikia mbunge anamkejeli kwa lugha isiyo na staha mbunge mwenzake au mbunge mwanasheria kumtusi mwanasheria mwenzake ni wazi nidhamu na hadhi ya Bunge inashuka, je wananchi walifikiriaje bunge la namna hiyo, nadhani ni wakati wa waheshimiwa hawa kubadilika ili kulirejeshea Bunge heshima yake,” alisema Jaji huyo aliyeitumikia Mahakama tangu mwaka 1974-1980 kabla ya kuwa mbunge wa Kilombero kwa awamu mbili za mwaka 1980-85 na 1990-1995.​

CHANZO: NIPASHE​

 

JUDGE MWESIUMO nadhani Wakati wa UBUNGE wako kulikuwa ni CHAMA KIMOJA TU BUNGENI; na Walikuwa Wabunge Wanamulikwa na BEAM; Walikuwa ni NDIO PRODIGY...

Sasa hivi ni DEMOKRASIA ya UKWELI wa VYAMA VINGI; BUNGE LETU BADO lina HESHIMA... Haujaona Wabunge wa UKRAINE;RUSSIA;INDIA wanavyotwangana BUNGENI?

Sasa hivi kuna TV nadhani unaangalia na kuona MABUNGE Mbalimbali DUNIANI
 
Hili siyo BUNGE la ndiyo MZEE. Namshauri ajaribu kuangalia mabunge mengine yenye mchanganyiko na upinzani kutoka nchi mbalimbali ajionee wtu wanavyokwidana.
 
Mheshimiwa jaji mstaafu bado "jana" ipo kichwani mwake. Hana budi kuamka ili aione "leo" amasivyo atajikuta yupo enzi za "pekosi"
 
bunge likishakua na vijana mjue hapo hakuna constructive arguments bali ni kashfa matusi na kukejeliana kama akina mwigulu wanavyofanya...generational differences ina play part sana
 
Ni kweli na sababu ni MAKINDA,NDUGAI na LUKUVI ila ningetegemea azungumze kuhusu MAHAKAMA pia uko ndio UOZO mkubwa.
 
Ndio faida za demokrasia Jaji. Hata wewe na mchango wako mwepesi lakini umepewa airtime na Nipashe. Heshima ni matokeo ya matendo na sio rangi.
 
kuna wazee wanataka kusababisha tuwadharau wazee wote wa nchi hii..
 
Ndivo ilivyo mara nyingi ukweli hasa ukisemwa kwa mtu ambaye fikra finyu zinafikiri kuwa aliyeambiwa ukweli hatakiwi kuambiwa ukweli waziwazi na ndipo msema kweli huambia kakosa heshima/hana adabu (kisa kasema ukweli peupe).

Mtazame kamanda Mnyika aliposema waziwazi kile alichonacho amri jeshi mkuu wetu kuwa ni dhaifu nini kilimpata aliishia kutolewa bungeni KWAMBA N MTOVU WA NIDHAMU. lakin kwa kuwa n kweli kesho yake alirudishwa bila mashart yoyote.

Hii ndo tz! bado mawazo mgando hayakwepeki, jukumu letu n kuendelea kukielimisha kizazi kipya huku tukiyayaweka kapun hayo mawazo mgando.
 
Ndio faida za demokrasia Jaji. Hata wewe na mchango wako mwepesi lakini umepewa airtime na Nipashe. Heshima ni matokeo ya matendo na sio rangi.

Mtamfanya asitoe tena maoni siku nyingine, punguzeni ukali wa maneno.!
 




Mbunge wa zamani wa Kilombero, Jaji mstaafu Edward Mwesiumo, amesema Bunge la sasa limepoteza hadhi na mvuto wake kutokana na vitendo vya baadhi ya wabunge wanaolitumia kujitafutia umaarufu badala ya kulitumia kutatua matatizo ya wananchi.



















Aidha, alisema lazima wabunge watambue kuwa uhuru na demokrasia iliyopo nchini haiwapi kibali cha kutoleana lugha za kejeli na kudhalilishana wenyewe kwa wenyewe bungeni kwani kufanya hivyo ni kujivunjia heshima mbele ya wananchi.

















Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanyika jana kwenye ofisi za gazeti hili, Mikocheni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Jaji Mwesiumo alisema kauli na vituko vinavyofanywa na baadhi ya wabunge bungeni inalipunguzia mvuto na heshima chombo hicho.





Jaji Mwesiumo ambaye pia aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alisema kwa mtazamo wake, hivi sasa wabunge wamekuwa wakitumia chombo hicho ambacho ni mhimili wa pili wa Tanzania kama kijiwe cha kujitafutia umaarufu na sio kuwasilishia matatizo ya wananchi.





Wabunge wa sasa wamekuwa wakilitumia Bunge kama sehemu ya kujitafutia umaarufu hivyo kutamka au kufanya kituko kwa kuamini watasikika na kuonwa badala ya kuwafikishia wananchi wao matatizo ili yatatuliwe na serikali, alisema Mwesiumo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Wakulima Tanzania (Taso).





Alisema hata lugha ya kibunge kwa sasa imesahauliwa na baadhi ya wabunge na ndio maana imeshuhudiwa wakitukanana na kukejeliana kama watu wasio na heshima tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.





Aliongeza kuwa hata kama ni uhuru na kushamiri kwa demekrasia, bado wabunge wanapaswa kujiheshimu na kukiheshimu chombo hicho kwa kupingana kistaarabu na kubwa kuhakikisha matatizo ya wananchi wao yanawasilishwa na kutautiwa ufumbuzi kwa njia za kiungwana.





Inapofikia mbunge anamkejeli kwa lugha isiyo na staha mbunge mwenzake au mbunge mwanasheria kumtusi mwanasheria mwenzake ni wazi nidhamu na hadhi ya Bunge inashuka, je wananchi walifikiriaje bunge la namna hiyo, nadhani ni wakati wa waheshimiwa hawa kubadilika ili kulirejeshea Bunge heshima yake, alisema Jaji huyo aliyeitumikia Mahakama tangu mwaka 1974-1980 kabla ya kuwa mbunge wa Kilombero kwa awamu mbili za mwaka 1980-85 na 1990-1995.​

CHANZO: NIPASHE​
RIP retired Judge Mwesiumo, kwa wanaomfahamu msiba upo nyumbani kwake Tabata, kesho wanasafirisha kwenda Ifakara
 
Back
Top Bottom